Ilikuwa
kama filamu au mchezo wa kuigiza, lakini kilichotokea kilikuwa kweli
mbele ya macho ya watu. Ndoa 10 zilifungwa mwishoni mwa wiki iliyopita
na kilichoshangaza zaidi ni wanandoa hao kufunga ndoa wakiwa kwenye
majeneza katika mji wa Wat Takien, Jimbo la Nonthaburi nchini Bangkok.
Wandoa
hao walifikia uamuzi huo kutokana na imani kuwa kwa kulala kwenye
jeneza muda mfupi baada ya kufunga ndo, kungeondoa mikosi kwenye maisha
na kuwafanya kuishi maisha ya furaha.
Wanandoa
hao walipanga majeneza yao yakiwa na rangi ya pinki na wakiwa ndani
yake walilala pamoja kama vile maiti inavyohifadhiwa tayari kwa kuzikwa.
Majeneza hayo yalitengenezwa maalumu kwa ajili ya kuweza kulala watu wawili bila shida.
Kadhalika,
wakiwa ndani ya majeneza, kila mmoja alishika ua na kulikumbatia
kifuani, kabla viongozi wa kimila kufunika jeneza hilo kwa kutumia
kitambaa cheupe ikiwa ni ishara ya kuondoa mikosi.
Kwa
mujibu wa gazeti la Bangkok Post, wanandoa hao baada ya kutoka kwenye
majeneza hayo, huanza maisha mapya wakiwa hawana mikosi kwa vile tayari
inakuwa imeondolewa kwenye baada ya kumalziika ibada.
Hata
hivyo, tukio hilo siyo mara ya kwanza kutokea nchini humo, kwani mwaka
jana wakati wa shehere za siku ya wapendanao zilifanyika na kisha
kufuatia na sherehe za kimila kama ilivyokuwa mwaka huu.
Lilipofanyika
tukio kama hilo mwaka jana, hakukuwa na mapngo wa kulifanya tena katika
mji wa Makha Bucha, lakini kutokana na maombi mengi kutoka kwa watu,
ililazimu ukufanyika tena.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni