MBUNGE wa jimbo la Iramba
wilayani Iramba mkoani Singida Bw Mwigulu Nchemba ameendelea kufanya
mikutano ya kuwashukuru wananchi wake kwa kumchagua kwa kishindo
katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwa kutekeleza ahadi mbali mbali
alizopata kuwaahidi wakati wa kampeni .
Mbunge Nchemba amekabidhi
bati hizo jana wakati wa mikutano yake ya kuwashukuru wananchi wake
wa jimbo la Iramba kwa kumchagua na kuanza utekelezaji wa ahadi zake.
Alisema kuwa lengo la
kuanza kukabidhi ahadi zake ni kuwafanya wananchi kuharakisha
ukamilishaji wa shughuli za kimaendeleo jimboni hasa katika nyanja ya
elimu na afya na kuwa bati hizo zitasaidia ujenzi wa vyumba vya
madarasa ,nyumba za walimu na Zahanati .
Kwani alisema ndoto yake ya
mbeleni ni kuona jimbo la Iramba na wilaya ya Iramba inaendelea
kuwa mbele katika ubora wa vyumba vya madarasa na wengine kufika
kujifunza Iramba
Hivyo alisema pamoja na
kuchangia bati kwa ajili ya ujenzi huo bado atajitolea kununua
tofari za kujengea ambazo kwa kila kijiji vijana watafyatua na yeye
atazinunua kwa bei ambayo wao watataka kama sehemu ya kutoa ajira
kwa vijana vijijini pia vifaa vyote vya viwandani kwa ajili ya
ujenzi wa miradi hiyo ni juu yake wananchi wanachotakiwa kufanya ni
kushiriki katika shughuli za kimaendeleo .
Pia aliwataka walimu na
watumishi wanaopangwa kufanya kazi katika wilaya ya Iramba
kujenga utamaduni wa kupenda kufanya kazi katika wilaya hiyo badala
ya kuripoti na kuondoka .
Nchemba ambae ni waziri wa
kilimo ,mifugo na uvuvi alisema kuwa vipaumbele vyake kwa wananchi
wake ni maji na umeme ambavyo tayari umeme umeanza kusambazwa
vijijini pia maji anaendelea jitihada japo alisema suala la
Miundombinu bado ni changamoto .
Wakati huo huo waziri Nchemba
ameshauri uongozi wa Halmashauri kuruhusu wanafunzi wanaopata
matatizo ya ugonjwa wakiwa shuleni kupatiwa matibabu ya bure katika
vituo vya afya ,Hospitali na zahanati katika jimbo hilo badala ya
kuwarudisha nyumbani .
Alisema kuna haja ya
Halmashauri kupitia vyanvzo vyake vya ndani kusaidia kuwalipia
matibabu wanafunzi hao na kuwa ofisi yake itasaidia kufidia pesa
hizo kwa kugharamia baadhi ya miradi ambayo inapaswa kutekelezwa na
Halmashauri kama ambavyo anafanya sasa kwa kujitolea kujenga vyumba vya
madarasa na Zahanati . |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni