Jumatatu, 31 Oktoba 2016

WATANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKIANA KATIKA KUTUNZA MAZINGIRA

Na: Frank Shija, MAELEZO.
WATANZANIA watakiwa kufanya jitihada za makusudi katika suala zima la utunzaji wa mazingira ikiwa ni hatua za kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Hali ya hewa na Tabia nchi.
Rai hiyo imetolewa leo na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua Tamasha la Kimataifa linalohusu Mabadiliko ya Tabia ya Nchi linalowakutanisha Wanasayansi, Watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na Mabadiliko ya Tabia ya nchi.
Amesema kuwa suala la Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia nchi siyo hadithi ni jambo ambalo lipo wazi kuwa ni janga ambalo ipo haja ya kuchukua hatua za makusudi katika kutatua changamoto zake.
“Wadau wote tuone haja ya kuyatunza mazingira yetu mwananchi na wadau wa mazingira kwa ujumla, ni muhimu kwa umoja wetu tukaongeza jitihada za kupanda miti katika maeneo yetu ili kukabiliana na hali tete ya uharibifu wa mazingira nchini”.Alisema Mama Samia.
Aidha alisema kuwa wakati sasa umefika wa kuacha uharibifu wa mazingira kuanzia leo na kuanza kuyatunza ili kukabiliana na athari za Mabadiliko hayo ya Hali ya Hewa na Tabia nchi.
Awali akimkaribisha Makamu wa Rais, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa umefika wakati wakuitazama upya mitaala yetu ili kutoa fursa kwa elimu ya mazingira inaingizwa katika masomo kuanzia ngazi ya msingi.
Aliongeza kuwa elimu ikitumika vizuri inaweza kusaidia kwa kuongeza uelewa miongoni mwa jamii hali itakayopelekea wananchi kutambua namna ya kukabiliana na athari za mabadiliko hayo na ikiwa ni pamoja na namna ya kuyahifadhi.
Mhandisi Manyanya alisema kuwa ni faraja kuona Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinamuenzi Mwl. Nyerere kwa Kuwa na Kigoda cha Mwalimu kinachohusiana na Mazingira kwani ni ukweli kwamba Mwalimu alikuwa Mwanamazingira na Muhifadhi wa Mazingira ndiyo maana utaona aliweza kuweka maeneo mengi ya Hifadhi za Taifa.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala alisema kuwa imekuwa ni kawaida duniani kote kuwa na Vigoda ambavyo utumiwa kama njia ya kuwaenzi baadhi ya watu kwa michango yao.
Wao kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanamuenzi Baba wa Taifa kwa kuwa na Kigoda cha Mwalimu ambacho kilianzishwa mwaka 2008 kikiwa kimoja na kuongeza kuwa mpaka kufikia sasa vimeanzishwa Vingine viwili ambacho kimoja kinahusu Elimu ya Maendeleo na kingine ndicho hiki cha Masuala ya Mazingira ambacho kinafanya kazi nzuri sana.
Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Mabadiliko ya Tabia ya nchi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amabye pia ndiye Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na Mabadiliko ya Tabia nchi, Profesa Pius Yanda amesema mkutano huo wa siku TANO utakuwa na jukumu kubwa la kujadili kwa kina namna bora ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabia ya nchi.

KONGAMANO LA BIASHARA KATI YA COMMORO NA TANZANIA KUFANYIKA ZANZIBAR


imagesNa Mwashungi Tahir -Maelezo Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya 361 ya Dar es salaam inaandaa Kongamano la pili la biashara baina ya Tanzania na Commoro.
Kongamano hilo ambalo linaratibiwa na Wizara ya Biashara , viwanda na masoko Zanzibar  litafanyika Novemba 19,2016, katika hoteli ya Seacliff iliyopo Kama nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Biashara, viwanda na masoko  Amina Salum Ali  wakati akizungumza na waandishi  wa habari huko ofisini kwake Migombani.
Waziri Amina amesema Mgeni rasmi anaetarajiwa 
kulifungua kongamano hilo ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein.
Amesema katika ufunguzi wa Kongamano hilo kutafanyika shughuli za uwasilishaji mada na majadiliano, mikutano ya ana kwa ana (B2B) na maonyesho ya wajasiriamali.
Ameongeza kuwa kutakuwa na mada zitazowakilishwa na kugusa maeneo ya uwekezaji,biashara na miundombinu ya usafirishaji wa bidhaa baina ya Tanzania na Comoro na kuangalia fursa na vikwazo katika biashara ili kurahisisha Sekta ya biashara.
Waziri Amina amesema kongamano hilo la biashara baina ya Tanzania na Commoro ni la pili, ambapo tamasha  la kwanza  kama hilo lilifanyika nchini Commoro  April 23, mwaka jana.
Akielezea kuhusu kongamano la kwanza, amesema washiriki zaidi ya hamsini kutoka Tanzania  wakiongozwa na aliekuwa Waziri wa Mambo ya nchi za nje Benerd Membe walishiriki Kongamano hilo.
“Kongamano la pili la biashara baina ya Tanzania na Commoro linatarajiwa kuwa na washiriki  zaidi ya mia moja wakiwemo wafanyabiashara, wawekezaji , wajasiriamali na wadau kutoka taasisi za umma” alisema waziri Amina.
Balozi Amina ameongeza kuwa  katika  kongamano  hilo atashauri  kuangaliwa upya suala la kodi  kwani wafanyabiashara wengi wamekuwa wakilalamikia  kodi iliyopo kati ya Tanzania na Comoro kuwa ni kubwa.
Naye Balozi wa Commoro  Elbadaoui Fakih amesema Tanzania imekuwa msaada mkubwa kwa nchi yake hasa kwa kusaidia  mambo mengi ikiwemo  biashara na masuala ya kiuchumi.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO AKUTANA NA WASAMBAZAJI WA GESI MAJUMBANI JIJINI DAR ES SALAAM


ngoo1
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiongoza kikao kilichoshirikisha kampuni zinazohusika na usambazaji wa gesi majumbani pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),  Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) na  Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja  nchini (PBPA).
ngoo2
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe (kushoto) pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),  Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) na  Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja  nchini (PBPA), wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa  yanatolewa na Waziri wa Nishati na Madini  Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani)
ngoo3
Watendaji kutoka kampuni zinazohusika na usambazaji wa  gesi majumbani  wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa  yanatolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
ngoo4
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo katika kikao hicho.
ngoo5
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Tanzania Association of Oil Marketing, Salum Busarara akieleza jambo katika kikao hicho

Rais Dk. Shein akutana na ujumbe wa JICA kutoka Japan


ksi1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Rais wa Taasisi ya Mashirikianoya Kimataifaya Japan(JICA) Bw.Yasushi Kanzaki alipofika Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]31/10/2016.
ksi2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Rais wa Taasisi ya Mashirikianoya Kimataifaya Japan(JICA) Bw.Yasushi Kanzaki (wa pili kulia) alipofika na ujumbe aliofuatana nao leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]31/10/2016.
ksi3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Rais wa Taasisi ya Mashirikianoya Kimataifaya Japan(JICA) Bw.Yasushi Kanzaki alipofika Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]31/10/2016.

KIGWANGALA:WANAWAKE WANAOFANYA NGONO BILA KINGA WANAUWEZEKANO MKUBWA WA KUPATA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI


Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya jamii wazee jinsia na Watoto Hamis Kigwangalaakiwa anazungumza na waandishi wa habari wanawake kuhusu tatizo la Saratani ya shingo ya Kizazi, katika Ukumbi wa Olasiti Lodge Jijini Arusha.,aliyepo kushoto kwake ni Dkt.Mathew Kasumuni kutoka hospital ya Mount Meru iliyopo jijini Arusha
Waandishi wa habari wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya jamii wazee jinsia na Watoto Hamis Kigwangala,Aliyepo kushoto kwake ni Dkt.Mwanahamis Ghembe kutoka Mountmeru Hospital
Waandishi wa habari wanawake wakifuatilia kwa karibu baadhi ya majibu ya yaliyokuwa yakijibiwa na madaktari walioendesha mafunzo,mafunzo hayo yalikwenda sambaba na upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi.

Magufuli alivyopokelewa na Kenyatta ikulu Nairobi



Maafisa wa Rais Uhuru Kenyatta, kwenye akaunti yake ya Twitter, wamepakia picha za jinsi Rais wa Tanzania John Magufuli alivyolakiwa ikulu, Nairobi.
Rais Magufuli akikagua gwaride la heshima
@UKenyatta
Rais Magufuli akikagua gwaride la heshima
Rais Magufuli na Rais Kenyatta
@UKenyatta
Rais Magufuli na Rais Kenyatta
Rais Kenyatta, Rais Magufuli na mkuu wa majeshi wa Kenya Jenerali Samson Mwathethe
@UKenyatta
Rais Kenyatta, Rais Magufuli na mkuu wa majeshi wa Kenya Jenerali Samson Mwathethe
Rais Kenyatta na Rais Magufuli wakiwa ikulu, Nairobi.
@UKenyatta
Rais Kenyatta na Rais Magufuli wakiwa ikulu, Nairobi.

Magufuli: Kenya ni mshirika wetu mkubwa Afrika

Magufuli: Kenya ni mshirika wetu mkubwa kibiashara Afrika
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kuwa Kenya ndio mshirika nambari moja wa Tanzania katika uwekezaji na biashara barani Afrika.
Akizungumza katika ikulu ya rais jijini Nairobi mda mfupi baada ya kuwasili nchini Kenya,Rais Magufuli amesisitiza kuwa hakuna taifa jingine ambalo limewekeza nchini mwake kama Kenya.
Amesema kuwa kulingana na rekodi za uwekezaji nchini Tanzania kuna takriban kampuni 529 nchini humo kutoka Kenya ambazo zinaingiza takriban dola bilioni 1.7 kila mwaka huku takriban Watanzania 57,260 wakiwa wameajiriwa.
Rais huyo vilevile ametoa wito kwa Wakenya wanaotaka kuwekeza nchini Tanzania kuharakisha hatua hiyo.
Aidha ameongezea kuwa amekuwa akiwasiliana na rais Uhuru Kenyatta mara kwa mara na kiwakosoa wale wanaodhani kwamba uhusiano wake na rais wa Kenya una utata.
Rais John Pombe Magufuli na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta baada ya kiongozi huyo wa Tanzania kuwasili nchini Kenyai
BBC

Magufuli alakiwa na waziri wa mambo ya nje

Wizara ya mambo ya nje Kenya imepakia picha za Rais Magufulia kilakiwa uwanja wa ndege na waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bi Amina Mohamed. Bi Mohamed anawania wadhifa wa rais wa tume ya Umoja wa Afrika (AU).
Magufuli awasili Kenya
@ForeignOfficeKE
Rais Magufuli akipatiwa shada la maua na mshichana uwanja wa ndege
@ForeignOfficeKE
Rais Magufuli akipatiwa shada la maua na mshichana uwanja wa ndege
Rais Magufuli na Bi Amina Mohamed
@ForeignOfficeKE
Rais Magufuli na Bi Amina Mohamed
Magufuli akitia saini kitabu cha wageni
@ForeignOfficeKE
Magufuli akitia saini kitabu cha wageni

Kenya inataka nini ziara ya Magufuli?

Msemaji wa Rais Kenyatta, Manoah Esipisu, Jumapili aligusia baadhi ya mambo ambayo Kenya inatarajia kutoka kwa ziara ya Rais Magufuli nchini Kenya.
Alisema: “Ziara ya Rais huyu inatupatia fursa ya kufanya upya na kukoleza uhusiano wetu katika nyanja mbalimbali. Viongozi wa nchi hizi watashauriana kuhusu masuala mbalimbali ya pamoja katika ngazi ya taifa kwa taifa na kanda. Wataangazia sana masuala ambayo tayari kumekuwa na mazungumzo, na tunatarajia matokeo ya mazungumzo hayo kutangazwa.
“Masuala kadha yatajadiliwa, ikiwemo ada ya vibali vya kufanyia kazi ambayo raia wa Kenya hutozwa, pamoja na karo ya juu ambayo Wakenya hutozwa vyuo vikuu (Tanzania). Mashauriano kuhusu kuondoa vikwazo vya kibiashara baina ya nchi hizi mbili pia yatafanyika. Kadhalika, na muhimu sana katika mazungumzo hayo ni shughuli za magari ya kusafirisha watalii yanayovuka mipaka.
“Muhimu katika mashauriano haya itakuwa pia kufufuliwa kwa Tume ya Ushirikiano wa Pamoja na Tanzania (JCC) ambayo ni jukwaa ambalo linaweza kutumiwa kutangaza biashara na uwekezaji  baina ya nchi zote mbili.
“Rais Kenyatta  pia atazungumza na Rais Magufuli kumhusu Bi Amina Mohammed (waziri wa mambo ya nje wa Kenya) anayewania wadhifa wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.

Magufuli awasili ikulu, Nairobi

Rais Magufuli amewasili katika ikulu ya Nairobi ambapo amekagua gwaride la heshima. Pia amepigiwa mizinga 21 kama ilivyo ada kwa viongozi wa mataifa wanapozuru Kenya.

Mambo matano atakayoyafanya Magufuli akiwa Kenya

Wakati wa ziara yake ya siku mbili Kenya Rais Magufuli, kwa mujibu wa ikulu ya Tanzania, anatarajiwa:
  1. Atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta
  2. Atatoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta.
  3. Atahudhuria dhifa ya kitaifa atakayoandaliwa na mwenyeji wake Ikulu Jijini  Nairobi.
  4. Atatembelea kiwanda cha maziwa cha  Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi
  5. Atazindua barabara mchepuko (Southern By-pass) iliyopo jijini Nairobi.
C & P