Shahidi huyo ambaye ni mpelelezi wa polisi kutoka Dar es Salaam, alisema uchunguzi waliofanya umebaini kuwa kiungo kimoja cha mtu mwenye ulemavu wa ngozi huuzwa hadi shilingi milioni 600.
Pia ilidai kuwa, viungo hivyo vya albino hupimwa ubora wake kwa kutumia wembe, shilingi moja ya zamani pamoja na redio.
Washtakiwa hiyo, Nasor Charles, Masaru Kahindi, Ndahanya Lumola na Singu Siantem wanadaiwa kumuua albino Zawadi Magimbu, mkazi wa Kijiji cha Nyamaruru wilayani Geita.
Ushahidi uliokuwa ukitolewa na mpelelezi huyo ulitokana na kuwahoji watuhumiwa hao.
Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wa Ngozi Mwanza (RAS),Alfred Kapole. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni