BALE ASAINI MKATABA MPYA REAL MADRID HADI 2022.
Mchezaji namba mbili kwa gharama kubwa ya usaji
li Gareth Bale amejitia kitanzi katika klabu ya Real Madrid kwa kusaini Mkataba mpya utakaomuweka hadi 2022.
Bale aliyevunja rekodi ya usajili akitokea timu ya Tottenham Hotspur mwaka 2-13 na baadaye Paul Pogba alivunja rekodi yake na kuwa mchezaji ghali kuliko wote duniani kwa usajili akitokea Juventus na kujiunga na timu yake ya Zamani ya Manchester United chini ya meneja mwenye maneno mengi kuliko wote Ligi Kuu ya Uingrereza, Jose Mourinho mwaka huu.
Tiyari ameisaidia Madrid kushinda vikombe vitano katika misimu mitatu ya nyuma ikiwemo ligi ya mabingwa Ulaya mara 2 huku akifunga magoli 62 katika michezo 135.
Kwa kusaini kwake anaungana na viungo wawili wa timu hiyo Luka Modric na Toni Kroos nao pia walisaini mikataba mipya mwezi huu.
Mkataba wa Bale unatajwa kuwa wa Euro 600,000 kwa wiki huku baada ya makato ya kodi ikiwa Euro 350,000
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni