Jumanne, 21 Aprili 2015

TMA YALENGA KUKIDHI MAHITAJI KATIKA SEKTA MBALIMBALI NCHINI

 

 

 Wataalamu  mbalimbali kutoka Mamlaka ya hali ya hewa wakiwa katika picha ya pamoja.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Dkt Agnes Kijazi akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa wastaalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali.

Baadhi  ya washiriki wakifuatilia kwa kina mkutano huo uliofanyikia katika ukumbi wa Hotel ya Bluepearl jijini Dar es Salaam


MAMLAKA ya ali ya hewa nchini (TMA) imesema ipo katika mkakati wa kubadilisha mfumo wa kuhifadhi takwimu za hali ya hewa kutoka mfumo wa analogia kwenda digitali.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk.Agnes Kijazi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari na kufafanua kuwa katika kutimiza hilo walisaini makubaliano ya kushirikiana na ofisi ya hali ya hewa Uingereza ambapo mambo makuu ilikuwa ni kuhakikisha watumiaji wa huduma za hali ya hewa nchini wanaridhika na huduma zitolewazo lengo ikiwa ni kuboresha mfumo wa kuhifadhi takwimu.

“Kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni TMA imekuwa ikikutana na wadau wa Sekta mbalimbali na kupata maoni yao juu ya huduma zitolewazo pamoja na kubadilisha namna ya uhifadhi wa takwimu za hali ya hewa ambapo kwa kupitia maoni hayo tumeona ni wakati muafaka wa kuwakutanisha wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali ili kujadili na kupata suluhisho la kuboresha huduma zetu,”amesema Kijazi.

Aidha amesema katika mkutano huo ambao umewahusisha pia wakuu wa kanda kutoka TMA na wasimamizi wa vituo vya hali ya hewa vinavyoendeshwa na mamlaka vilivyopo nchini, washiriki watapata fursa ya kujadili na kutolea maamzi maoni ya wadau wa sekta ya kilimo, nishati, maji, afya na habari na pia kujipanga  katika kuwafikia wadau wengine.

Ameongeza kuwa mbali na changamoto za uwepo wa taarifa nyingi za hali ya hewa zilizo kwenye makaratasi ambazo wanataka kuziweka katika mfumo wa kidigitali pia wanakibiliwa na ukosefu wa ofisi maalumu ya kufanyia kazi suala ambalo wanalishighulikia hivi sasa pamoja na upungufu wa wataalamu na vituo vya hali ya hewa ambapo kwa sasa wanavyo vituo 28 wakati malengo yao ni kuwa na vituo 70.

Kijazi amesema kuwa mara kwa mara wamekuwa wakitumia maoni wanayoyapata kutoka kwa wadau mbalimbali hasa wakulima kwa kuangalia mahitaji binafsi kulingana na sekta yao pale wanapotaka kufahamu vipindi vya mvua ili kujiandaa na shughuli za kilimo alikadhalika vipindi vya ukame.

Amesema mbali na wakulima kutaka kupata taarifa za misimu ya mvua pia huhitaji kujua vipindi vya upepo mkali ili kuweka tahadhari kwa ajili ya kulinda mimea kama migomba na matunda kwa kuweka miti ili isianguke ukiachana na taarifa za jumla kwa ajili ya watu mbalimbali ambazo hutolewa na dawati lao.

Jumapili, 19 Aprili 2015

POLISI WAVAMIA VITUO VYA MAFUNZO YA DINI YA KIISLAM DODOMA.


Jeshi la polisi Mkoa wa Dodoma limeweka chini ya ulinzi na kufanyia uchunguzi vituo vitatu vilivyokusanya watoto 115 kutoka mikoa 13 Nchini kwa lengo la kuwapatia mafunzo ya dini ya kiislamu.

 

Vituo hivyo vyote vipo katika eneo la Nkuhungu,lililopo katika manispaa ya Dodoma.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alisema wanafanya uchunguzi katika vituo hivyo kutokana na kuhusika  kuendesha vituo vya kulelea watoto bila kusajiliwa na hatarishi.

 

"Jana saa saa sita usiku tulifanya upekuzi katika vituo vitatu,katika kituo cha kwanzatukafanikiwa kupata watoto takribani 63,kati yao 46chini ya miaka 18.

 

Katika  kituo cha pili tulikuta watoto 40,kati yaowalio chini ya umri miaka 18 walikuwa 12 na kituo cha tatu tulikuta  watoto saba  ,kati yao walio chini ya umri miaka 18 ni watano".Alisema Misime.

 

Alisema katika idadi watoto hao,63 wana umri chini ya miaka 18 na wengine 52 umri wao ni miaka 25,na wote ni wanaume wengi  wanatoka Wilaya ya Kondoa ambao ni 50 na 26 wanatokea katika \wilaya ya Dodoma mjini,Chamwino na Mpwapwa.

 

"Watoto wanaosalia wanatokea  mikoa ya Kagera,Dar es Salaam,Kilimanjaro,Zanzibar,Tanga,Tabora

Singida,Pwani,Lindi,Mtwara,Geita,Mwanza na Manyara".Alisema Misime.

 

Alisema watoto hao walikutwa usiku wakiwa wamechanganywa bila kujali umri wao,jambo ambalo ni hatarishi.

 

"Uchunguzi unaendelea na yeyote atayeguswa na ushahidi kuwa amekiuka sharia,atafikishwa mahakamani ikiwepo wazai walioruhusu watoto hao kuwa katika uangalizi amao si wa kutosha kama sharia ya motto ya mwaka 2009 inavyoelekeza".Alisisitiza Misime.

 

Akizungumzia tukio hilo,Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mustafa Rajab,alisema hakuna dhambi yeyote kwa watoto hao kulelewa katika kituo hicho.

 

"Hayo ni mafunzo katika madrasa  ambazo zilianza zamani ulimwenguni kote,polisi haina mamlaka ya kufunga madrasa labda kama watakuta kuna tatizo lolote la kuhatarisha amani"Alisema Rajab.

 

Walikizungumza katika eneo hilo,baadhi ya watoto walisema wapo hapo kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya dini ya kiislam

 

" Mimi nimetoka Kondoa lakini nilipokuja hapa nimeandikishwa Shule ya msingi Nkuhunhu,nikimaliza kusoma dini hapa huwa nakwenda shuleni".Alisema mmoja wa watoto hao

 

Mmoja wa majirani Mama Naomi alisema siku zoteamekuwa akiwaona watotro hao wakishinda hapo na hajawahi kuwaona wakienda shule kusoma.

 

"Chakula na kuni za kupikia huwa wan aletewa na walimu wao,wanajipikia wenyewe,watoto wadogo kazi yao ni kuosha vyombo."Alisema Mama Naomi.

.









 

LOWASA AUNGANA NA WANANCHI KATIKA MATEMBEZI YA KUPINGA MAUAJI YA ALBINO

 




 



 Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye pia ni Munge wa Monduli akiongoza matembezi  matembezi hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Matembezi hayo yaliyoandaliwa na vijana wa TEMEKE yaliyoanzia katika uwanja wa Taifa na kumalizika katika viwanja vya  TTC Changombe jijini Dar es Salaam



 



Baadhi ya Wananchi waliojitokeza katika kuunga matembezi hayo ya kulaani na kupinga mauaji ya albino. jijini DAR ES salaam.



Mheshimiwa Lowassa akiwa pamoja na baadhi ya Wananchi katika matembezi hayo.



TEMESA KUWEKA NGUVU KATIKA SOKO LA USHINDANI NCHINI


Pichani Katibu Mkuu wa Wizara  ya ujenzi Eng.Mussa Iyombe(katikati)
 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe amezungumzia umuhimu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) kutangaza huduma wanazozitoa kwa Wananchi ili jamii iweze kunufaika na huduma hizo kwa wakati na  gharama nafuu.

 Akizungumza na Menejimenti ya TEMESA jijini Dar es salaam leo, Eng. Iyombe amesisitiza Wakala huo kuwa na wafanyakazi wenye weledi, waliokabidhiwa mamlaka kamili na wabunifu ili kuhuisha huduma zinazotolewa kwa wananchi na kujiongezea mapato.

“Hakikisheni mnatumia wataalamu mlionao kuleta tija kwa Wakala na kwa Serikali kwa ujumla ili mfikie malengo yenu na kuipunguzia Serikali mzigo wa kuwahudumia”, alisisitiza Eng. Iyombe. SOKO LA USHINDANI

Aidha Eng. Iyombe ameagiza TEMESA kuimarisha uhusiano wake na jamii hasa sekta binafsi ili kubadili mtazamo uliopo sasa kuwa Wakala huo unatengeneza magari ya Serikali peke yake na hivyo kushindwa kuteka soko la sekta binafsi.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) Eng. Marceline Magesa amemshukuru Katibu Mkuu kwa kuwapatia vifaa mbalimbali na mitambo na kuahidi kuwa vitatumika vizuri ili kuimarisha utendaji kazi wa TEMESA.

“Asilimia 100 ya mapato kwa baadhi ya mikoa tunayaacha mikoani ili kufufua mitambo iliyoko na kuboresha huduma za Ufundi, hivyo tumieni fursa hii kubuni miradi mingi ya kuongeza mapato”, amesema Eng. Magesa.

Ubunifu, kujitangaza na kutoa motisha kwa wafanyakazi inachangia ari ya kufanya kazi ambapo TEMESA mkoa wa Pwani na Tanga imeelezwa kufanya vizuri na hivyo kuhudumia taasisi mbalimbali binafsi na za umma.

Jumatano, 15 Aprili 2015

AJALI ZA BARABARANI ZAZUA GUMZO

Eneo ilipotokea ajali ya basi la Jordan linalofanya safari za Arusha Mwanza iliyotokea leo .
 
Baadhi ya mashuhuda wa ajali ya basi la Jordan  wakifuatilia kwa karibu .

Basi la kampuni ya Air Jordan linalofanya safari zake Mwanza ,Arusha limepata ajali mbaya iliyotokea eneo la Nzega leo amabapo mtu mmoja amefariki na wengine 28 wamejeruhiwa na chanzo cha ajali hiyo inasemekana ni mwendo kasi wa dereva.

MAGAIDI 10 YAKAMATWA MOROGORO


 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia watu kumi kwa tuhuma za kukutwa na silaha za moto zaidi ya 30 pamoja na milipuko.

Watu hao walikamatwa leo eneo la msikiti wa Suni  Kidatu ambapo ndipo walipojifungia huku wameshika bendera yenye maneno ya kiarabu yenye tafsiri ya Mungu ni mmoja pamoja na mavazi ya kijeshi.

Hata hivyo  mmoja  ya  watuhumiwa hao (Ahmad Makwendo) alimjeruhi askari kwa kumkata na jambia eneo la shingoni wakati wa purukushani za kuwakamata watu hao ambapo inasadikika walikuwa wakifanya maandalizi ya ugaidi.

                                                                                                                                                                           
jeshi la polisi Mkoani Morogoro akionyesha vifaa vilivyokamatwa kutoka kwa watuhumiwa hao ni mavazi ya jeshi,milipuko na vifaa vya moto.(PICHANI JUU).
 
 

Jumanne, 14 Aprili 2015

LOWASA AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA SHULE WILAYANI KAHAMA

 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea zawadi ya kitabu cha Mungu (Biblia) kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Dayosisi ya Shinyanga,Dkt. John Kanon Nkola mara baada ya kuendesha Harambee ya Kuchangisha fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Pastoreti ya Kahama Mjini.ambapo zaidi ya Shilingi Milion 212 zilipatikana zikiwemo na ahadi.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono waumini wa Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Pastoreti ya Kahama Mjini,wakati alipokuwa akiwasili kwenye kanisa hilo kwa ajili ya kuendesha Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa hilo.
 
 
 .Pichani chini na juu, Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe na kufungua pazia katika jiwe la msingi ikiwa ni ishara ya Ufunguzi rasmi wa Jengo la Madarasa ya Shule ya awali ya Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Pastoreti ya Kahama Mjini.ambapo baadae aliendesha Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa hilo.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipanda Mti katika eneo la Kanisa hilo.
 .
 

LIPUMBA ASEMA SERIKALI IMESHINDWA

Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF mh Prof. IBRAHIM LIPUMBA akizungumza na viongozi wa Chama hicho pamoja na wanahabari wakati akifungua kikao baraza kuu la Uongozi la Taifa la Chama hicho leo makao makuu jijini Dar es Salaam.kulia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho MAALIM SEIF SHARIF HAMAD,na kushoto ni makamu wa rais wa chama hicho zanzibar JUMA DUNI HAJI

Chama cha Wananchi CUF kimesema kuwa ni ukweli usipingika kuwa kwa sasa Serikali ipo taabani kutokana na mambo mengi yanayotokea huku serikali ikiwa haitoi majibu yanayowaridhisha wananchi jambo ambalo limewafanya Watanzania kukata tamaa na Nchi yao.
Akifungua kikao cha kawaida cha baraza la uongozi taifa la chama hicho mwenyekiti wa CUF Mh. Ibrahim  Haroun Lipumba amesema kuwa swala la   uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na mchakato mzima wa upigaji kura imeonyesha wazi kuwa Serikali ya Tanzania imeshindwa kufanikisha zoezi hilo huku ikiitupia mzigo wote tume ya Taifa ya uchaguzi ambayo na yenyewe imeshindwa.Amesema kuwa kushindwa kumalizika kwa uandikishwaji wa daftari hilo kwa muda uliopangwa ni jambo ambalo lilikuwa haliepukiki kwani vyama vya upinzani pamoja na wadau mbalimbali walishaitahadharisha serikali juu ya mchakato huo lakini serikali ilishindwa kusikiliza kilio chao na matokeo yake mchakato huo umeshindwa kufanikiwa.
Amesema kuwa moja ya ajenda za kikao hicho cha baraza kuu la uongozi la Chama hicho ni pamoja na kujadili maswala hayo yanayohusiana na kushindwa kufanikiwa kwa daftari hilo la wapiga kura na kujadili nini cha kufanya ili uchagauzi uweze kufanyika na pia ufanyike kwa amani na upendo.
Aidha Prof. Lipumba amesema kuwa serikali ya Tanzania imeshindwa kuwa sikivu kwa Wananchi wake ambao ndio waliowaweka madarakani, huku akitolea mfano sakata la migomo ya wafanyabiashara,madereva na mambo mengine yanayoendelea ambapo amesema badala ya serikali kukaa chini na watu hao ili kuwasikiliza imekuwa kinyume kwani wamekuwa wakitumia ubabe na kuwaacha walalamikaji hao kukosa la kufanya.
Picha  juu ni baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho kilichoanza leo jijini Dar es salaam

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amesema kuwa kikao hicho cha kawaida cha baraza kuu la uongozi taifa ambacho  kitajadiliana kwa siku mbili mfululizo  pamoja na mambo mengine watajadili muungano wa chama chao pamoja na vyama vingine vya upinzani umoja uliopewa jina la UKAWA pamoja na kujadili ni jinsi gani ya kuimarisha umoja huo kuelekea uchaguzi ujao mwishoni mwa mwaka huu.

Jumatatu, 13 Aprili 2015

RAIS KIKWETE AHUDHURIA UZINDUZI WA KOZI YA MAADILI

 Mmoja wa Wasanii kutoka Bendi ya Mrisho Mpoto akifanya onyesho katika Uzinduzi wa Kozi Maalumu ya Maadili na Uongozi.

 Mhe.Dkt.Jakaya Mrisgo Kikwete akiimba wimbo wa Taifa katika Uzinduzi wa wa Kozi Maalumu ya Maadili na Uongozi uliofanyika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  leo jijini Dar es Salaam.

 Rais Kikwete (katikati)akionesha kitabu kitachotumika kufundisha Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi kilichozinduliwa leo Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(kulia)Prof.Shardrack Mwakalila, Mkuu wa Chuo(kushoto)Dkt.Shukuru Kawambwa,Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

 

 

Mhe.Pius Msekwa akitoa neno la shukurani baada ya kusimikwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa Kibweta Cha Mwalimu Nyerere na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo jijini Dar es Salaam.



 Brass Bendi ya Polisi ikiongoza kuimba wimbo Taifa katika Uzinduzi wa Kozi Maalum ya Maadili na Uongozi uliofanyika katika Uwanja wa Chuo hicho(MNMA).


 Pichani( kushoto)Rais Kikwete (katikati)Prof.Mwakalila na( kulia)Mhe.Pius Msekwa wakiimba Wimbo wa Taifa.

 

Wakiwa katika picha ya pamoja na Ubalozi.

 

 

 Wakiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.



Wakiwa katika picha ya pamoja na Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Jumapili, 12 Aprili 2015

AJALI MBAYA YA GARI YATOKEA KAHAMA


Basi la Wibonela likiokolewa baada ya ajali hiyo leo asubuhi eneo la Fantom Kahama.
 

Basi la Wibonela linalofanya safari zake kahama Dar limeua watu zaidi ya watano na kujeruhi wengi leo asubuhi eneo la Fantom Kahama. Chanzo ni mwendo kasi uliomshinda dereva wa basi hilo kukata kona ya kuingia barabara kuu hivyo kuruka nje na kusababisha basi hilo kupinduka. . Mpaka sasa haijajulikana majeruhi ni wangapi na waliokufa ni wangapi.