Alhamisi, 26 Februari 2015

Kiungo kimoja cha albino shilingi milioni 600

Shahidi katika kesi ya mauaji ya albino mkoani Geita, jana alitoa ushahidi wake mbele ya mahakama ya mkoa na kudai kuwa, viungo vya albino vinauzwa bei mbaya.
Shahidi huyo ambaye ni mpelelezi wa polisi kutoka Dar es Salaam, alisema uchunguzi waliofanya umebaini kuwa kiungo kimoja cha mtu mwenye ulemavu wa ngozi huuzwa hadi shilingi milioni 600.
Pia ilidai kuwa, viungo hivyo vya albino hupimwa ubora wake kwa kutumia wembe, shilingi moja ya zamani pamoja na redio.
Washtakiwa hiyo,  Nasor Charles, Masaru Kahindi, Ndahanya Lumola na Singu Siantem wanadaiwa kumuua albino Zawadi Magimbu, mkazi wa Kijiji cha Nyamaruru wilayani Geita.
Ushahidi uliokuwa ukitolewa na mpelelezi huyo ulitokana na kuwahoji watuhumiwa hao.
Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wa Ngozi Mwanza (RAS),Alfred Kapole.

Jumanne, 24 Februari 2015

HEINEKEN UNVEILS CLUB 777 SPORTS LOUNGE TO IGNITE UEFA CHAMPIONS LEAGUE EXPERIENCE

Heineken Tanzania Country Manager Michael Mbungu (third from left in grey suit) looks on as Mrs Jackie Mlatie pops a bottle of champagne to signify the official launch of Club 777, in Kawe Dar es salaam. He is flanked by Mr. Femin Mabachi (extreme right), the group CEO of Club 777. Looking on from left are Heineken Brand ambassodors Irene Jackson and Nuru.
Heineken Tanzania Country Manager Michael Mbungu (first from left in grey suit) is all smiles as Mr. Mlatie Assey gives a toast to signify the launch of a new hotspot in town Club 777 which located in Kawe, Dar es Salaam.
Come in for the grand tour: Mr. Mlatie Assey (centre left) who is the Managing director seems to say during the official launch of Club 777 in Kawe, Dar es Salaam. Centre right is Heineken Tanzania’s Country Manager Michael Mbungu ushering guests (not in picture) present during the launch.

The new Heineken® Club 777 Sports Lounge at Kawe in Dar es Salaam, which officially opened its doors to the public over the weekend, aims to keep consumers and sports fans up to date with live action from all the major sporting events around the world. The Heineken Club 777 Lounge is the first of its kind in Tanzania.

Situated at a residential area near the beach, it also offers a relief for the consumer who wants to relax and enjoy away from the hustle of the city. The Club 777 Lounge puts a strong emphasis on sports coverage and customers can keep connected and up to date with the latest scores and all the action with live screenings throughout the venue, which is complemented by more general entertainment through the many display screens.

Speaking during the launch of the Club HEINEKEN Tanzania Country Manager Mr. Michael Mbungu commented: “Bringing this premium brand experience to Dar es Salaam with a world-class brand and in an innovative business-class-lounge style concept is a powerful example of our commitment to delighting consumers and adding new dimensions to the Heineken fresh and unexpected approach of partnerships.

We partnered with the bar as it fits within our brand profile and ambition. ‘We aim to create exciting worldly experiences to consumers by interacting with them in a way Heineken® can do.

“The Heineken Lounge is a new and refreshing experience for Dar es salaam consumers and patrons, with all the convenience and benefits of a traditional bar and with the opportunity to escape from the hustle with complimentary Wi-Fi and power points to recharge phones and laptops, and complimentary daily newspapers.’’ Added Mr. Mlatie Assey, CEO of the Club.

The Lounge offers cold Heineken as well as a broad selection of other alcoholic and non-alcoholic beverages, alongside gourmet snacks and light meals.

WALIOANDAMANA KUDAI AJIRA JKT WAFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

Na Tinah Reuben

VIJANA sita waliokuwa katika mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wanaodaiwa kupanga kuandamana mpaka kwa Rais Jakaya Kikwete kudai ajira,wamefikishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam.

Wakisomewa mashtaka yao na mwendesha mashtaka wa serikali,Tumaini Kwema mbele ya Hakimu Mkazi ,Frank Mushi alidai  kuwa,washtakiwa hao wanadaiwa kufanya fujo,kufanya mkusanyiko usiokuwa wa halali ili kuilazimisha serikali kuwapatia kazi na kushawishi kutenda makosa ya jinai kwa kuandamana mnamo Februari 15 mwaka huu eneo la Msimbazi Centre jijini Dar es salaam.

Washitakiwa hao ni George Gagris,Linus Immanuel,Pharas Owera,Emmanuel Richard,Ridhwan Brayson na Jacob Joseph.

 Baada ya kusomewa mashtaka na mwendesha mashtaka,Tumaini Kwema,watuhumiwa hao wote kwa pamoja walikana mashtaka hayo.

Washtakiwa hao wamerudishwa tena rumande kutokana na kutokidhi masharti na vigezo vya dhamana,kesi hiyo itatajwa tena Machi 6 mwaka huu.
 Baadhi ya vijana waliokuwa katika mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wanaodaiwa kupanga kuandamana mpaka kwa Rais Jakaya Kikwete kudai ajira,wakiwa chini ya ulinzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,jijini Dar es salaam leo.
 Watuhumiwa hao wakipandishwa kwenye gari ya polisi.

Kombe la Dunia 2022 kuchezwa Novemba Qatar

Fainali za Kombe la Dunia mwaka za mwaka 2022 nchini Qatar zinaweza kuchezwa Novemba au Desemba. Kila mwaka fainali za Kombe la Dunia huchezwa katikati ya mwaka (Juni na Julai), lakini za mwaka huo zinaweza kuchezwa mwishoni mwa mwaka ili kuepuka joto kali nchini Qatar linalofika nyuzi joto 40 kati ya Juni na Julai.
Kamati maalumu ya Shirikisho la Soka Ulimwenguni (Fifa), imesema kuwa kama fainali hizo zitachezwa katikakati ya mwaka kama ratiba inavyotaka, zinaweza kuwaathiri wachezaji na mashabiki ambao hawajazoea hali hiyo ya joto.
Hivyo basi, njia ya kunusuru hali hiyo ni kuipeleka mashindano hayo hadi Desemba ambako kunakuwa na nyuzi joto 25.
Mapendezo hayo yanatarajia kujadiliwa na Kamati ya Utendaji ya Fifa itakayokuna mjini Zurich, Uswisi kati ya Machi 19 na 20 March.
Kamati hiyo ya kufuatilia maandalizi inaongozwa na Sheikh Salman bin Ebrahim Al-Khalifa, ambaye pia amependekeza michuano hiyo kuchezwa kwa muda mfupi zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika miaka ya hivi karibuni zilipoanza kushiriki timu zaidi ya 30.
Bosi huyo wa kamati amependekeza michuano hiyo kuanza  Novemba 26 hadi Desemba 23, mwaka  2022
Hata hivyo, Fifa imesema haina mpango wa kupunguza timu kutoka 32 za sasa zinazocheza mechi 64


Madaktari watumia saa 26 kuwatenganisha pacha

Pacha walioungana kifua na tumbo wamefanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha na hali zao zinaendelea vizuri. Huo ni upasuaji wa kwanza kufanikiwa katika historia ya pacha walioungana kifua na tumbo kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha na bado wakabaki salama.
Knatalye Hope na Adeline Faith Mata walizaliwa kwenye Jimbo la Texas nchini Marekani, Aprili mwaka jana kwa wazazi Elysse na John Eric.
Wazazi hao walielezwa mapema kabla hata ya kuzaliwa watoto hao kuwa picha zinaonyesha wameungana sehemu ya kifua, lakini baada ya kuzaliwa muungano wa maumbo yao ulikuwa zaidi ya kifua, kwani walikuwa wakishirikiana tumbo, ini, utumbo na sehemu ya nyonga. Upasuaji huo wa kwanza na pekee kwa aina yake, ulichukua saa 26 hadi kukamilika.
Upasuaji huyo uliofanyika mwanzoni mwa mwezi, uliwashirikisha madaktari bingwa wa upasuaji 12.


                  Pacha wanavyoonekana kabla ya kunyiwa upasuaji uliochukua zaidi ya saa 26



              Wakiandaliwa kabla ya kufanyiwa upasuaji

          Timu ya wataalamu waliobeba jukumu la kufanya upasuaji

Nemc kuvibana viwanda vinavyochafua mazingira

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc), limesema halitasita kuvifungia viwanda vitakavyokwenda kinyume na sheria na utaratibu wa kutunza mazingira.
Kauli hiyo imekuja takriban sita tano tangu Nemc itangaze kukifungia kiwanda cha nguo cha 21 Century cha Morogoro kutokana na kushindwa kutakatisha maji ya kiwandani kabla ya kuruhusiwa kuingia mto Ruvu.
Ofisa Mwandamizi wa Mazingira wa Nemc, Glory Kombe alisema hayo juzi wakatia akuzungumzia hatua za kuchukuliwa dhidi ya uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na shughuli za viwanda.
Kufungiwa kwa kiwanda hicho cha Morogoro kumekuja baada ya awali kufungiwa kiwanda cha kutengeneza sementi (Twiga cement) cha Dar es Salaam.
Kiwanda hicho ambacho sasa kimeruhusiwa kuendelea na kazi, kilifungwa kutokana na kushindwa kudhibiri vumbi lililokuwa likitokana na uzalishajiwa bidhaa hiyo, hivyo kuleta athari kwa wananchi.
Kombe alisema Nemc hatakuwa tayari kuona viwanda vikichafua mazingira kama vile hakuna sheria zinazowaelekeza namna bora ya kulinda mazingara ili kuepusha hatari.

Jumatatu, 23 Februari 2015

FURSA MILIONI 885 ZA CHINA,TANZANIA KUNUFAIKA NAZO

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Gavana wa Benki Kuu nchini,Profesa Beno Ndulu amesema kazi milioni 885 za nchi ya jamhuri ya watu wa China wameshindwa kuziendesha,hivyo Tanzania inaweza kufaidika na kazi hizo katika kuongeza pato la taifa kwa sekta ya viwanda.

Profesa Ndulu ameyasema hayo leo katika warsha ya kujadili chamgamoto na jinsi ya kukabiliana nazo kwa ukuaji wa Uchumi kutokana na rasilimali zilizopo nchini.

Amesema pato  la taifa katika sekta ya viwanda limezidi kukua kwa dola  za Marekani milioni 1.3 hiyo ni tofauti  na miaka 10 iliyopita,hivyo kutokana na hali hiyo sekta ya viwanda itazidi kuongeza  pato la taifa kuliko ilivyo sasa.

Amesema sekta nyingine inayoongeza pato la taifa ni sekta ya usafirishaji ambayo imechangia pato la taifa dola za Kimarekani milioni 8.6.

Kwa upande wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (PAC),Zitto Kabwe amesema  uchumi umeshuka na uchumi uliopo unashikiliwa na watu wachache ambao ni wafanyabiashara 

Amesema serikali iweke kipaumbele katika kilimo kutokana na kuwa na hali mbaya ya kiuchumi na wananchi wasifurahie kuwepo hali ya uchumi iliyopo sasa.

WALIODAI AJIRA JKT KWA KUANDAMANA HADI IKULU WAKAMATWA

Na Tinah Reuben

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa kutekwa kwa kiongozi wa kupanga maandamano kwa waliochwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),George Mgoba ni mchezo wa kuigiza ‘filamu’ na litaendelea kufanya uchunguzi wa kina wa tukio hilo.
Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake.Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova (pichani),amesema kuwa tukio la kutekwa kwa George limekaa kama mchezo wa kuigiza hivyo jeshi la polisi linafanya uchunguzi walihusika na tukio hilo.

Amesema wa umoja wa vijana hao walioandamana na kuongozwa na ,George haujasajiliwa sehemu yeyote kwa mamlaka zinahusika na usajili wa asasi nchini.

Kamanda Kova amesema vijana hao walidai kuwa wataajiriwa na jeshi hilo jambo ambalo halina ukweli wowote kutoka katika mamlaka ya jeshi hilo.

Aidha amesema vijana hao suala la ajira sio la serikali kutokana na ujuzi walioupata wanaweza kujiajiri sehemu yeyote  kutokana ma mafunzo waliyapata katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Kamanda Kova amesema kuna vijana wanne wamekamatwa ambao walikuwa katika mpango wa kuratibu maandamano ya kwenda Ikulu ili Rais Jakaya Kikwete awasikilize.

Amesema Makamu Mwenyekiti wa umoja huo ,Barali Kiwango amesalimisha mikoni mwa jeshi la Polisi ambapo wanaendelea kufanya  naye mahojiano na kuwataka vijana hao wasikutane kwa ajili ya maandamano na wataobainika kufanya hivyo nguvu ya dola itachukua mkondo wake..

Ijumaa, 20 Februari 2015

Robert Mugabe atimiza miaka 91



Kiongozi wa nchi mzee kuliko wote duniani, Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, Jumamosi wiki hii anatimiza miaka 91 ya kuzaliwa, huku sherehe kubwa ikimsubiri.
Sherehe hiyo kubwa imezua gumzo hasa kutokana na kiasi kikubwa cha pesa kitakachotumika wakati wananchi wengi wa nchi hiyo wanaishi katika hali ya umaskini kupindukia.
Mugabe aliingia madarakani mwaka 1980 na tangu wakati huo ameendelea kubaki kwenye madaraka hadi sasa. Pia ana mpango wa kuwania kiti cha urais katika uchaguzi ujao wa nchi hiyo.
Utawala wa Mugabe umekuwa ukilalamikiwa na jumuiya za kimataifa kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu, kutumia vyombo vya dola kuwabana wapinzani.
Lakini sera yake ya kuwapokonya ardhi baadhi ya walowezi wa Uingereza, iliongeza mjadala wa namna anavyoendesha serikali yake.

Wafunga ndoa wakiwa wamelala kwenye majeneza

Ilikuwa kama filamu au mchezo wa kuigiza, lakini kilichotokea kilikuwa kweli mbele ya macho ya watu. Ndoa 10 zilifungwa mwishoni mwa wiki iliyopita na kilichoshangaza zaidi ni wanandoa hao kufunga ndoa wakiwa kwenye majeneza katika mji wa Wat Takien, Jimbo la Nonthaburi nchini  Bangkok.
Wandoa hao walifikia uamuzi huo kutokana na imani kuwa kwa kulala kwenye jeneza muda mfupi baada ya kufunga ndo, kungeondoa mikosi kwenye maisha na kuwafanya kuishi maisha ya furaha.
Wanandoa hao walipanga majeneza yao yakiwa na rangi ya pinki na wakiwa ndani yake walilala pamoja kama vile maiti inavyohifadhiwa tayari kwa kuzikwa.
Majeneza hayo yalitengenezwa maalumu kwa ajili ya kuweza kulala watu wawili bila shida.
Kadhalika, wakiwa ndani ya majeneza, kila mmoja alishika ua na kulikumbatia kifuani, kabla viongozi wa kimila kufunika jeneza hilo kwa kutumia kitambaa cheupe ikiwa ni ishara ya kuondoa mikosi.
Kwa mujibu wa gazeti la Bangkok Post, wanandoa hao baada ya kutoka kwenye majeneza hayo, huanza maisha mapya wakiwa hawana mikosi kwa vile tayari inakuwa imeondolewa kwenye baada ya kumalziika ibada.
Hata hivyo, tukio hilo siyo mara ya kwanza kutokea nchini humo, kwani mwaka jana wakati wa shehere za siku ya wapendanao zilifanyika na kisha kufuatia na sherehe za kimila kama ilivyokuwa mwaka huu.
Lilipofanyika tukio kama hilo mwaka jana, hakukuwa na mapngo wa kulifanya tena katika mji wa Makha Bucha, lakini kutokana na maombi mengi kutoka kwa watu, ililazimu ukufanyika tena.





Alhamisi, 5 Februari 2015

Vikosi vya Chad vyawaua wapiganaji 200.

Jeshi la Chad linasema kuwa limewaua wapiganaji 200 wa kundi la boko Haram huku nao wakipoteza wanajeshi 9 katika vita vikali vya kuuteka mji muhimu kazkazni mashariki mwa Nigeria.
Wapiganaji wa Boko Haram waliwauwa watu 30 baada ya kutoroka mapigano hayo na kuelekea nchini Cameroon,mkaazi mmoja amesema.

Vilikuwa vita vikali vilivyowahusisha wapiganaji wa Chad tangu waingie Nigeria ili kukabiliana na wanamgambo hao.
Wanajeshi wa Chad.
Vikosi vya Chad na vile vya Cameroon pia vinaendelea kuangusha mabomu katika msitu mkubwa wa sambiza ambapo wapiganaji hao wana kambi.

Boko Haram wanadaiwa kutorokea katika katika msitu huo baada ya kuwateka zaidi ya wasichana 200 wa shule mnamo mwezi Aprili kutoka mji wa kazkazini mashariki mwa Nigeria wa Chibok.
Haijulikani iwapo bado washichana hao wapo katika msitu huo.




 Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kwa niaba ya vyama 10 visivyo na uwakilishi wa wabunge Bungeni wakati wakitoa tamko kuhusu viongozi wa dini kutojihusisha na masuala ya siasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu 2015 . Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Sauti ya Umma (Sau), Ali Kaniki na Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima Tanzania (AFP), Rashid Rai.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima Tanzania (AFP), Rashid Rai (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Naibu  Katibu Mkuu wa Chama cha UMD, Moshi Kigundula na Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Sauti ya Umma (Sau), Ali Kaniki (kulia), akizungumza katika mkutano huo kuhusu suala zima la Nishati ya umeme nchini na sakata la Escrow. Kushoto Kiongozi wa chama cha Jahazi Asilia Mbwana Kibande na Amina Mcheka kutoka chama cha Chausta.
 Naibu Katibu Mkuu wa wa Chama cha UPDP, Felix Makuwa (kulia), akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 Mwakilishi kutoka chama cha Chausta, Amina Mcheka akitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa katika mkutano huo.
 Mwakilishi kutoka chama cha Jahazi Asilia, Mbwana Kibande (kushoto) naye akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 viongozi wa vyama hivyo wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hizo.
…………………………………………………………………………….
Dotto Mwaibale
VYAMA kumi visivyokuwa na uwakilishi bungeni vimewaonya  viongozi wa dini nchini katika kipindi cha mwaka huu ambako kutafanyika uchaguzi mkuu kutojihusisha na masuala ya siasa kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na katiba ya nchi.
Aidha, vyama hivyo vimeitaka serikali kupitia upya mikataba ya makampuni yanayozalisha umeme nchini kwa kuwa baadhi yanauza nishati hiyo kwa gharama kubwa licha ya kwamba baadhi yanazalisha umeme kwa kutumia gesi na kusababisha wananchi kuingia gharama kubwa.
Tamko hilo limetolewa na makatibu wakuu wa vyama vya AFP, CCK, SAU, UMD, Chausta, UPDP, NRA, Jahazi, Chauma na DP ikiwa ni salamu za kukaribisha mwaka mpya wa 2015.
Katibu Mkuu wa AFP, Rashid Rai, akisoma tamko hilo jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wenzake, alisema katika miaka ya hivi karibuni kumejitokeza tabia ya viongozi wa dini kujihusisha na masuala ya siasa hususani kipindi cha uchaguzi mkuu na hivyo kuwachanganya wananchi.
Rai alisema viongozi hao wamekuwa wakitoa matamko kwenye vyombo vya habari kupendekeza au kutoa sifa ya kiongozi anayefaa kuongoza nchi au asiyefaa kupewa nafasi ya uongozi wa umma katika Taifa.
Alisema viongozi wa dini lazima watambue kuwa sheria inazuia viongozi wa dini kujihusisha na masuala ya siasa kwani hali hiyo inawachanganya wananchi kushindwa kujua kama viongozi hao wamebadilisha majukumu yao.
“Unakuta kiongozi wa dini anasema Rais ajaye awe ni mwadilifu na mcha Mungu, au anasema  kiongozi huyu ni chaguo la Mungu, maana yake ni nini,kila dini au dhehebu lina vigezo vyake vya uadilifu na ucha  Mungu,”alisema.
Rai alisema kama viongozi wa dini wanaona watu waliopo kwenye siasa wanafaidi sana ni bora wakaachana na masuala ya kuhubiri dini badala yake waanzishe vyama vya siasa au wajiunge na vyama vya siasa ili waendelee kupata neema wanayohisi inapatikana huko.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha SAU, Ali Kaniki, alisema sakata la akaunti ya Tegeta Escrow limetoa fundisho kwa serikali kuona umuhimu wa kupitia upya mikata ya makapuni yote ya makampuni yanayozalisha umeme.
Alisema baadhi ya makampuni yanayozalisha umeme na kuliuzia Shirika la Umeme nchini (Tanesco) yanatoza tozo kubwa hali ambayo imekuwa ikisababisha gharama za umeme kuwa kubwa hapa nchini.
“Tunayo makampuni yanayozalisha umeme hapa nchini ambayo ni Songas, IPTL Aggreko na Symbion, ukiangalia yote IPTL ndiyo inayouza umeme kwa bei ndogo ukilinganisha na mengi, tunataka serikali ipitie mikataba ya makampuni haya,”alisema.
Naye Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi, alisema katika hali ya kushangaza baadhi ya makampuni licha ya kwamba yanatumia nishati ya gesi kuzalisha umeme lakini yamekuwa yakiuza umeme kwa bei ya juu. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)