KAMPUNI YA MANTRA YAMWAGA MSAADA WA MADAWATI KWA SHULE ZA MSINGI WILAYANI SONGEA
Mkuu
wa mkoa wa Ruvuma, Dkt. Bilnith Mahenge (kushoto) akisalimiana na
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mantra Tanzania, Frederick Kibodya
alipofika katika kata ya Majengo kupokea msaada wa madawati 500
yaliyotolewa na kampuni hiyo.
Mtendaji
kata ya Majengo katika manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, Yusuf Mshamu
(kulia) akimpokea Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Bilnith Mahenge
aliyetembelea katika kata hiyo kupokea msaada wa madawati 500 yenye
thamani ya shilingi milioni 40 yaliyotolewa na kampuni ya Mantra
Tanzania inayofanya utafiti wa madini ya Uran katika mto Mkuju wilayani
Namtumbo.
Sehemu
ya madawati 500 yaliyotolewa na kampuni ya Mantra Tanzania yakiwa
tayari kabla ya kukabidhiwa kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Dkt. Bilinith
Mahenge yatakayosambazwa katika shule za msingi wilayani Songea kwa
ajili ya kukabilianana upungufu wa madawati.
Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Bilinith Mahenge wa kwanza mbele akikagua
sehemu ya madawati 500 yaliyotolewa na kampuni ya Mantra Tanzania
inayofanya utafiti wa madini ya Uran katika mto Mkuju wilayani Namtumbo
mkoani humo,katikati nni mkuu wa wilaya ya Songea Oraleti Komando Mgema
na wa kwanza kushoto ni mkurugenzi mkuu wa Mantra Frederick Kibodya.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Mantra inayofanya utafiti wa madini ya Uran katika
mto Mkuju wilayani Namtumbo, Frederick Kibodya (kushoto), akikabidhi kwa
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Bilinith Mahenge moja kati ya madawati 500
yenye thamani ya shilingi milioni 40 ili yasaidie kupunguza tatizo la
madawati kwa shule za msingi mkoani Ruvuma.
Mkuu
wa mkoa wa Ruvuma Dkt Bilinith Mahenge akikabidhi moja ya madawati 500
yaliyotolewa na kampuni ya Mantra Tanzania kwa Mkuu wa Wilaya ya
Songea, Oraleti Komando Mgema ili yasaidie kupunguza uhaba wamadawati
kwa shule za msingi wilayani humo.
Mkuu
wa mkoa wa Ruvuma Dkt Bilinith Mahenge akizungumza na
wananchi,viongozi na wawakilishi wa kampuni ya Mantra Tanzania katika
viwanja vya stendi ya malori kata ya Majengo katika manispaa ya Songea
baada ya kupokea msaada wa madawati 500 kutoka kwa kampuni ya Mantra
inayofanya utafiti wa madini ya Uran katika mto Mkuju wilayani Namtumbo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni