WANAODAI BUNGE KUONYESHWA LIVE WATAKIWA KUOMBA KWA UTULIVU

Aidha Katibu Mkuu wa Chama hicho, amesema kwamba amani iliyoko ni hazina kubwa ambayo nchi nyingine inatamani kuwa nayo.
Almas aliyasema hayo leo
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika
ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO).
“Leo hii tupo tunaopigania
kutaka kuona Bunge Live, lakini yote haya ni kwa kuwa Tanzania amani
tunayo, sidhani kama nchi kama Afghastan siku watakayoamua kuonyesha
Bunge Live kwa mwaka mzima, kwa saa 24 kama wataweza kukaa kuangalia
Bunge hilo, hivyo basi wale wanaotaka hayo, kwanza tudumishe amani
yetu,” alisema Almas.
Almas alieleza kuwa, amani ya
Tanzania ni zaidi ya dhahabu ambayo Tanzania inajivunia hivyo ni lazima
Watanzania kuitunza na kuithamini amani ambayo ipo kwa sasa na kuacha
kuchochea mambo ambayo yanaweza kuleta machafuko katika nchi na amani
ambayo leo haithaminiwi ikaja kukumbukwa siku moja.
Pia, alisema yeye ni mmojawapo
wa watu wanaopenda kuona Bunge Live lakini jambo hilo halishadadii kama
inavyofanywa na watu wengine kwani anajua kwa kufanya hivyo anaweza
kuhatarisha Amani ya Tanzania na hata hilo Bunge halitaweza kuliona tena
kutokana na kutokuwa na Amani ndani ya nchi.
Vilevile, amewataka waandishi wa habari kuandika yale yaliyo
mazuri ya nchi kuliko mabaya machache ili kuzidi kuitangaza Tanzania
vyema kimataifa, kwani sio uzalendo kuona mambo yote mabaya yanakuwa
ukurasa wa kwanza, bali kwanza yarekebishwe kwakuwa ni makosa yanayoweza
kurekebishwa. Kalamu za waandishi wa habari ni chachu ya amani na
maendeleo ya Taifa la Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni