MVUVI AFARIKI AKIVUA BAHARINI MICHEWENI PEMBA
Na Masanja Mabula –Pemba ..
MZEE mmoja anayejulikana kwa jina la Saleh Ali Mbwana mwenye umri wa miaka 45 mkaazi wa Maziwang’ombe Wilaya ya Micheweni amefariki dunia baada ya kuzama maji baharini akiwa katika shuhuli zake za uvuvi .
Akidhibitisha kutokea kwa tokeo hilo kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Kamishna Msaidizi Haji Khamis Haji amesema tukio hilo limetokea oktoba 20 mwaka huu majira ya saa saba za mchana katika bahari ya Maziwang’ombe .
Amesema kwamba kabla ya kifo chake , marahemu aliondoka nyumbani kwake kwenda baharini kuvua , na alifikutwa na mauti hayo katika bahari wakati akitekeleza shuhuli zake za uvuvi.
Kkufuatia kutokea kwa tukio hilo Kamanda Haji amewataka wananchi hususani wanaotoka maeneo ya ukanda wa bahari wanapokwenda kuvua au kulima mwani kufuatana na wenzao ili patakapo tokea hitilafu waweze kusaidiana .
“Wito wangu kwa wananchi ni kuacha kwenda baharini aidha kwa uvuvi au kulima mwani wakiwa mmoja mmoja , bali wafuatane na wenzao ili kuweza kusaidiana panapotokea matatizo ”alisisitiza.
Akizungumza baada ya uchunguzi daktari dhamana wa hospitali ya Wilaya ya Micheweni Dk Rashid Daudi Mkasha amesema chanzo cha kifo chake kimesababishwa na kukosa hewa baada ya kukaa nchini ya bahari kwa muda mrefu .
Alifahamisha kwamba kitendo cha kukaa chini ya maji baharini kumesababisha kunywa maji mengi na kupelekea kukosa uwezo wa kuvuta hewa kutokana na maji aliyokunywa bila kutegemea.
“Uchunguzi wa kitaalamu umebainisha kwamba kifo kimesababishwa na kunywa maji mengi wakati akiwa chini ya maji ya bahari pamoja na kukosa uwezo wa kuvuta pumzi ”alifahamisha.
Mashuda wa tukio hilo ambao hawakutaka kutajwa majina yao wameeleza kuwa kabla ya kifo chake Saleh aliondoka nyumbani kwake kuelekea baharini kutafuta riziki na kukutwa na mauti .
Mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ngudu na jamaa baada ya kufanyiwa uchunguzi na dk wa Serikali ambapo mazishi yake yalifanyika katika maburi ya Maziwang’ombe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni