MAKOCHA TANZANIA WAANZA KUIVA

Kidao amesema japo kozi hiyo
ilikuwa hatua ya kwanza ‘Module 1’ kwa sasa wameiva kiasi kwamba
watakapomaliza Novemba, mwaka huu wana uhakika wa kupeleka vyeti vyao
sehemu yoyote duniani kuomba kazi na kushinda kwa kuwa wameiva vilivyo.
Wakufunzi wa kozi hiyo walitokea CAF, Sunday Kayuni na Salum Madadi
ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF.
Baada ya kusikiliza kauli hiyo ya
Kidao, Rais wa TFF Jamal Malinzi moja kwa moja akawasisitiza makocha
hao kufanya kazi kwa juhudi na kuwaeleza kuwa hatua waliyofikia ni kubwa
kwa kuwa baadhi ya makocha kutoka nje hawana vyeti na kukosa sifa ya
kufundisha timu kubwa ikiwamo timu za mataifa ngazi mbalimbali.
Rais Malinzi alitaka makocha hao
kuangazia mpira wa miguu kwa wavulana wengi wakiwa wanatokea katika
mashindano yanayodhaminiwa na Kampuni ya simu ya Airtel pamoja na soko
la wasichana ambalo kwa sasa linashika chati kila kona ya dunia.
Naye, Makamu wa Rais wa TFF,
Wallace Karia alimpongeza Rais Malinzi kwa namna anavyoratibu na
kuzikubali kozi mbalimbali za waamuzi na makocha. “Kwa muda mrefu au
tuseme kwa miaka mingi hakujafanyika kozi nyingi kama kipindi cha
uongozi wako ukisaidiana na mimi pamoja na kamati nzima ya utendaji
pamoja na sekretarieti.”
“Fanyeni utafiti ninyi makocha.
Utaona kuwa sehemu kubwa nchi za Afrika zimefanikiwa kwa kutumia makocha
wazawa. Leo ninyi ni makocha wa ngazi ya juu kabisa hivyo mna uwezo wa
kufanya vema na kusaidia timu zetu na timu za taifa,” alisisitiza Karia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni