Jumapili, 3 Aprili 2016

RAIS DKT. MAGUFULI NA  ODINGA WASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA PILI YA PASAKA CHATO MKOANI GEITA.

G1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  Waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga wakisali katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli amesali ibada ya jumapili ya pili ya Pasaka tangu kuchaguliwa kuwa Rais.G5Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga pamoja na Mke wa Raila Bi. Ida Odinga wakifatilia kwa makini mahubiri ya Paroko  Padre Henry Mulinganisa katika ibada ya pili ya pasaka Chato Mkoani Geita.G7Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.G8Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisali katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.G2Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Bi. Ida Odinga, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Raila Odinga pamoja na Rais Dkt. John Magufuli wakifatilia kwa makini mahubiri yaliyokuwa yakitolewa katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.G12Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga, Mke wa Raila Bi. Ida Odinga pamoja na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakishukuru mara baada ya ibada.G6Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Sakramenti takatifu kutoka kwa Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Chato Padre Henry Mulinganisa 


G3Kikundi cha Kwaya ya vijana wakiimba katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.G9Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waumini wa kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita. Rais Dkt. Magufuli amechangia kiasi cha Shilingi milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa jipya la la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.G10Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiwasalimia waumini wa kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.G11Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Bi. Ida Odinga pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakifurahia salamu zilizokuwa zikitolewa na Raila  Odinga katika kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.G4Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono kutakiana amani ya bwana na masista wa kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.G13Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Raila Odinga wakiagana na waumini wa kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.G14Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Sista Maria Theleza Ntihabose wa kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
PICHA NA IKULU
……………………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye yupo mapumzikoni nyumbani kwake Lubambangwe katika kijijini cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita, kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais, ameungana na waumini wenzake wa Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato, kusali ibada ya Jumapili ya Pili ya Pasaka ambapo pamoja na mambo mengine amewahusia watanzania wote  kuendelea kuliombea Taifa ili liendelee kuwa na amani.
“Niwaombe watanzania wote tuendelee kushirikiana na kushikamana, kwa umoja wetu na siku zote tumtangilize Mungu mbele. Wakati tunaadhimisha wiki moja baada ya kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, Yesu Kristo alikufa kwa sababu ya dhambi zetu, sisi wote tujitahidi kufuata matendo ya Yesu Kristo ya kusameheana, kupendana, kushirikiana na tusibaguane” Amebainisha Rais Magufuli
Pamoja na Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, ibada hiyo imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Amoro Odinga na Mkewe Mama Ida Odinga, ambao ni familia rafiki wa Rais Magufuli, waliowasili hapa Chato jana jioni Tarehe 02 April, 2016 kwa mapumziko wakitokea Nairobi, Kenya.
Katika salamu zake kwa waumini wa Parokia ya Chato, Mheshimiwa Odinga amewashukuru watanzania kwa uhusiano mzuri walionao na wakenya, huku akitoa mfano wa jinsi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyojitoa kupigania uhuru wa mataifa mengi ya Afrika ikiwemo Kenya.
Mheshimiwa Odinga ametoa mfano wake mwenyewe kuwa Mwalimu Nyerere alimpatia pasi ya kusafiria ya Tanzania, aliyoitumia kwa miaka mitatu kwa ajili ya kwenda kusoma nje ya nchi, baada ya utawala wa Kikoloni wa Kenya kukataa kumpa pasi hiyo.
Kuhusu urafiki wake na Rais Magufuli, Mheshimiwa Odinga amesema urafiki huo ulianza tangu Rais Magufuli alipoteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi na yeye kuwa Waziri mwenye dhamana ya ujenzi wa Kenya, ambapo mara kadhaa walibadilishana uzoefu na kushirikiana katika mipango ya miradi ya ujenzi wa barabara, na kwa umuhimu huo ametoa wito kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendeleza ushirikiano na mshikamano ulioasisiwa na waasisi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania, Jalamogi Odinga wa Kenya na Milton Obote wa Uganda.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
03 April, 2016





Waziri Nape akutana na TAJATI


 WAZIRI NAPE AKUTANA NA VIONGOZI WA TAJATI

 4
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na viongozi wa TAJATI (hawapo pichani) alipowatembelea ofisini kwao kuona shughuli wanazozifanya leo Jijini Mbeya.

 5


 
Baadhi ya viongozi wa TAJATI wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) alipofika katika ofisi zao kuona shughuli wanazozifanya na kuwapa motisha wa kuandika habari za kiutafiti leo Jijini Mbeya.

 http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2016/04/210.jpg
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisoma kipeperushi alichopewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) ili kuweza kujua kazi wanazozifanya leo Jijini Mbeya alipowatembelea na kuwataka kuendela kuandika habari za kiutafiti ili kuboresha fani ya uandishi wa habari. Kushoto ni mwenyekiti wa TAJATI Bw. Ulimboka Mwakilili na kulia ni makamu mwenyekiti TAJATI Bw. Christopher Nyenyembe.


 6

 Makamu mwenyekiti TAJATI Bw. Christopher Nyenyembe (kushoto) akimuonyesha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye moja ya ofisi wanayoiandaa kwa ajili ya matumizi ya studio ya kurushia matangazo alipotembelea ofisi zao kuona shughuli wanazozifanya leo Jijini Mbeya.

 8

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akizungumza na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) alipowasili katika ofisi zao kuona kazi wanazozifanya leo Jijini Mbeya.


 7
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) baada ya kuzungumza nao leo Jijini Mbeya.
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo, Mbeya




Ijumaa, 1 Aprili 2016

KWA MAZOEZI HAYA, KAZI IPO KESHO EL CLASICO

Winga wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo (kushoto chini) akiwa mazoezini na nyota mwenzake wa timu hiyo, James Rodriguez kujiandaa na mchezo wa El Clasico wa La Liga dhidi ya mahasimu Barcelona kesho usiku Uwanja Camp Nou.

 

 (Left to right) Marcelo, Karim Benzema and Cristiano Ronaldo are put through their paces during training 



 

NDASA AFIKISHWA KIZIMBANI




MBUNGE WA SUMWE, RICHARD NDASA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUOMBA RUSHWA.
NA SHARIFA MARIRA, Dar

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 1/4/2016 imemfikisha Mahakamani Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa Mbunge wa Sumwe ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Mtaji na Uwekezaji kwa kosa la kushawishi na kuomba Rushwa ya Shilingi Milioni thelathini (30,000,000/-) kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15 (i)(a) na (2).

Richard Ndasa, Mbunge wa Sumve (CCM)
Mh Richard Ndassa akichangia hoja kwenye mkutano .

 

 Akiwa kama mjumbe wa Kamati ya Mtaji na Uwekezaji tarehe 13/3/2016 Mhe. Ndassa alimwomba rushwa ya shilingi Milioni 30 kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Felchesmi J. Mramba ili amsaidie kuwashawishi wajumbe wengine wa Kamati Mtaji na Uwekezaji kupitisha bila kipingamizi taarifa ya TANESCO kwa mwaka 2015/2016.

Mbunge huyo amefunguliwa kesi namba 118/2016 na alisomewa mashtaka hayo na Wakili wa TAKUKURU Dennis Lekayo akishirikiana na Emmanuel Jacob katika Mahakama ya Kisutu mbele ya Mhe. Hakimu Emirius Mchauro.

Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kupata mdhamini mmoja na kulipa shilingi milioni 10. Uchunguzi wa shauri hili bado unaendelea na kesi hii itatajwa tena tarehe 18/4/2016.

NAIBU WAZIRI AIPONGEZA "TWIGA STARS"





NA RAYMOND URIO, Dar
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura ameipongeza timu ya soka la Wanawake, “Twiga Stars” kwa kazi waliyoifanya kwenye mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa upande wa wanawake yatakayo fanyika nchini Cameroon.
Pongezi hizo zimeenda kwa kikosi  kizima kutokana na juhudi walizo onesha kwenye mechi dhidi ya Zimbabwe hapa nchini, ile na marudiano kuwa ni juhudi nzuri ya kutovunjika moyo kwenye kuipeperusha bendera ya nchini.










 
Naibu waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura,akiwapongeza wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake nchini “Twiga Stars” kwa kiwango walichokionyesha katika mechi ya marudiano na timu ya Zimbabwe alipokutana nao katika ukumbi wa Idara ya Habri MAELEZO,Dar es Salaam, jana.Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira wa Miguu Wanawake nchini (TWFA),Amina Karuna na Makamu mwenyekiti wa chama hicho,Rose Kisiwa. Picha na Raymond Urio


Akizungumza na waandishi wa Habari jana, jijini Dar es salaam Naibu Waziri Annastazia, alisema kuwa ni jambo zuri la kuipongeza timu yetu hasa ukiangalia ni mchango mkubwa waliionesha japo hatupo tena katika mashindano hayo ila kwa juhudi waliionesha ni muhimu sana kuwapongeza.
“ Wachezaji wetu wameonesha kazi nzuri katika mechi labda kwakuwa tatizo ni kutokuwa imara sana kwa muda nah ii inatokana na kutokuwa na Ligi zao.
“Nimepanga kuisadia timu hii kwa kutaka kuweza kufika mabli na hata kuibua vipaji vingine na kusimamia vyema soka kwa upandea wa wanawake,” alisema Annastia.
 Hata hivyo Annastazia alisema kuwa anawaomba wazazi wote nchini kutokuwa na imani za zamani kutowapa fursa watoto wa kike kukuza kitu anachotaka hasa kwa upande wa mchezo kama huu wa mpira wa miguu na kuamini ni wanaume pekee ndio wanaocheza,
Licha hivyo Meneja wa timu hiyo Furaha Francis, alisema kuwa uongozi wa timu unamuomba Naibu huyo kupitia serikali hii kusimamaia vyema swa la mpira wa miguu kwa upande wa wanawake kutokana na kusahaulika tangia nyuma.
“ Tulipoenda Zimbabwe tumeona, serikali ipo mstari wa mbele kuisimamaia timu yao na kujojali ni upande upi walionao, ila kwetu kitu kama hiko hakipo na si jambo jema inatakiwa na sisi tupate kuona thamani yetu iko wapi kwenye suala la soka” alisema Furaha.





















SHIRIKA LA POSTA KUZINDUA HUDUMA MPYA YA "POSTA MLANGONI" APRILL 5 MWAKA HUU



NA RAYMOND URIO, Dar
KATIKA Kuhakikisha kuwa Shirika la Posta Tanzania linashiriki na kuchangia kikamilifu jitihada za serikali ya awamu ya Tano za kuleta maendeleo ya haraka kwa mwanachi, shirika hili kuanzia jumanne litaanza kutoa huduma ya kupokea barua, nyaraka, taarifa na bidhaa mbalimbali kutoka ndani ya nje ya nchi na kuzifikisha nyumbani.


 
  Kaimu Poster Master Mkuu wa shirika la Posta Tanzania, Fortunatus Kapinga akizungumza jana na waandishi wa habari jana, jijini Dar es Salaam ( hawapo pichani), kwenye ukumbi za Ofisi hizo, kuhusiana na shirika hilo kufungua huduma ya "Posta Mlangoni" huduma hiyo itazinduliwa Aprill 5 mwaka huu, kushoto ni Meneja mkuu wa rasilimali za shirika la Posta Tanzania, James Sando.
 
Huduma hii inayojulikana kama “Posta Mlangoni” itaanza katika baadhi ya kata za hapa jijini Dar es Salaam, Arusha na Dodoma inaboresha ile iliyokuwapo tangu enzi za ukoloni ya masanduku yaliyoko Ofisini za Posta ambayo mtumiwa nanlazimika kufuata yeye mwenyewe barua, vifurushi, taarifa au bidhaa aluizotumiwa kupitia Ofisi za Posta.
Serikali kupitia Ofisi ya Raisi ( TAMISEMI ) tayari imeweka miundombinu hiyo katika kata 8 za jiji la Arusha, kata 8 za manispaa ya Dodoma na kata 32 kwa jiji la Dar es Salaam. Miundombinu hiyo ni mitaa kuwekewa nguzo za kuonesha jina la mtaaa, nyumba zilizopo kwenye mtaa huo kuwekewa nambari za kiposta.
Baada ya kuznzisha huduma hii jumanne ijayo hapa Dar es Salaam, Arusha na Dodoma ndani ya kipindi hiki cha mwaka 2015 na 2016, awamu ya pili itakayotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2016 na 2017 itahusu mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Tanga, Morogoro, Kagera, Mtwara, Lindi, Shinyanga, Pwani, Manyara, Simiyu na Geita pamoja na Tanznia visiwani( Unguja na Pemba).
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, kwenye ukumbi wa ofisi hizo, Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta nchini, Fortunatus Kapinga, alisema kuwa Huduma hii ni msukumo mpya wa ndani ya shirika wa kuhakikisha kuwa yanakuweko mabadiliko katika uendeshaji na utoaji wa huduma za mawasiliano ya Posta nchini ili kukabiliana na kasi ya teknolojia, kukidhi mahitaji ya soko, kuboresha maisha ya wananchi na kufanya Tanzania kuwa kinara wa hudumabora za mawasiliano.
“Kupitia huduma hii yamefanyika mabadiliko ya mifumo ya uendeshaji katika baadhi ya Ofisi ili kuhakikisha kuwa uchambuzi wa barua unafanyika kwa uhakika zaidi, anwanwi zitatambuliwa ili kuongeza kasi ya kusafirisha na kusambaza barua,
“Aidha kipindi hiki cha mpito ambapo hapo baadae ndani ya kipindi cha miaka mitatu shirika litasambaza huduma ya “Posta Mlangoni” nchi nzima,” alisema Kapinga.
Hata hivyo Kapinga alisema kuwa huduma hii imeanzishwa sasa kutokana na jitihada zax serikali kuweka miundombinu ya Anwani za Makazi na Postikodi kupitia wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini ( TCRA) na wadau wengine.
“ Miundombinu hii ni pamoja na barabara na Mtaa kuperwa majina yanayosomeka kwenye nguzo zilizosimikwa pamoja nanyumba kupewa majina yanasomeka  kwenye nguzo zilizo simikwa na nyumba zilizo pewa namba,” alisema Kapinga.


POLISI: UHAKIKI WA SILAHA KUENDELEA MIKOA YOTE,


BAADA ya wakazi ya jiji la Dar es Salaam kuanza usajili wa kuhakiki Silaha Jeshi la Polisi nchini limetoa miezi mitatu kwa mikoa mengine nchini  kwa wamiliki wote kufanya uhakiki wa silaha la sivyo sheria itachukua mkondo wake.

Akizungumza jijini hapa jana, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo, Nsato Malijani, alisema wananchi wamejitokeza kusajili na kuhakiki silaha zao ambapo rais Dk John Magufuli alikuwa wa kwanza kufanya hivyo na kwamba hali ya uhalifu wa makundi bado ipo, kuwataka wananchi wananchi kutoa taarifa endapo wakibainika makundi wanaojihusisha na uhalifu na yenye silaha. 

 

Kamishina wa oparesheni na mafunzo wa makao mkuu ya jeshi la polisi, Nsato Mssanzya akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani), kuhusiana na jeshi la polisi nchini kutoa linatoa muda wa miezi mitatau kwa ajili ya kukamilisha zoezi la kuhakiki silaha  kwa nchi nzima.

Kamishina Malijani alisema uamuzi wa kutoa muda huo katika mikoa iliyobaki ni kutokana na kwamba awali walitoa  muda mchache hali ambayo ilisababisha msongamano katika vituo vya polisi.

 Alisema hali hiyo imechangia kwa kiwango kikubwa mchakato huo kutofanyika kwa haraka jambo ambalo limekuwa kero na kuleta mkanganyiko kwa wamiliki pamoja na kupunguza hali ya usalama katika vituo vya polisi.

 "Hivyo ni imani yangu kwamba muda huo utatosha kwani utatoa nafasi kwa watu ambao hawajalipia ada ya umiliki wa silaha zao kulipia na kusajili pamoja na kuondoa msongamano wa watu katika vituo vya polisi waliojitokeza kwaajili ya kusajili silaha zao," alisema.

Alisema jeshi hilo halikuweka wazi idadi kamili ya sialaha ambazo hazikulipiwa na kiwango chake na kuweka wazi kuwa jambo hilo litaelezwa mara baada ya kukamilika kwa mchakato huo na kukusanya taarifa kutoka katika mikoa yote nchini.

Alisema hali ondoa msongamano wa watu katika vituo vya polisi waliojitokeza kwaajili ya kusajili silaha zao," alisema.

Akizungumzia uhalifu na ukamataji wa silaha,alisema hivi karibuni jeshi hilo limefanikiwa kukamata watu katika maeneo mbalimbali wanaojihusisha na uhalifu wa kimakundi ambao bado wanaendelea kufanyiwa uchunguzi.

"Watu hawa wamekamatwa Mafia, jeshi linaendelea kuwafanyia uchunguzi ili tuweze kupata taarifa mbalimbali na kuweza kuwatia

nguvuni wengine ili tutokomeze kabisa suala la uhalifu nchini," alisema

Alisema  wanaendelea kufanya msako katika maeneo yote nchini kuhakikisha vikundi hivyo vinadhibitiwa na kutoa rai kwa wananchi kuongeza ushirikiano ili uwakamata watu hao.

"Jeshi kama jeshi pekeake haliwezi likakakamata wahalifu wote bila kupata ushirikiano wa wananchi kwani wengi wao wapo miongoni mwao hivyo wananafasi kubwa ya kuwaona na kutoa taarifa ili waweze kukamatwa," alisema Malijani.