TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINI

Katika kipindi cha mwezi mmoja
yaani mwezi wa Aprili 2016, idadi ya wagonjwa imekuwa ikipungua kwa
kiasi kikubwa lakini katika kipindi cha mwezi Mei, 2016 kasi ya
maambukizi imeanza tena kuongezeka.
. Takwimu za wiki iliyopita
kuanzia tarehe 2 hadi 8 Mei 2016 zinaonyesha kuwa, kasi ya ugonjwa wa
kipindupindu imeongezeka, ambapo idadi ya wagonjwa wapya walioripotiwa
ni 138 na vifo 2, ikilinganishwa na wagonjwa wapya 104 walioripotiwa
wiki iliyotangulia, sawa na ongezeko la 32%. Takwimu hizi ni zinaonesha
kuwa juhudi zaidi ziahitajika katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu.
Mikoa ambayo imeendelea kuongoza
kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wiki hii ni Kilimanjaro (58, kifo
1), Dar es Salaam (29) na Morogoro (22, kifo 1), Pwani (16) na Mara
(15). Halmashauri zilizoongoza kutoa wagonjwa wengi ni Same), Kinondoni,
Mvomero), Mbulu, Tarime vijijini, Ilala, Tarime mjini, Temeke, Morogoro
vijijini Kilolo Morogoro mjini, Bagamoyo, Kisarawe.
Katika wiki iliyopita, mikoa
ambayo haikuwa na wagonjwa wa kipindupindu ni Kigoma, Dodoma, Mwanza,
Geita, Singida, Shinyanga, Arusha, Tanga, Tabora, Lindi, Kagera, Rukwa,
Katavi, Mbeya, Simiyu na Mtwara.
Kama nilivyoeleza hapo juu,
takwimu zinaonyesha kuwa ugonjwa unaongezeka, hivyo tunahitaji kuchukua
tahadhari kubwa, hususan wakati wa huu wa mvua, ambapo kuna uwezekano
mkubwa wa maji ya mvua kusambaza vimelea vya ugonjwa huu. Tujitahidi
kuzuia maambukizi, na pia kuendelea kutoa taarifa za ugonjwa kila siku,
hata kama hakuna wagonjwa, na kusimamia kikamilifu hatua mbalimbali za
udhibiti wa mlipuko huo.
Wizara inaendelea kutoa rai kwa
wananchi wote kuzingatia kanuni za usafi binafsi na usafi wa mazingira.
Aidha wananchi wanashauriwa kutumia maji safi na salama na hii ni
pamoja na kuhakikisha maji ya kunywa yanachemshwa au kutibiwa kwa dawa
kama maagizo ya wataalam yanavyoelekeza. Napenda pia kusisitiza kwa
wananchi wanaokaa kandokando ya Mto Pangani hususani mikoa ya Tanga na
Kilimanjaro, kuwa maji ya mto huo si salama, kwa kuwa yamechafuliwa na
vimelea vya kipindupindu. Ni muhimu sana kuyachemsha au kuyatibu kwa
dawa maji hayo kabla ya kuyatumia nyumbani. Napenda kusisitiza tena
kwamba ni marufuku kwa watu kutitirisha maji taka ovyo,
hasa katika kipindi hiki cha mvua na mamlaka husika zinatakiwa kuchukua
hatua za kisheria kwa wale wote watakaokiuka agizo hili. Aidha
tunawasihi viongozi mbalimbali wa ngazi zote; za vitongoji, vijiji, kata
na tarafa kusimamia kikamilifu suala hili, hususan wakati huu wa mvua
za masika
Tunaendelea kuisihi jamii
kuungana na Halmashauri, Mikoa pamoja na Wizara katika juhudi za
kupambana na kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu kwa kuzingatia
yafuatayo:
- Kujenga na kutumia vyoo bora katika maeneo tunamoishi ili kupunguza hatari ya kuenea kwa ugonjwa huu.
- Kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni kabla ya kula, baada ya kutumia choo na baada ya kumsafisha motto aliyejisaidia.
- Mamlaka za maji zilizopo nchini zihakikishe upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.
- Kuzingatia ushauri na elimu sahihi kuhusu ugonjwa wa kipindupindu, ili jamii iondokane na imani potofu kuhusu kipindupindu. Viongozi wa dini, watu mashuhuri na waganga wa tiba mbadala wasaidie kuhamasisha jamii zao kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu,
- .
- Kufikisha wagonjwa wa Kipindupindu mapema katika vituo vya kutolea huduma ili wawahi kupata matibabu.
- Kuzingatia matumizi sahihi ya ORS kwa wagonjwa walioanza kuonesha dalili ili kupunguza athari za ugonjwa.
- Watumishi wa afya kutoa takwimu sahihi na kamili za ugonjwa kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na Wizara.
Wizara inawapongeza na
kuwashukuru wadau wote kwa jitihada za dhati zinazoendelea kutekelezwa
na katika kusimamia kikamilifu miongozo inayotolewa na Wizara ili
kuutokomeza ugonjwa huu, wakiwemo wataalamu wa sekta mbalimbali,
Mashirika ya Kimataifa, Watumishi, Mikoa na Halmashauri pamoja na
waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla.
Serikali kupitia Wizara yangu
inaendelea na utaratibu wa kutoa taarifa ya mwenendo wa mlipuko wa
ugonjwa wa Kipindupindu nchini kila wiki kama tulivyoahidi. Takwimu za
ugonjwa huu zinaonyesha kuwa hadi kufikia tarehe 08 Mei 2016, kulikuwa
na jumla ya wagonjwa 21,262 ambao wametolewa taarifa ya kuwa na ugonjwa
huu, na kati ya hao, watu 333 wamepoteza maisha.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni