Jumanne, 24 Februari 2015

Nemc kuvibana viwanda vinavyochafua mazingira

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc), limesema halitasita kuvifungia viwanda vitakavyokwenda kinyume na sheria na utaratibu wa kutunza mazingira.
Kauli hiyo imekuja takriban sita tano tangu Nemc itangaze kukifungia kiwanda cha nguo cha 21 Century cha Morogoro kutokana na kushindwa kutakatisha maji ya kiwandani kabla ya kuruhusiwa kuingia mto Ruvu.
Ofisa Mwandamizi wa Mazingira wa Nemc, Glory Kombe alisema hayo juzi wakatia akuzungumzia hatua za kuchukuliwa dhidi ya uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na shughuli za viwanda.
Kufungiwa kwa kiwanda hicho cha Morogoro kumekuja baada ya awali kufungiwa kiwanda cha kutengeneza sementi (Twiga cement) cha Dar es Salaam.
Kiwanda hicho ambacho sasa kimeruhusiwa kuendelea na kazi, kilifungwa kutokana na kushindwa kudhibiri vumbi lililokuwa likitokana na uzalishajiwa bidhaa hiyo, hivyo kuleta athari kwa wananchi.
Kombe alisema Nemc hatakuwa tayari kuona viwanda vikichafua mazingira kama vile hakuna sheria zinazowaelekeza namna bora ya kulinda mazingara ili kuepusha hatari.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni