Pacha
walioungana kifua na tumbo wamefanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha na
hali zao zinaendelea vizuri. Huo ni upasuaji wa kwanza kufanikiwa katika
historia ya pacha walioungana kifua na tumbo kufanyiwa upasuaji wa
kuwatenganisha na bado wakabaki salama.
Knatalye Hope na Adeline
Faith Mata walizaliwa kwenye Jimbo la Texas nchini Marekani, Aprili
mwaka jana kwa wazazi Elysse na John Eric.
Wazazi hao walielezwa
mapema kabla hata ya kuzaliwa watoto hao kuwa picha zinaonyesha
wameungana sehemu ya kifua, lakini baada ya kuzaliwa muungano wa maumbo
yao ulikuwa zaidi ya kifua, kwani walikuwa wakishirikiana tumbo, ini,
utumbo na sehemu ya nyonga. Upasuaji huo wa kwanza na pekee kwa aina
yake, ulichukua saa 26 hadi kukamilika.
Upasuaji huyo uliofanyika mwanzoni mwa mwezi, uliwashirikisha madaktari bingwa wa upasuaji 12.
Pacha wanavyoonekana kabla ya kunyiwa upasuaji uliochukua zaidi ya saa 26
Wakiandaliwa kabla ya kufanyiwa upasuaji
Timu ya wataalamu waliobeba jukumu la kufanya upasuaji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni