Bodi ya Filamu yasitisha usambazaji wa “Imebuma”
Mhusika
Mkuu katika filamu ya “Imebuma” Bw. Eliasa Mkaly (Rashidi kisoda)
akimbembeleza muigizaji na mtayarishaji wa filamu hiyo Bi Sarah Nyika
(Asha Mauno) mara baada ya Bodi ya Filamu Tanzania kusitizaji usambazaji
wa filamu hiyo.
( Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO)
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisso akizungumza na
waigizaji wa filamu ya “Imebuma” (Hawapo Pichani) wakati wa ukaguzi wa
filamu hiyo kabla ya kupelekwa sokoni kulia ni 2 Afisa Utamaduni Bw.
Julius Tairo.
Afisa
Utamaduni Bw. Julius Tairo (wa Pili Kushoto) akitoa maelekezo kwa
waigizaji wa filamu ya “Imebuma” (Hawapo Pichani) wakati wa ukaguzi wa
filamu hiyo kabla ya kupelekwa sokoni kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi
ya Filamu Tanzania Joyce Fisso.
Mhusika
Mkuu katika filamu ya “Imebuma” Bw. Eliasa Mkaly (Rashidi kisoda)
akitoa maelezo kuhusu filamu hiyo wakati wa ukaguzi wa filamu ya
“Imebuma” kabla ya kupelekwa sokoni kulia ni waigizaji wa filamu hiyo.
( Picha zote na Shamimu Nyaki WHUSM)
………………………………………………………………………………………………………….
Na Shamimu Nyaki WHUSM
Bodi ya Filamu Tanzania imesitisha usambazaji wa filamu ya “Imebuma” mpaka pale maudhui yake yatakapofanyiwa marekebisho.
Akisitisha usambazaji wa filamu
hiyo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi Joyce Fisso amesema
mtengenezaji wa filamu hiyo hana kibali cha kutengenza filamu kutoka
Bodi ya Filamu na hajazingatia Sheria na kanuni za utengenezaji wa
filamu.
Bi Joyce Fisso amesema filamu
hiyo imesitishwa kwenda sokoni kutokana na kukiuka vifungu vya kanuni za
sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ya mwaka 2011 ambayo inakataza
kuonesha namna yoyote ya udhalilishaji wa kibinadamu katika filamu na
maigizo.
“Baada ya kuangalia kwa makini
filamu hii na kuona mapungufu ambayo yanakinzana na Kanuni za Sheria ya
filamu na Michezo ya kuigiza nimeamua kuisitisha usambazaji wake mpaka
pale wahusika watakaporekebisha maudhi yake” Alisema Bi Joyce.
Bi Joyce amefafanua kuwa filamu
hiyo imeonesha baadhi ya matukio ya udhalilishaji wa kibinadamu,
ushawishi wa matendo ya ngono na ushoga ambayo ni kinyume na madili ya
mtanzania.
Aidha kwa upande wake Afisa
Utamaduni kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Julius Tairo amewataka
waandaaji na waigizaji wa filamu nchini kufanya utafiti wa kutosha
kuhusu maudhui ya filamu kabla ya kutengeneza ili kuondokana na
utengenezaji wa filamu zisizofata Sheria na kanuni za utengenezaji wa
filamu Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni