Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mgwhira amesema hawana
matatizo na Ukawa na kwamba wanachosubiri hadi sasa ni majibu ya barua
yao kuomba kujiunga na muungano huo.
Alitoa kauli hiyo juzi wakati viongozi wa chama walipofanya ziara ya
kutembelea Hospitali ya Meru na kugawa vitu mbalimbali kwenye wodi ya
wajawazito.
“Hatuna matatizo na Ukawa, tunaunga mkono muungano wowote wa upinzani
ulio halali,” alisema kiongozi huyo.
Alisema tangu wawasilishe maombi yao, bado hawajapata mrejesho, hivyo
wanaendelea kusubiri.
Akifafanua kuhusu barua hiyo, alisema waliomba mwongozo wa namna ya
kujiunga na Ukawa.
Alisema chama chao kimepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi katika
mikoa mbalimbali na hilo lilithibitika katika awamu ya kwanza ya ziara
yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni