MSHAMA AWAPA MWEZI MMOJA WAKAZI WA KAZAMOYO ZAIDI YA 600 HUKO SOGA KULIACHIA ENEO
Mkurugenzi halmashauri ya wilaya 
ya Kibaha, Tatu Selemani akielezea jambo kwa wananchi wa Soga, 
walioshiriki kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama
 wakati alipokwenda kuzungumza hatima ya wana Kazamoyo . 
 (Picha na Mwamvua Mwinyi)
…………………………………………………………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Soga
WAKAZI zaidi ya 600 waliovamia 
shamba kwenye Kijiji cha Soga kata ya Soga wilayani Kibaha mkoani 
Pwani(KAZAMOYO)wamepewa mwezi mmoja kuhama kwenye shamba hilo ambalo 
limerudishwa mikononi mwa serikali.
Agizo hilo limekuja  baada ya aliyekuwa mmiliki wa shamba hilo Jangil Kasamal kunyanganywa kwa kushindwa kuliendeleza.
Mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama ,alisema agizo hilo ni kuanzia mwezi huu hadi Novemba 18 
baada ya kutoa miezi miwili tangu agosti hadi oktoba mwaka huu kuwataka waondoke lakini hawakufanya hivyo.
Alitoa kauli hiyo akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kwenye kijiji hicho.
Mshama alielezea kuwa watu hao 
hawako kisheria hivyo wanapaswa kuondoka ili shamba hilo lenye ukubwa wa
 hekari 900 litumike kwa shughuli nyingine za kijamii.
“Kamishna wa ardhi ameshatoa 
maelekezo juu ya shamba hilo kuwa baada ya hati ya umiliki kutenguliwa 
limerudishwa kwa halmashauri ambayo itaweka huduma za kijamii na si watu
 kujigawia kama wana Kazamoyo walivyofanya,” alisema Mshama.
Alisema wananchi hao ambao wengi 
wao wanatokea Jijini Dar es Salaam na kulipa jina eneo hilo kuwa 
Kazamoyo na kujiwekea uongozi wao ambao hauko kisheria kwa madai ya 
kushindwa kupatiwa huduma na uongozi wa kijiji cha Soga.
“Kutokana na hali halisi iliyopo 
na tangu mwanzo tulitoa maagizo muondoke kwani tayari wizara na vyombo 
husika vimeona kuwa taratibu za kukaa hapo zimekiukwa.
,” alisema Mshama.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya 
wilaya ya Kibaha Tatu Seleman alisema kuwa wamepata barua toka kwa 
waziri wa ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi ,Wiliamu Lukuvi ikisema 
kuwa watu hao wako hapo kinyume cha sheria.
Seleman alisema kuwa barua ya 
Waziri ilikuja baada ya wananchi hao kumwandikia barua wakitaka 
wamilikishwe eneo hilo ili wkae hapo kihalali.
Mmoja wa wakazi walioko kwenye 
eneo hilo alifafanua aliingia hapo baada ya kusikia eneo hilo linagawiwa
 ambalo lilikuwa shamba pori .
Awali Mery Kaijage alisema 
waliamua kuvamia shamba hilo na kugawana na kuanza kulima na kujenga 
kutokana na viongozi wa kijiji kuliuza eneo hilo kinyume cha sheria.
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni