Waziri Mkuu Mgeni Rasmi Kongamano la ushiriki wa watanzania katika uwekezaji.


Picha na Daudi Manongi,MAELEZO
…………………………………………………………………………………..
Na Daudi Manongi -MAELEZO -Dar es Salaaam
SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri
Mkuu imeandaa kongamano kongamano la siku mbili la uwekezaji
litakalojadili mipango madhubuti ya kuhakikisha Watanzania wanashiriki
kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.
Kongamano hilo linatarajia kufanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 -22 Julai mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo Jijiji Dar es
Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt.Hamis
Issa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu kongamano
hilo.
Dkt. Issa alisema Serikali
imepitisha Sera ya ushiriki wa watanzania katika sekta ya Mafuta na Gesi
asilia, hatua ambayo itasadia wananchi wazawa kushiriki kikamilifu
katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.
“Msukumo mkubwa wa serikali kwa
sasa ni kuongeza ushiriki katika uwekezaji unaochochewa na ugunduzi
mkubwa wa gesi asilia katika kina kirefu cha bahari ambao utaweza
kuwanufasha Watanzania” alisema Dkt. Issa.
Aidha alisema kuwa kutokana
ushiriki huo wa Watanzania kuwa suala mtambuka na agenda endelevu,
Serikali iliiagiza Baraza la Taifa la Uwezeshaji kuanzisha Idara ya
ushiriki wa watanzania katika uwekezaji ambayo imeanza kutekeleza
majukumu yake mwezi Novemba mwaka 2015.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Beng’i Issa alisema kuwa katika kongamano
hilo linatarajia kushirikisha jumla ya wajumbe 350 wakiwemo
wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, Watendaji wa Serikali Kuu na
halmashauri za Miji na Majiji.
Akizungumzia kuhusu manufaa ya
kongamano hilo, Beng’i alisema Watanzania watanufaika zaidi kwa kuwa
wataongeza ujuzi na uzoefu katika kushirikiana na wafanyabiashara
wakubwa waliopo nje ya nchi wanaojihusisha na sekta za mafuta, gesi,
kilimo, fedha, bima, ujenzi na manunuzi ya umma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni