Jumatatu, 18 Julai 2016

MKUU WA WILAYA MJINI ZANZIBAR AZINDUA MABARAZA YA VIJANA JIMBO LA MAGOMENI.

1Brasbend ya Chipkizi ikiongoza maandamano ya uzinduzi wa mabaraza ya vijana Jimbo la Magomeni katika shamrashamra za uzinduzi wa mabaraza hayo uliofanyika uwanja wa Magae Meya Mjini Zanzibar.
2Sabra Abdalla Amer akisoma risala ya vijana katika uzinduzi wa mabaraza ya vijana Jimbo la Magomeni.
3Mwenyekiti wa mabaraza ya Vijana Jimbo la Magomeni Kassim Lila Msoma akimkaribisha mgeni rasmin katika uzinduzi wa mabaraza ya vijana Jimbo la Magomeni, Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bi. Marina  Joel Tomas (hayupo pichani).
4Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bi. Marina Joel Tomas akizungumza na Vijana wa Jimbo la Magomeni katika uzinduzi wa mabaraza ya Vijana Jimbo la Magomeni kabla yakulizindua rasmin Baraza hilo Julay 16, (kulia) Mbunge wa Jimbo hilo Jamal Kassim Ali na (kushoto) Mwenyekiti wa mabaraza ya Vijana Jimbo la Magomeni Kassim Lila Msoma.
5Baadhi ya Vijana wa mabaraza ya vijana Jimbo la Magomeni wakimsikiliza Mgeni rasmin Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bi. Marina Joel Tomas hayupo (pichani) wakati wa uzinduzi huo.
6Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bi. Marina Joel Tomas na Mbunge wa Jimbo la Magomeni Jamal Kassim Ali wakiwapungia mkono Vijana kuwaaga baada ya uzinduzi wa mabaraza ya Vijana Jimbo la Magomeni.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
………………………………………………………………………………………..
Na Maryam Kidiko/Maelezo Zanzibar.  
“Serikali ni muhimu kusimamia tamaduni na mila za kizanzibar ili sisi vijana tuweze kufata njia walizopita viongozi wetu na sio kuvuruga mila hizo” Alisema Mwenyekiti huyo.
Akizitaja changamoto mbali mbali zinazowakabili katika jimbo lao alisema vijana hawana elimu ya kutosha ya ujasiriamali hivyo hupelekea vijana wengi kutegemea ajira kutoka Serikalini jambo ambalo hurejesha nyuma maendeleo ya vijana na kujiingiza katika utumiaji wa madawa ya kulevya pamoja na uhalifu .
Hata hivyo alisema vijana hawana ofisi, vianzio vya kuanzishia miradi pamoja na vitendea kazi vitavyoweza kuwaendeshea miradi mbali mbali katika mabaraza yao.
Uzinduzi wa mabaraza ya vijana umefikia mwisho kwa Wilaya ya Mjini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni