BALOZI WA KUWAIT NCHINI TANZANIA AZUNGUMZA NA WAZIRI WA AFYA KUHUSU MRADI WA MATENGENEZO YA HOSPITALI KUU YA MNAZIMMOJA.
Waziri
wa Afya Mahamoud Thabit Kombo akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini
Tanzaania Jasem Al Najim alipomtembelea Ofisini kwake kumuelezea juu ya
Mradi wa kuifanyia matengenezo makubwa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja,
Mjini Zanzibar.
Waziri
wa Afya Mahamoud Thabit Kombo akiwa na mgeni wake Balozi wa Kuwait
nchini Tanzania akimtembelea Hospitali Kuu ya Mnazimmoja ambayo
itafanyiwa matengenezo makubwa na Serikali ya nchi hiyo.
Waziri
wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania
wakitembelea wagonjwa waliolazwa katika wodi ya wanaume waliopata ajali
katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.

……………………………………………………………………………………………………….
NA RAMADHANI ALI-MAELEZO ZANZIBAR
Serikali ya Kuwait itayafanyia
matengenezo makubwa majengo yote makongwe ya Hospitali Kuu ya
Mnazimmoja, mradi utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 84 za
Tanzania.
Akizungumza na Waziri wa Afya
Mahmoud Thabit Kombo Ofisini kwake Mnazimmoja, Balozi wa Kuwait nchini
Tanzania Jasim Al-Najim alisema Serikali ya nchi yake tayari imekubali
kutekeleza mradi huo haraka iwezekanavyo.
Alisema timu ya wataalamu kutoka
Kuwait inatarajiwa kuwasili Zanzibar mwezi Ogasti kwa ajili ya kufanya
uchunguzi yakinifu na kazi za matengenezo ya Hospitali zitaanza mara
tu baada ya wataalamu hao kumaliza kazi hiyo.
Aliongeza kuwa kufanikiwa kwa
mradi huo mkubwa utafungua milango kwa Serikali ya Kuwait kupitia
Mashirika ya misaada ya nchi hiyo kusaidia miradi mengine midogo midogo
na vifaa kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya Afya na sekta nyengine za
kiuchumi na kijamii.
Balozi Al-Nagim alisema hatua
hiyo ni kuonyesha umoja, ushirikiano na mapenzi ya dhati yaliopo kati
ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Kuwait.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit
Kombo aliishukuru Serikali ya Kuwait kwa kukubali kutekeleza mradi huo
mkubwa ambao utawasaidia wananchi wote wa Zanzibar.
Aidha alizishukuru Wizara za
Fedha za Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mpinduzi ya
Zanzibar, ambazo zilikubali kutekelezwa kwa mradi huo ndani ya Wizara ya
Afya.
Balozi Al-Najim alipata nafasi ya
kutembelea baadhi ya wodi za kulaza wagonjwa na sehemu ya kuhifadhia
maiti ya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja, ambapo kutokana na kuguswa na
sehemu hiyo, alisema itakuwa ya kwanza kufanyiwa matengenezo mradi huo
utakapoanza.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni