Jumanne, 14 Aprili 2015

LIPUMBA ASEMA SERIKALI IMESHINDWA

Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF mh Prof. IBRAHIM LIPUMBA akizungumza na viongozi wa Chama hicho pamoja na wanahabari wakati akifungua kikao baraza kuu la Uongozi la Taifa la Chama hicho leo makao makuu jijini Dar es Salaam.kulia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho MAALIM SEIF SHARIF HAMAD,na kushoto ni makamu wa rais wa chama hicho zanzibar JUMA DUNI HAJI

Chama cha Wananchi CUF kimesema kuwa ni ukweli usipingika kuwa kwa sasa Serikali ipo taabani kutokana na mambo mengi yanayotokea huku serikali ikiwa haitoi majibu yanayowaridhisha wananchi jambo ambalo limewafanya Watanzania kukata tamaa na Nchi yao.
Akifungua kikao cha kawaida cha baraza la uongozi taifa la chama hicho mwenyekiti wa CUF Mh. Ibrahim  Haroun Lipumba amesema kuwa swala la   uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na mchakato mzima wa upigaji kura imeonyesha wazi kuwa Serikali ya Tanzania imeshindwa kufanikisha zoezi hilo huku ikiitupia mzigo wote tume ya Taifa ya uchaguzi ambayo na yenyewe imeshindwa.Amesema kuwa kushindwa kumalizika kwa uandikishwaji wa daftari hilo kwa muda uliopangwa ni jambo ambalo lilikuwa haliepukiki kwani vyama vya upinzani pamoja na wadau mbalimbali walishaitahadharisha serikali juu ya mchakato huo lakini serikali ilishindwa kusikiliza kilio chao na matokeo yake mchakato huo umeshindwa kufanikiwa.
Amesema kuwa moja ya ajenda za kikao hicho cha baraza kuu la uongozi la Chama hicho ni pamoja na kujadili maswala hayo yanayohusiana na kushindwa kufanikiwa kwa daftari hilo la wapiga kura na kujadili nini cha kufanya ili uchagauzi uweze kufanyika na pia ufanyike kwa amani na upendo.
Aidha Prof. Lipumba amesema kuwa serikali ya Tanzania imeshindwa kuwa sikivu kwa Wananchi wake ambao ndio waliowaweka madarakani, huku akitolea mfano sakata la migomo ya wafanyabiashara,madereva na mambo mengine yanayoendelea ambapo amesema badala ya serikali kukaa chini na watu hao ili kuwasikiliza imekuwa kinyume kwani wamekuwa wakitumia ubabe na kuwaacha walalamikaji hao kukosa la kufanya.
Picha  juu ni baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho kilichoanza leo jijini Dar es salaam

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amesema kuwa kikao hicho cha kawaida cha baraza kuu la uongozi taifa ambacho  kitajadiliana kwa siku mbili mfululizo  pamoja na mambo mengine watajadili muungano wa chama chao pamoja na vyama vingine vya upinzani umoja uliopewa jina la UKAWA pamoja na kujadili ni jinsi gani ya kuimarisha umoja huo kuelekea uchaguzi ujao mwishoni mwa mwaka huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni