Ijumaa, 20 Februari 2015
Robert Mugabe atimiza miaka 91
Kiongozi wa nchi mzee kuliko wote duniani, Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Jumamosi wiki hii anatimiza miaka 91 ya kuzaliwa, huku sherehe kubwa ikimsubiri.
Sherehe hiyo kubwa imezua gumzo hasa kutokana na kiasi kikubwa cha pesa kitakachotumika wakati wananchi wengi wa nchi hiyo wanaishi katika hali ya umaskini kupindukia.
Mugabe aliingia madarakani mwaka 1980 na tangu wakati huo ameendelea kubaki kwenye madaraka hadi sasa. Pia ana mpango wa kuwania kiti cha urais katika uchaguzi ujao wa nchi hiyo.
Utawala wa Mugabe umekuwa ukilalamikiwa na jumuiya za kimataifa kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu, kutumia vyombo vya dola kuwabana wapinzani.
Lakini sera yake ya kuwapokonya ardhi baadhi ya walowezi wa Uingereza, iliongeza mjadala wa namna anavyoendesha serikali yake.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni