Wataalamu mbalimbali kutoka Mamlaka ya hali ya hewa wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Dkt Agnes Kijazi akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa wastaalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa kina mkutano huo uliofanyikia katika ukumbi wa Hotel ya Bluepearl jijini Dar es Salaam
MAMLAKA ya ali ya hewa nchini (TMA) imesema ipo katika mkakati wa kubadilisha mfumo wa kuhifadhi takwimu za hali ya hewa kutoka mfumo wa analogia kwenda digitali.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk.Agnes Kijazi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari na kufafanua kuwa katika kutimiza hilo walisaini makubaliano ya kushirikiana na ofisi ya hali ya hewa Uingereza ambapo mambo makuu ilikuwa ni kuhakikisha watumiaji wa huduma za hali ya hewa nchini wanaridhika na huduma zitolewazo lengo ikiwa ni kuboresha mfumo wa kuhifadhi takwimu.
“Kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni TMA imekuwa ikikutana na wadau wa Sekta mbalimbali na kupata maoni yao juu ya huduma zitolewazo pamoja na kubadilisha namna ya uhifadhi wa takwimu za hali ya hewa ambapo kwa kupitia maoni hayo tumeona ni wakati muafaka wa kuwakutanisha wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali ili kujadili na kupata suluhisho la kuboresha huduma zetu,”amesema Kijazi.
Aidha amesema katika mkutano huo ambao umewahusisha pia wakuu wa kanda kutoka TMA na wasimamizi wa vituo vya hali ya hewa vinavyoendeshwa na mamlaka vilivyopo nchini, washiriki watapata fursa ya kujadili na kutolea maamzi maoni ya wadau wa sekta ya kilimo, nishati, maji, afya na habari na pia kujipanga katika kuwafikia wadau wengine.
Ameongeza kuwa mbali na changamoto za uwepo wa taarifa nyingi za hali ya hewa zilizo kwenye makaratasi ambazo wanataka kuziweka katika mfumo wa kidigitali pia wanakibiliwa na ukosefu wa ofisi maalumu ya kufanyia kazi suala ambalo wanalishighulikia hivi sasa pamoja na upungufu wa wataalamu na vituo vya hali ya hewa ambapo kwa sasa wanavyo vituo 28 wakati malengo yao ni kuwa na vituo 70.
Kijazi amesema kuwa mara kwa mara wamekuwa wakitumia maoni wanayoyapata kutoka kwa wadau mbalimbali hasa wakulima kwa kuangalia mahitaji binafsi kulingana na sekta yao pale wanapotaka kufahamu vipindi vya mvua ili kujiandaa na shughuli za kilimo alikadhalika vipindi vya ukame.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni