“NAVY KENZO KUMSINDIKIZA MISS TANGA 2016”
NA, MWANDISHI WETU TANGA
MSANII
wa Mziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania Navy Kenzo anatarajiwa
kutumbuiza kwenye shindano la kumtafuta malkia wa Mkoa wa Tanga Miss
Tanga 2016 litakalofanyika Julai 29 mwaka huu kwenye ukumbi wa Hotel ya
Tanga Beach Resort.
Licha
ya Navy Kenzo wasanii wengine ambao watasindikiza onyesho hilo kwa
kutoa burudani ni kundi la mziki wa kizazi kipya mkoani Tanga,Wazenji
Classic pamoja na Dances.
Akizungumza
jana,Mratibu wa Onyesho hilo, alisema kuwa maandalizi ya kuelekea
shindano hilo yanaendelea vizuri ambapo tayari warembo watakaoshiriki
wameanza kuingia kambini .
Shindano
hilo ambalo limeandaliwa na kituo cha Radio cha TK FM 88.5 kilichopo
mjini Tanga kwa kushirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort wameelezea
namna walivyo jipanga kuhakikisha onyesho hilo linakuwa na ushindani
mkubwa kutokana na aina ya warembo waliopo .
“Nisema tu tumejiandaa vizuri kuhakikisha shindano hilo linafanyika kwa
umakini mkubwa ili kuwawezesha wadau wa tasnia ya urembo mkoani hapa
kuweza kupata ladha halisi ya onyesho hilo kwani licha ya kuwaona
warembo wakali wakini pia mzee wa kamatia chini atakuwepo kuwapagawisha
“Alisema.
“Alisema.
Hata
hivyo alisema kuwa mazoezi ya warembo watanaoshiriki onyesho hilo
yanaendelea kwenye ukumbi wa New Hotel uliopo mjini hapa kuanzia saa
kumi jioni.
Aidha
alisema kuwa kabla ya kufanyika shindano hilo warembo hao watapata
fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii mkoani hapa
ikiwemo Mapango ya Amboni na Hifadhi ya Taifa ya Saadani.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
KING CASINO, LLC GIVES A $100 FREE BET
JibuFutaKING CASINO, LLC GIVES A $100 FREE jancasino.com BET https://jancasino.com/review/merit-casino/ to try. Visit us today and receive 출장안마 a $100 FREE BET! Sign herzamanindir.com/ up at our new https://octcasino.com/ site!