Jumanne, 24 Februari 2015

Kombe la Dunia 2022 kuchezwa Novemba Qatar

Fainali za Kombe la Dunia mwaka za mwaka 2022 nchini Qatar zinaweza kuchezwa Novemba au Desemba. Kila mwaka fainali za Kombe la Dunia huchezwa katikati ya mwaka (Juni na Julai), lakini za mwaka huo zinaweza kuchezwa mwishoni mwa mwaka ili kuepuka joto kali nchini Qatar linalofika nyuzi joto 40 kati ya Juni na Julai.
Kamati maalumu ya Shirikisho la Soka Ulimwenguni (Fifa), imesema kuwa kama fainali hizo zitachezwa katikakati ya mwaka kama ratiba inavyotaka, zinaweza kuwaathiri wachezaji na mashabiki ambao hawajazoea hali hiyo ya joto.
Hivyo basi, njia ya kunusuru hali hiyo ni kuipeleka mashindano hayo hadi Desemba ambako kunakuwa na nyuzi joto 25.
Mapendezo hayo yanatarajia kujadiliwa na Kamati ya Utendaji ya Fifa itakayokuna mjini Zurich, Uswisi kati ya Machi 19 na 20 March.
Kamati hiyo ya kufuatilia maandalizi inaongozwa na Sheikh Salman bin Ebrahim Al-Khalifa, ambaye pia amependekeza michuano hiyo kuchezwa kwa muda mfupi zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika miaka ya hivi karibuni zilipoanza kushiriki timu zaidi ya 30.
Bosi huyo wa kamati amependekeza michuano hiyo kuanza  Novemba 26 hadi Desemba 23, mwaka  2022
Hata hivyo, Fifa imesema haina mpango wa kupunguza timu kutoka 32 za sasa zinazocheza mechi 64


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni