Jumamosi, 17 Desemba 2016

ZIARA YA MAJALIWA HALMASHAURI YA ARUSHA

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya wanawake wa kimasai baada ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016. kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
piga
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipiga ngoma ya msanja iliyokuwa ikichezwa na wnanwake wa Arusha baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ziduka
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
twisha
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimtwisha ndoo ya maji bibi Agness Silima ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Onderet wilayani Arusha Desemba 17, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pikaaaa
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa eneo la Kwamrombo wilayani Arusha ambao   walijipanga kwa wingi barabarani na kumshawishi kusimama  ili kuzungumza nao. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Arusha  Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pikaaa-2222
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa kizungumza na wananchi wa kijiji cha Ormapinu  wilayani Arusha ambao wlijipanga  kwa wingi barabarani na kumshawishi kusismama ili kuwasikiliza. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ZIARA YA MAJALIWA HALMASHAURI YA ARUSHA

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya wanawake wa kimasai baada ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016. kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
piga
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipiga ngoma ya msanja iliyokuwa ikichezwa na wnanwake wa Arusha baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ziduka
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
twisha
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimtwisha ndoo ya maji bibi Agness Silima ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Onderet wilayani Arusha Desemba 17, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pikaaaa
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa eneo la Kwamrombo wilayani Arusha ambao   walijipanga kwa wingi barabarani na kumshawishi kusimama  ili kuzungumza nao. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Arusha  Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
pikaaa-2222
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa kizungumza na wananchi wa kijiji cha Ormapinu  wilayani Arusha ambao wlijipanga  kwa wingi barabarani na kumshawishi kusismama ili kuwasikiliza. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA USA RIVER

rive
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ngaraseru- Usa River wilayani Arumeru Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
rix
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya kikundi cha sana cha Chuo Kikuu cha Makumira cha Arusha baada ya kuwasili kwenye  uwanja wa Ngaraseru – Usa River wilayani Arumeru kuhutubia mkutano wa hadhara Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
rev
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  kisalimiana na viongozi wa dini baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ngaraseru- Usa River wilayani Arumeru  kuhutubia mkutano wa hadhara.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA KAMPENI YA KITAIFA YA KUDHIBITI MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza  kwenye viwanja vya Leaders Club.
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza ambapo aliwaambia wananchi walishiriki kwenye tukio hilo kuwa siri kubwa ya mafanikio yake ya kuonekana yupo imara ni mazoezi hivyo aliwataka wananchi wajenge tabia ya kushiriki na kufanya mazoezi kwani kutawaepusha na maradhi mengi .
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim akihutubia kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzindua rasmi Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza matembezi ikiwa sehemu ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi akiongozana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim kabla ya kufungua Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza  kwenye viwanja vya Leaders Club viongozi
wengine walioshiriki matembezi hayo ni pamoja na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalah, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja  na viongozi mbali mbali mara baada ya kufungua wa Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza  kwenye viwanja vya Leaders Club.
                      ………………………………………………………………………………………. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa muda wa miezi mitatu kwa Halmashauri zote nchini kurudisha serikalini haraka maeneo ya michezo yaliyovamiwa na watu kwa ajili ya kufanya shughuli zao binafsi.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo baada ya kushiriki matembezi na kuzindua wa kampeni ya Kitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwenye viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais ameonya kuwa kama watendaji wa mikoa na halmashauri watashindwa kurudisha maeneo hayo basi watenge haraka maeneo mengine kwa ajili ya wananchi kufanya mazoezi kama hatua ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Katika kuunga mkono utaratibu wa kufanya mazoezi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi wa mikoa na wilaya zote kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi angalau kwa mwezi mara Moja.
“Nitamke kuwa kila Jumamosi ya pili ya mwezi itakuwa siku ya mazoezi kwa afya kwa sababu mazoezi ni afya na nawaasa wananchi kufanya mazoezi na kuanzisha na kujiunga na vikundi vya mazoezi na serikali itatimiza wajibu wake wa kuweka mazingira mazuri ya kufanyia mazoezi kote nchini”
Makamu wa Rais pia ameagiza watendaji wa Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia kurudisha
mchakamchaka mashuleni kulingana na maeneo yalivyo.
Amesema mchakamchaka utasaidia kuimarisha afya za wanafunzi na kukabiliana na magonjwa
mbalimbali.
“Natoa rai utaratibu wa mchakamchaka katika shule zetu urudishwe mara Moja katika Muda
ambao utaonekana ni mwafaka kwa shule husika”.
Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais ameiagiza Wizara ya Afya kukamilisha haraka mchakato wa kuunda kamati
ya kushughulikia magonjwa yasiyo ya kuambukiza itakayojumuisha wadau kutoka wizara mbalimbali nchini.
Amesisitiza kuwa mchakato huo ni lazima ukamilike tarehe 1 machi mwaka 2017.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza yamekuwa yanaongezeka sana duniani kote hasa kwenye nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania ambapo magonjwa hayo mpaka sasa yanachangia asilimia 27 ya vifo Duniani
Amesema utafiti uliofanyika mwaka 2012 uliohusisha wilaya 53 hapa nchini umeonyesha viashiria hatarishi vya magonjwa hayo ambapo asilimia 26 ya wananchi ni wanene kupita kiasi,asilimia 26 wana lehemu nyingi mwilini na asilimia 25.9 wanashinikizo kubwa la damu.
Utafiti huo pia ulionyesha kuwa asilimia 15.9 ya wananchi wanavuta sigara na asilimia
97.2 ya wananchi wanakula mboga mboga na matunda chini ya mara tano kwa siku.
Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema watanzania wanaweza kukabiliana na magonjwa hayo kwa kufanya mazoezi ya viungo angalau mara tatu kwa wiki kwa muda wa nusu saa, kuzingatia ulaji wa vyakula unaofaa,kupunguza matumizi ya pombe kupita kiasi na kujiepusha na matumizi ya tumbaku.
Kwaupande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi katika nasaha
zake amewahimiza Watanzania kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya zao.
Amesema kama watanzania watafanya mazoezi wataepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza
ikiwemo ugonjwa wa moyo,kisukari,uti wa mgongo na mifumo ya neva na figo.

MAYODA yaomba Serikali kushirikiana na Sekta binafsi

MWENYEKITI Mtendaji wa Mayoda Economic Development Group, Agustino Matefu, ameishauri serikali kushirikiana na sekta binafsi ili kukuza viwanda vidogovidogo na kuongeza thamani ya bidhaa nch
 aini
Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Mayoda Economic Development Group, Augustino Matefu (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu kutoa wito kwa serikali kuunga mkono sekta binafsi ili kukuza uchumi kupitia Viwanda vidogovidogo kupitia wajisiriamali mbalimbali. Katikati ni Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Iddi Majuto na Mratibu wa taasisi hiyo Cleopas John. (Picha na Raymond Urio)

Matefua alitoa ushauri huo jijini Dar es Salaam jana, alipozunguzma na waandishi wa habari juu ya fursa mbalimbali zilizopo nchni.
“Ukiimarisha viowanda vidogovidogo ndio mwanzo wa kukua kwa uchuni nchini, hivyo kuwaunganisha watu katika vikundi na kurasimisha shughuli zao”. Alisema Agustino.
Alisema Mayoda imekuwa ikiwakutanisha wajasiriamali mbalimbali wakiwemo wavuvi, wakulima, wafugaji, mama ntilie na bodaboda na kuwafundisha fursa zilizopo nchini ikiwemo kuwasaidia kupata mikopo mbalimbali.

Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Mayoda Economic Development Group, Augustino Matefu (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu kutoa wito kwa serikali kuunga mkono sekta binafsi ili kukuza uchumi kupitia Viwanda vidogovidogo kupitia wajisiriamali mbalimbali. Katikati ni Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Iddi Majuto na Mratibu wa taasisi hiyo Cleopas John. (Picha na Raymond Urio)

“Mayoda inatoa elimu na kuunda vikundi vyenye wataalamu  mbalimbali ili kuwasajili na kupata uwezashaji ambao huvisaidia baadae kuwa viwanda vidogo vidogo, “ alisema.



Jumatatu, 5 Desemba 2016

ZIARA YA MCHENGERWA ILIVYOBAINI MADUDU YA UUZWAJI ARDHI RUFIJI

 Mbunge wa Jimbo la Rufiji ,Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Chumbi A,B na C vilivyopo katika jimbo lake mwishoni mwa wiki.

ZIARA ya Mbunge wa Rufiji,Mohamed Mchengerwa,(CCM) imebaini uuzwaji wa ardhi iliyokuwa imetengwa kwa ajili ya kiwanda cha sukari katika kijiji cha Chumbi ambayo imeuzwa kwa hekari moja shilingi 10,000.

Baada ya Mbunge huyo kufika katika mkutano wa hadhara wa kushukuru wananchi na kusikiliza kero zao juzi katika kijiji cha Chumbi alikutana na kilio cha eneo lenye ekari 2400 kuuzwa kwa shilingi milioni 24 pekee.

Wananchi wa eneo hilo walimtaja Diwani wa Kata ya Chumbi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Chumbi C,Salum Mtimbuko (CCM) kuwa ndiye aliyeuza eneo hilo kwa muwekezaji ambaye anamjua mwenyewe na alipewa Baraka zote na Mkuu wa Wilaya hiyo Juma Njwayo.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapo,Mussa Mngeresa,ndiye aliyeeleza jambo hilo huku akishangiliwa na wananchi akimtaka mbunge huyo kumpeleka Mkuu wa Mkoa huo,Mhandisi Evarist Ndikilo,ili atatue kero hiyo kwani Njwayo ameshindwa.
‘’Uuzwaji huu ulifanywa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Chumbi C ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Chumbi ,Salum Mtimbuko (CCM)  na alipata Baraka kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji,Juma Njwayo,ambaye wananchi walimueleza suala hilo kabla lakini hakulifanyia kazi na kuwataka waache majungu’’alisema

Alisema viongozi hao wamewaudhi wananchi kwa kuuza ardhi kwa muwekezaji ambaye wanamjua wenyewe na kwamba ukifanyika uchaguzi wakati wowote kabla masuala hayo hayajataftiwa ufumbuzi CCM itapoteza nafasi hivyo kumuomba Mbunge huyo kufanya jitihada za kuwaleta viongozi wa mkoa,Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Akizungumzia suala hilo Mchengerwa alilaani kitendo cha viongozi hao kutaka kukwamisha maendeleo ya viwanda jimboni hapo kwani alishazungumza na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage,kuhusu ujenzi wa kiwanda cha sukari katika eneo hilo ambalo kwa sasa wananchi wamesema halipo.

‘’Jamani huku ni kurudishana nyuma na kutotambua juhudi za serikali na tunaowatetea haiwezekani viongozi wahusike kuuza ardhi ya kiwanda,wananchi tusikubali,sheria inaruhusu kuongea upya  na muwekezaji huyo ili atuachie ardhi yetu au aongeze fedha tukatafute eneo linguine,kuuza shilingi 10,000 ekari moja ni aibu’’
Akijibu tuhuma hizo diwani huyo alisema’’Nyie mnanionea wivu,wengine nimewasadia sana kuwalisha na familia zenu alafu mnanisema hapa,au kwasababu mnaniona naishi vizuri na wake zangu wawili na nina nyumba na magari? Pumbavu’’

Hata hivyo majibu ya diwani hiyo yalizua tafrani kwa wananchi kumzoea na kumtaka Mchengerwa arudi kwa mara nyingine na Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo,Ili aweze kutatua kero zilizopo kwani viongozi wanauza maeneo kiholela na wanaposhitaki wa Mkuu wa Wilaya anakuwa upande wa wauzaji ardhi.

Mchengerwa aliwaleza wananchi hao kwamba ameshawasiliana na Mhandisi Ndikilo ,kuahidi kufanya ziara katika maeneo hayo Desemba 5 mwaka huu .
 

Ijumaa, 2 Desemba 2016

Miaka 55 ya Uhuru Jimbo la Igalula linajivunia Mafanikio Makubwa


mfutakamba1
Na.  Immaculate Makilika – MAELEZO
WANANCHI wa Jimbo la Igulula wilayani Uyui Mkoani Tabora wamepongeza hatua na jitihada zilizofikiwa na Serikali katika kuboresha miundombinu ya huduma za maendeleo ya jamii katika kipindi cha miaka 55 ya uhuru wa Tanzania Bara.
Wanazitaja huduma hizo ni pamoja na maji, afya, nishati, na elimu ambazo kwa kipindi kirefu zilikuwa zikikwamisha maendeleo ya wananchi, na kukamilika kwake kunahitimisha ndoto za siku nyingi za kupatikana kwa  huduma muhimu  jimboni  humo.
Wakitolea mfano wanasema mwaka 2015 jimbo hilo  limepata  nishati ya umeme kupitia gridi ya Taifa kwa asilimia 70 na hivyo kufanya kata za Goeko, Ngololo, Kigwa na Igalula kupata nishati hiyo adhimu sambamba na  kufikisha umeme wa mwanga wa jua katika kata za Tara, Loya, na Lutende.
Mbunge wa jimbo la Igalula Athumani Mfutakamba akizungumza na mwandishi wa habari hii, anaeleza kinagaubaga neema zilizopatikana ndani ya miaka 55 ya Uhuru katika jimbo hilo na kukiri wazi zinamfanya awe na shauku ya kuhadithia kila mara.
Dkt. Mfutakamba anasema jitihada hizo za Serikali pamoja na wadau wengine za kufikisha umeme katika jimbo la Igalula imekua nyenzo muhimu  kwa uchumi na ustawi wa maendeleo ya jimbo hilo.
“Umeme huu umekua ukitumika si tu kuwashia taa ama kumulika majumbani na mitaani ila hutumika pia  hospitalini, shuleni na katika shughuli mbalimbali zinazotumia nishati hiyo” anasema Dkt Mfutakamba.
Kwa mujibu wa Dkt. Mfutakamba anasema jimbo hilo limepata mafanikio makubwa katika sekta ya maji kwa kujenga visima virefu viwili vilivyoweza kutatua matatizo ya maji katika jimbo hilo.
Dkt. Mfutakamaba alisema jimbo hilo pia limefanikiwa kukamilisha ujenzi wa zahanati za Imalaseko, Goeko, Ngololo, Igalula na Loya pamoja na kupata vitanda ambavyo vinatumika kusaidia wanawake wanaojifungua.
Kuhusu sekta ya elimu, Mbunge Mfutakamba alisema kwa miaka mingi jimbo hilo halikuwa na shule ya sekondari, ambapo hadi sasa jimbo limeweza kuwa na shule ya sekondari Goeko.
Sambamba na hayo, Mbunge huyo aliipongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ikiwemo za kusimamia kikamilifu rasilimali fedha na watu.
“Ni lazima tuunge mkono jitihada hizo kwa kulipa kodi ili fedha zitakazopatikana zisaidie katika shughuli mbalimbali za kutuletea maendeleo, badala ya kutegemea wafadhili pekee” alisema Mbunge huyo