Rais Magufuli ameongoza viongozi mbalimbali wa nchi na mamia waliojitokeza kuaga mwili wa marehemu Dk.Didas Masaburi wakati wa kuagwa mapema leo Jijini Dar eS alaam katika viwanja vya Karimjee.
Hali katika kuaga mwili:
Awali ndugu wa familia walimuomba Rais Magufuli angalau atoe neon kidogo licha ya kuwa hawakumpangia, kwa heshima walimtaka angalaui kidogo ili ndugu na jamaa wajue uwepo wake na heshima.
Bila kutegemewa na wengi, katika kuuga mwili wa aliyekuwa meya wa jiji hilo, Dk Didas Masaburi aliyefariki Jumatano iliyopita na kusema Masaburi ana wake wanne au watano na watoto zaidi ya 20.
Kauli ya Dk Magufuli ameitoa muda mfupi baada ya msomaji wa wasifu wa Dk Masaburi kusema kuwa ameacha mke mmoja waliyefunga naye ndoa Jannet Masaburi na wajane wawili kauli ambayo ilizua miguno kutoka kwa waombolezaji.
Hata hivyo, Rais Magufuli aliwaomba familia kuwa na umoja na amani kwani licha ya marehemy kuacha Mwanamke huyo aliyetangazwa hapo, amebainisha kuwa, anamfahamu Dk Masaburi kuwa alikuwa na wake wanne au watano hivi na watoto ni zaidi ya 20.
“Kwa tabia zetu za Afrika, kuwa na wanawake zaidi ya wawili watatu watano ama 10 ni kitu cha kawaida. Hata Mfalme Seleman alikuwa na wanawake zaidi ya 1000, lakini ametajwa katika vitabu vyote vitakativu, nachukua nafasi ya kuwapa pole sana wake zote wa marehemu wa Masaburi. Inawezekana tukasema ana watoto 20, lakini ninavyojua ana watoto zaidi ya 20.” Amesema Rais Mgufuli na kusababisha umati wore kuangua kucheko na vigelegele.
Katika tukio hilo mbali na Magufuli pia marais wastaafu na walikuwepo akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Dk.Garib Bilal, Ali Hasan Mwinyi na wengineo wakiwemo wabunge na mabalozi.
Rais Magufuli akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Dk.Didas Masaburi wakati kuaga mapema leo Jijini Dar eS alaam katika viwanja vya Karimjee.
PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE-MODEWJI BLOG
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni