Jumatatu, 23 Februari 2015

WALIODAI AJIRA JKT KWA KUANDAMANA HADI IKULU WAKAMATWA

Na Tinah Reuben

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa kutekwa kwa kiongozi wa kupanga maandamano kwa waliochwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),George Mgoba ni mchezo wa kuigiza ‘filamu’ na litaendelea kufanya uchunguzi wa kina wa tukio hilo.
Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake.Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova (pichani),amesema kuwa tukio la kutekwa kwa George limekaa kama mchezo wa kuigiza hivyo jeshi la polisi linafanya uchunguzi walihusika na tukio hilo.

Amesema wa umoja wa vijana hao walioandamana na kuongozwa na ,George haujasajiliwa sehemu yeyote kwa mamlaka zinahusika na usajili wa asasi nchini.

Kamanda Kova amesema vijana hao walidai kuwa wataajiriwa na jeshi hilo jambo ambalo halina ukweli wowote kutoka katika mamlaka ya jeshi hilo.

Aidha amesema vijana hao suala la ajira sio la serikali kutokana na ujuzi walioupata wanaweza kujiajiri sehemu yeyote  kutokana ma mafunzo waliyapata katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Kamanda Kova amesema kuna vijana wanne wamekamatwa ambao walikuwa katika mpango wa kuratibu maandamano ya kwenda Ikulu ili Rais Jakaya Kikwete awasikilize.

Amesema Makamu Mwenyekiti wa umoja huo ,Barali Kiwango amesalimisha mikoni mwa jeshi la Polisi ambapo wanaendelea kufanya  naye mahojiano na kuwataka vijana hao wasikutane kwa ajili ya maandamano na wataobainika kufanya hivyo nguvu ya dola itachukua mkondo wake..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni