SERIKALI KUENDELEA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA KEMIKALI
Mkuu
wa Kitengo Cha Utafiti na Ubora wa Mifumo Bw. Benny Mallya kutoka Ofisi
ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu utekelezaji wa
sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali sura 182 ili kuzuia athari
zinazoweza kujitokeza kwa wasafirishaji na watumiaji wa kemikali hapa
nchini. Kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Frank
Mvungi na kulia ni Afisa Habari wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw.
Sylvester Omari.
Mkuu
wa Kitengo Cha Utafiti na Ubora wa Mifumo Bw. Benny Mallya kutoka Ofisi
ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali akizungumza na
waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu hatua
zinazochukuliwa na Serikali ikiwemo kutoa mafunzo kwa wasimamizi 61 wa
shughuli za usafirishaji wa kemikali na madereva 123 hapa nchini. Kulia
ni Afisa Habari wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Bw. Sylvester Omari.
…………………………………………………………………………………………………….
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali itatoa mafunzo kwa
wasimamizi 61 wa shughuli za Kemikali na madereva 123 wanaosafirisha
Kemikali mbalimbali ili kuzuia athari zinazotokana na matumizi
yasiyozingatia sheria na kanuni za kemikali.
Akizungumza leo jijini Dar es
salaam wakati wa mkutano na vyombo vya habari Mkuu wa Kitengo Cha
Utafiti na ubora wa Mifumo Bw. Benny Mallya kutoka Ofisi ya Wakala wa
Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali amesema mafunzo hayo ni sehemu ya
utekelezaji wa sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani
na majumbani sura 182.
Alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2015 matukio ya kemikali yalisababisha vifo 14.
“Jumla ya matukio 11 ya ajali za
Kemikali yalitolewa taarifa katika kipindi cha mwaka jana pekee na
kusababisha uharibifu mkubwa wa mali ikiwemo kuungua moto magari na tani
250 za kemikali”.alisisitiza Mallya.
Akifafanua kuhusu matukio hayo
Mallya amesema kuwa ajali hizo zilisababishwa na kukosekana kwa uelewa
juu ya athari zinazoweza kusababishwa na kemikali hizo miongoni mwa
wasafirishaji na watumiaji.
Kama sehemu ya utekelezaji wa
sheria hii,Serikali inatarajia kuendelea kufanya mafunzo ya wadau
kuhusiana na kemikali zenye kusababisha mlipuko.
Mafunzo hayo yatatolewa kwa wakuu
wa polisi wa Usalama barabarani nchi nzima yanalenga kuongeza uelewa
kwa wadau wanaohusika katik a kutumia na kusafirisha kemikali ili kuzuia
athari zinazoweza kujitokeza.
Katika kukabiliana na madhara
yatokanayo na matumizi yasiliyo salama,ajali na matukio ya
kemikali,Serikali iliamua kutunga sheria ya usimamizi na udhibiti wa
kemikali za viwandani na majumbani sura 182 (The Industrial and Consumer
Chemicals Management and Control) Act Capt 182).
Lengo kuu la sheria hii ni
kuhakikisha kuwa kemikali zinatumika katika hali iliyo salama bila
kuleta athari kwa watu na mazingira.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni