Ijumaa, 14 Agosti 2015

JWTZ YAWAPA ONYO KALI WANASIASA






 



 



JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ), limekanusha kuwanyang'anya kadi za kupigia kura maofisa na askari wake kama ilivyodaiwa na mmoja wa viongozi wa chama kimoja cha siasa na kutolewa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii



 



Amezungumza hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na  waandishi  habari Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kanali Ngemela Lubinga alisema madai hayo siyo ya kweli na kuwa jeshi hilo halijafanya hivyo na wala haliwezi kufanya hivyo.



 



“Wanajeshi hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama chochote cha kisiasa na kuwa mwanajeshi haruhusiwi kuwa shabiki wa chama chochote cha kisiasa”alisema Lubinga.



 



Lubinga alisema Jeshi la Wananchi Tanzania linafanya kazi zake kama 'professional state organ duniani na kuwa mwanajeshi anayekiuka huchukuliwa hatua za kinidhamu za kijeshi wala si za kiraia.



Alisema Jeshi la Wananchi Tanzania limesikitishwa na kauli hiyo iliyotolewa na kiongozi



huyo na amewatakaWananchi na viongozi wa kisiasa wafanye kazi zao za kisiasa na zisianzishwe hoja nje ya maeneo hayo ya kisiasa kwani lugha hizo za upotoshaji zinaweza kuleta hofu, ukakasi na wasiwasi kwa Wananchi.



 



Aliongeza kuwa jeshi hilo linaendelea na shughuli zake kama kawaida halipendi litolewe kauli za upotoshaji, kusikoeleweka ufuatwe utaratibu wa kuuliza kupata majibu ya uhakika kwani Wananchi wanaimani na jeshi lao.

 



Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),


NAPE:WANAOIKIMBIA CCM NI OIL CHAFU

Na Tinah Reuben

KATIBU mwenezi na itikadi wa CCM Nape Nnauye amekanusha habari zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa mgombea wao wa uraisi John Pombe Magufuli amehaidi kuwapatia kompyuta mpakato  kila mwalimu pamoja na kila kijiji kupatiwa milioni 50.

Nape amezungumza hayo leo Jijini Dar es salaam alipokuta na Waandishi wa Habari alipokuwa anatoa taarifa hiyo iliyokanusha na kusema kuwa waliotoa taarifa hiyo wanalengo lakuwachafua na kutaka waonekana wameanza kampeni mapema.

Alisema hakuna sehemu ambayo Magufuli aliwahi kuongea kauli hiyo na anawashangaa watu pamoja na mitandao ya kijamii inayoeneza ujumbe huo ambao sio wa kweli hata kidogo.

Aliongeza kuwa wapo watu wasioitakia mema CCM na kwamba wamebaini mbinu hizo chafu na wanazifanyia kazi.



"Watu walianda waraka ule walidai kuona umeandikwa katika ilani ya CCM kitu ambacho sio kweli kwani Ilani imetoka rasmi jana",alisema Nape.

Akitolea ufanunuzi kuhusu kuhama kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja,Nape alisema kuwa Mgeja alijitoa baada ya mwanaye wa Kike kushindwa katika mchakato wa Viti maalum mkoa wa Shinyanga.

Alisema kuwa baada ya mwanae kushindwa Mgeja alitaka chama kimbebe mwanae kinyume cha misingi ya chama na alipokataliwa alikasirikia na kutangaza uamuzi wake wa kukihama cham.

"Watu walikimbia CCM wamekimbia kwa mabaya yao pia walionzisha vyama upinzani wote misingi yao ni CCM na kama wanaondoka atushangai.....kwanza walioaznisha hivyo vyama hawajafanikiwa na wanaokwenda hawata fanikiwa,"alisema Nape

Aliongeza kuwa kitendo cha wanachama hao kujiondoa CCM nisawa na fundi anayetoa Dizeli chafu ndani ya injini ya Gari na kuwepa safi.

Alisema kuwa anawashangaa wapinzani wanavyopokea dizeli chafu zinazopelekea injini zao kuwa mbovu na zosizofa kabisa.

Aidha alisema kwa kawadia chama kinautaratibu wa kupokea wanachama wapya hivyo ni kitendo cha kushangaza kuona wapinzani wanapokea wanachama walioshindwa katika vyama vyao.

Ijumaa, 8 Mei 2015

ACT-Wazalendo: Tunasubiri Ukawa watukaribishe kwenye umoja


Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mgwhira amesema hawana matatizo na Ukawa na kwamba wanachosubiri hadi sasa ni majibu ya barua yao kuomba kujiunga na muungano huo.
Alitoa kauli hiyo juzi wakati viongozi wa chama walipofanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Meru na kugawa vitu mbalimbali kwenye wodi ya wajawazito.
“Hatuna matatizo na Ukawa, tunaunga mkono muungano wowote wa upinzani ulio halali,” alisema kiongozi huyo.
Alisema tangu wawasilishe maombi yao, bado hawajapata mrejesho, hivyo wanaendelea kusubiri.
Akifafanua kuhusu barua hiyo, alisema waliomba mwongozo wa namna ya kujiunga na Ukawa.
Alisema chama chao kimepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi katika mikoa mbalimbali na hilo lilithibitika katika awamu ya kwanza ya ziara yao.
Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimesababisha mafuriko makubwa na kulazimisha baadhi ya wananchi kukimbia makazi yao.

Jumanne, 21 Aprili 2015

TMA YALENGA KUKIDHI MAHITAJI KATIKA SEKTA MBALIMBALI NCHINI

 

 

 Wataalamu  mbalimbali kutoka Mamlaka ya hali ya hewa wakiwa katika picha ya pamoja.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa Dkt Agnes Kijazi akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa wastaalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali.

Baadhi  ya washiriki wakifuatilia kwa kina mkutano huo uliofanyikia katika ukumbi wa Hotel ya Bluepearl jijini Dar es Salaam


MAMLAKA ya ali ya hewa nchini (TMA) imesema ipo katika mkakati wa kubadilisha mfumo wa kuhifadhi takwimu za hali ya hewa kutoka mfumo wa analogia kwenda digitali.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk.Agnes Kijazi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari na kufafanua kuwa katika kutimiza hilo walisaini makubaliano ya kushirikiana na ofisi ya hali ya hewa Uingereza ambapo mambo makuu ilikuwa ni kuhakikisha watumiaji wa huduma za hali ya hewa nchini wanaridhika na huduma zitolewazo lengo ikiwa ni kuboresha mfumo wa kuhifadhi takwimu.

“Kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni TMA imekuwa ikikutana na wadau wa Sekta mbalimbali na kupata maoni yao juu ya huduma zitolewazo pamoja na kubadilisha namna ya uhifadhi wa takwimu za hali ya hewa ambapo kwa kupitia maoni hayo tumeona ni wakati muafaka wa kuwakutanisha wataalamu wa hali ya hewa kutoka vitengo mbalimbali ili kujadili na kupata suluhisho la kuboresha huduma zetu,”amesema Kijazi.

Aidha amesema katika mkutano huo ambao umewahusisha pia wakuu wa kanda kutoka TMA na wasimamizi wa vituo vya hali ya hewa vinavyoendeshwa na mamlaka vilivyopo nchini, washiriki watapata fursa ya kujadili na kutolea maamzi maoni ya wadau wa sekta ya kilimo, nishati, maji, afya na habari na pia kujipanga  katika kuwafikia wadau wengine.

Ameongeza kuwa mbali na changamoto za uwepo wa taarifa nyingi za hali ya hewa zilizo kwenye makaratasi ambazo wanataka kuziweka katika mfumo wa kidigitali pia wanakibiliwa na ukosefu wa ofisi maalumu ya kufanyia kazi suala ambalo wanalishighulikia hivi sasa pamoja na upungufu wa wataalamu na vituo vya hali ya hewa ambapo kwa sasa wanavyo vituo 28 wakati malengo yao ni kuwa na vituo 70.

Kijazi amesema kuwa mara kwa mara wamekuwa wakitumia maoni wanayoyapata kutoka kwa wadau mbalimbali hasa wakulima kwa kuangalia mahitaji binafsi kulingana na sekta yao pale wanapotaka kufahamu vipindi vya mvua ili kujiandaa na shughuli za kilimo alikadhalika vipindi vya ukame.

Amesema mbali na wakulima kutaka kupata taarifa za misimu ya mvua pia huhitaji kujua vipindi vya upepo mkali ili kuweka tahadhari kwa ajili ya kulinda mimea kama migomba na matunda kwa kuweka miti ili isianguke ukiachana na taarifa za jumla kwa ajili ya watu mbalimbali ambazo hutolewa na dawati lao.

Jumapili, 19 Aprili 2015

POLISI WAVAMIA VITUO VYA MAFUNZO YA DINI YA KIISLAM DODOMA.


Jeshi la polisi Mkoa wa Dodoma limeweka chini ya ulinzi na kufanyia uchunguzi vituo vitatu vilivyokusanya watoto 115 kutoka mikoa 13 Nchini kwa lengo la kuwapatia mafunzo ya dini ya kiislamu.

 

Vituo hivyo vyote vipo katika eneo la Nkuhungu,lililopo katika manispaa ya Dodoma.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alisema wanafanya uchunguzi katika vituo hivyo kutokana na kuhusika  kuendesha vituo vya kulelea watoto bila kusajiliwa na hatarishi.

 

"Jana saa saa sita usiku tulifanya upekuzi katika vituo vitatu,katika kituo cha kwanzatukafanikiwa kupata watoto takribani 63,kati yao 46chini ya miaka 18.

 

Katika  kituo cha pili tulikuta watoto 40,kati yaowalio chini ya umri miaka 18 walikuwa 12 na kituo cha tatu tulikuta  watoto saba  ,kati yao walio chini ya umri miaka 18 ni watano".Alisema Misime.

 

Alisema katika idadi watoto hao,63 wana umri chini ya miaka 18 na wengine 52 umri wao ni miaka 25,na wote ni wanaume wengi  wanatoka Wilaya ya Kondoa ambao ni 50 na 26 wanatokea katika \wilaya ya Dodoma mjini,Chamwino na Mpwapwa.

 

"Watoto wanaosalia wanatokea  mikoa ya Kagera,Dar es Salaam,Kilimanjaro,Zanzibar,Tanga,Tabora

Singida,Pwani,Lindi,Mtwara,Geita,Mwanza na Manyara".Alisema Misime.

 

Alisema watoto hao walikutwa usiku wakiwa wamechanganywa bila kujali umri wao,jambo ambalo ni hatarishi.

 

"Uchunguzi unaendelea na yeyote atayeguswa na ushahidi kuwa amekiuka sharia,atafikishwa mahakamani ikiwepo wazai walioruhusu watoto hao kuwa katika uangalizi amao si wa kutosha kama sharia ya motto ya mwaka 2009 inavyoelekeza".Alisisitiza Misime.

 

Akizungumzia tukio hilo,Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mustafa Rajab,alisema hakuna dhambi yeyote kwa watoto hao kulelewa katika kituo hicho.

 

"Hayo ni mafunzo katika madrasa  ambazo zilianza zamani ulimwenguni kote,polisi haina mamlaka ya kufunga madrasa labda kama watakuta kuna tatizo lolote la kuhatarisha amani"Alisema Rajab.

 

Walikizungumza katika eneo hilo,baadhi ya watoto walisema wapo hapo kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya dini ya kiislam

 

" Mimi nimetoka Kondoa lakini nilipokuja hapa nimeandikishwa Shule ya msingi Nkuhunhu,nikimaliza kusoma dini hapa huwa nakwenda shuleni".Alisema mmoja wa watoto hao

 

Mmoja wa majirani Mama Naomi alisema siku zoteamekuwa akiwaona watotro hao wakishinda hapo na hajawahi kuwaona wakienda shule kusoma.

 

"Chakula na kuni za kupikia huwa wan aletewa na walimu wao,wanajipikia wenyewe,watoto wadogo kazi yao ni kuosha vyombo."Alisema Mama Naomi.

.









 

LOWASA AUNGANA NA WANANCHI KATIKA MATEMBEZI YA KUPINGA MAUAJI YA ALBINO

 




 



 Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye pia ni Munge wa Monduli akiongoza matembezi  matembezi hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Matembezi hayo yaliyoandaliwa na vijana wa TEMEKE yaliyoanzia katika uwanja wa Taifa na kumalizika katika viwanja vya  TTC Changombe jijini Dar es Salaam



 



Baadhi ya Wananchi waliojitokeza katika kuunga matembezi hayo ya kulaani na kupinga mauaji ya albino. jijini DAR ES salaam.



Mheshimiwa Lowassa akiwa pamoja na baadhi ya Wananchi katika matembezi hayo.