Jumatatu, 9 Mei 2016

NAIBU WAZIRI AGELINA MABULA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA ARDHI

By Newsroom May 9, 2016 
A1 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukubi wa mikutano wa Shirika la Nyumba Upanga jijini Dar es salaam, Naibu Waziri Angelina Mabula amewaasa wafanyakazi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa nidhamu na uadilifu kwani kumekuwa na malalamiko kutoka katika halmashauri mbalimbali nchini wananchi wakilalamikia wafanayakai wa idara za Ardhi jambo ambalo ziyo zuri, Jirekebisheni mfanye kazi kwa maslahi ya watanzania ili wananchi waweze kutatuliwa shida zao katika masuala ya migogoro ya ardhi bila matatizo wala vikwazo.
A2 
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Bw. Yamungu Kayandabila akimkaribisha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula ili kufungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo katika mkutano uliofanyika mwishoni mwa wiki Upanga jijini Dar es salaam. A3 
Baadhi ya wafanyakazi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula  wakati alipokuwa akifungua rasmi mkutano huo.
A4 A5 A6 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mh. Angelina Mabula akiwa ameketi meza kuu pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bw. Yamungu Kayandabila  watatu kutoka kushoto pamoja  viongozi wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Ardhi.
A7

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni