Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Gavana wa Benki Kuu nchini,Profesa Beno Ndulu amesema kazi milioni 885 za nchi ya jamhuri ya watu wa China wameshindwa kuziendesha,hivyo Tanzania inaweza kufaidika na kazi hizo katika kuongeza pato la taifa kwa sekta ya viwanda.
Profesa Ndulu ameyasema hayo leo katika warsha ya kujadili chamgamoto na jinsi ya kukabiliana nazo kwa ukuaji wa Uchumi kutokana na rasilimali zilizopo nchini.
Amesema pato la taifa katika sekta ya viwanda limezidi kukua kwa dola za Marekani milioni 1.3 hiyo ni tofauti na miaka 10 iliyopita,hivyo kutokana na hali hiyo sekta ya viwanda itazidi kuongeza pato la taifa kuliko ilivyo sasa.
Amesema sekta nyingine inayoongeza pato la taifa ni sekta ya usafirishaji ambayo imechangia pato la taifa dola za Kimarekani milioni 8.6.
Kwa upande wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (PAC),Zitto Kabwe amesema uchumi umeshuka na uchumi uliopo unashikiliwa na watu wachache ambao ni wafanyabiashara
Amesema serikali iweke kipaumbele katika kilimo kutokana na kuwa na hali mbaya ya kiuchumi na wananchi wasifurahie kuwepo hali ya uchumi iliyopo sasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni