Pichani Katibu Mkuu wa Wizara ya ujenzi Eng.Mussa Iyombe(katikati)
Jumapili, 19 Aprili 2015
TEMESA KUWEKA NGUVU KATIKA SOKO LA USHINDANI NCHINI
Pichani Katibu Mkuu wa Wizara ya ujenzi Eng.Mussa Iyombe(katikati)
Akizungumza na Menejimenti ya TEMESA jijini Dar es salaam
leo, Eng. Iyombe amesisitiza Wakala huo kuwa na wafanyakazi wenye weledi,
waliokabidhiwa mamlaka kamili na wabunifu ili kuhuisha huduma zinazotolewa kwa
wananchi na kujiongezea mapato.
“Hakikisheni mnatumia
wataalamu mlionao kuleta tija kwa Wakala na kwa Serikali kwa ujumla ili mfikie
malengo yenu na kuipunguzia Serikali mzigo wa kuwahudumia”, alisisitiza Eng.
Iyombe. SOKO LA USHINDANI
Aidha Eng. Iyombe
ameagiza TEMESA kuimarisha uhusiano wake na jamii hasa sekta binafsi ili
kubadili mtazamo uliopo sasa kuwa Wakala huo unatengeneza magari ya Serikali
peke yake na hivyo kushindwa kuteka soko la sekta binafsi.
Kwa upande wake Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) Eng. Marceline Magesa
amemshukuru Katibu Mkuu kwa kuwapatia vifaa mbalimbali na mitambo na kuahidi
kuwa vitatumika vizuri ili kuimarisha utendaji kazi wa TEMESA.
“Asilimia 100 ya
mapato kwa baadhi ya mikoa tunayaacha mikoani ili kufufua mitambo iliyoko na
kuboresha huduma za Ufundi, hivyo tumieni fursa hii kubuni miradi mingi ya
kuongeza mapato”, amesema Eng. Magesa.
Ubunifu, kujitangaza
na kutoa motisha kwa wafanyakazi inachangia ari ya kufanya kazi ambapo TEMESA
mkoa wa Pwani na Tanga imeelezwa kufanya vizuri na hivyo kuhudumia taasisi
mbalimbali binafsi na za umma.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni