Jumatatu, 31 Oktoba 2016

Magufuli alivyopokelewa na Kenyatta ikulu Nairobi



Maafisa wa Rais Uhuru Kenyatta, kwenye akaunti yake ya Twitter, wamepakia picha za jinsi Rais wa Tanzania John Magufuli alivyolakiwa ikulu, Nairobi.
Rais Magufuli akikagua gwaride la heshima
@UKenyatta
Rais Magufuli akikagua gwaride la heshima
Rais Magufuli na Rais Kenyatta
@UKenyatta
Rais Magufuli na Rais Kenyatta
Rais Kenyatta, Rais Magufuli na mkuu wa majeshi wa Kenya Jenerali Samson Mwathethe
@UKenyatta
Rais Kenyatta, Rais Magufuli na mkuu wa majeshi wa Kenya Jenerali Samson Mwathethe
Rais Kenyatta na Rais Magufuli wakiwa ikulu, Nairobi.
@UKenyatta
Rais Kenyatta na Rais Magufuli wakiwa ikulu, Nairobi.

Magufuli: Kenya ni mshirika wetu mkubwa Afrika

Magufuli: Kenya ni mshirika wetu mkubwa kibiashara Afrika
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa Kenya ndio mshirika nambari moja wa Tanzania katika uwekezaji na biashara barani Afrika.
Akizungumza katika ikulu ya rais jijini Nairobi mda mfupi baada ya kuwasili nchini Kenya,Rais Magufuli amesisitiza kuwa hakuna taifa jingine ambalo limewekeza nchini mwake kama Kenya.
Amesema kuwa kulingana na rekodi za uwekezaji nchini Tanzania kuna takriban kampuni 529 nchini humo kutoka Kenya ambazo zinaingiza takriban dola bilioni 1.7 kila mwaka huku takriban Watanzania 57,260 wakiwa wameajiriwa.
Rais huyo vilevile ametoa wito kwa Wakenya wanaotaka kuwekeza nchini Tanzania kuharakisha hatua hiyo.
Aidha ameongezea kuwa amekuwa akiwasiliana na rais Uhuru Kenyatta mara kwa mara na kiwakosoa wale wanaodhani kwamba uhusiano wake na rais wa Kenya una utata.
Rais John Pombe Magufuli na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta baada ya kiongozi huyo wa Tanzania kuwasili nchini Kenyai
BBC

Magufuli alakiwa na waziri wa mambo ya nje

Wizara ya mambo ya nje Kenya imepakia picha za Rais Magufulia kilakiwa uwanja wa ndege na waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bi Amina Mohamed. Bi Mohamed anawania wadhifa wa rais wa tume ya Umoja wa Afrika (AU).
Magufuli awasili Kenya
@ForeignOfficeKE
Rais Magufuli akipatiwa shada la maua na mshichana uwanja wa ndege
@ForeignOfficeKE
Rais Magufuli akipatiwa shada la maua na mshichana uwanja wa ndege
Rais Magufuli na Bi Amina Mohamed
@ForeignOfficeKE
Rais Magufuli na Bi Amina Mohamed
Magufuli akitia saini kitabu cha wageni
@ForeignOfficeKE
Magufuli akitia saini kitabu cha wageni

Kenya inataka nini ziara ya Magufuli?

Msemaji wa Rais Kenyatta, Manoah Esipisu, Jumapili aligusia baadhi ya mambo ambayo Kenya inatarajia kutoka kwa ziara ya Rais Magufuli nchini Kenya.
Alisema: “Ziara ya Rais huyu inatupatia fursa ya kufanya upya na kukoleza uhusiano wetu katika nyanja mbalimbali. Viongozi wa nchi hizi watashauriana kuhusu masuala mbalimbali ya pamoja katika ngazi ya taifa kwa taifa na kanda. Wataangazia sana masuala ambayo tayari kumekuwa na mazungumzo, na tunatarajia matokeo ya mazungumzo hayo kutangazwa.
“Masuala kadha yatajadiliwa, ikiwemo ada ya vibali vya kufanyia kazi ambayo raia wa Kenya hutozwa, pamoja na karo ya juu ambayo Wakenya hutozwa vyuo vikuu (Tanzania). Mashauriano kuhusu kuondoa vikwazo vya kibiashara baina ya nchi hizi mbili pia yatafanyika. Kadhalika, na muhimu sana katika mazungumzo hayo ni shughuli za magari ya kusafirisha watalii yanayovuka mipaka.
“Muhimu katika mashauriano haya itakuwa pia kufufuliwa kwa Tume ya Ushirikiano wa Pamoja na Tanzania (JCC) ambayo ni jukwaa ambalo linaweza kutumiwa kutangaza biashara na uwekezaji  baina ya nchi zote mbili.
“Rais Kenyatta  pia atazungumza na Rais Magufuli kumhusu Bi Amina Mohammed (waziri wa mambo ya nje wa Kenya) anayewania wadhifa wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.

Magufuli awasili ikulu, Nairobi

Rais Magufuli amewasili katika ikulu ya Nairobi ambapo amekagua gwaride la heshima. Pia amepigiwa mizinga 21 kama ilivyo ada kwa viongozi wa mataifa wanapozuru Kenya.

Mambo matano atakayoyafanya Magufuli akiwa Kenya

Wakati wa ziara yake ya siku mbili Kenya Rais Magufuli, kwa mujibu wa ikulu ya Tanzania, anatarajiwa:
  1. Atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta
  2. Atatoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta.
  3. Atahudhuria dhifa ya kitaifa atakayoandaliwa na mwenyeji wake Ikulu Jijini  Nairobi.
  4. Atatembelea kiwanda cha maziwa cha  Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi
  5. Atazindua barabara mchepuko (Southern By-pass) iliyopo jijini Nairobi.
C & P 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni