Jeshi la Polisi Mkoa
wa Morogoro linawashikilia watu kumi kwa tuhuma za kukutwa na silaha za moto
zaidi ya 30 pamoja na milipuko.
Watu hao walikamatwa
leo eneo la msikiti wa Suni Kidatu
ambapo ndipo walipojifungia huku wameshika bendera yenye maneno ya kiarabu
yenye tafsiri ya Mungu ni mmoja pamoja na mavazi ya kijeshi.
Hata hivyo mmoja
ya watuhumiwa hao (Ahmad
Makwendo) alimjeruhi askari kwa kumkata na jambia eneo la shingoni wakati wa
purukushani za kuwakamata watu hao ambapo inasadikika walikuwa wakifanya
maandalizi ya ugaidi.
jeshi la polisi Mkoani Morogoro akionyesha vifaa vilivyokamatwa kutoka kwa watuhumiwa hao ni mavazi ya jeshi,milipuko na vifaa vya moto.(PICHANI JUU).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni