Ijumaa, 27 Novemba 2015

MAHAKAMA KUU TANZANIA KUFUNGUA NJIA KWA WAANDISHI WA HABARI



JAJI  kiongozi wa Mahakama kuu ya Tanzania Shaaban Lila amesema kuwa majaji wa Tanzania wanabusara katika kufanya maamuzi yao na ndio maana hata vyombo vya habari nchini hata vinapowachafua hawaangaiki kufikisha kwenye vyombo vya dola.

ALIYEKUWA MGURUGENZI MSAIDIZI WA SHUGHULI ZA BUNGE BI.HELLEN MBEBA AFARIKI

Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah, anasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wa Bunge, Bi. Hellen Stephen Mbeba (36), aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi-Shughuli za Bunge, kilichotokea ghafla leo Ijumaa tarehe 27/11/2015 wakati akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu..

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI,AWAVUA GAMBA BAADHI YA MAAFISA TRA



Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi maofisa watano na watumishi watatu wa mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)kutokana na upotevu wa makontena
349 yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni 80.

Alhamisi, 8 Oktoba 2015

MAKAMU MWENYEKITI NCCR-MAGEUZI ASEMA YEYE BADO KIONGOZI




MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi(Bara) Leticiaa Mosore amesema mpaka sasa bado anaendelea kushikilia wadhifa huo kwani kikao kilichoitishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa James Mbatia hakikuwa na uhalali wa kikatiba.

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA TAKWIMU DAR ES SALAAM LEO.


 

 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto), akihutubia wakati akifungua mkutano wa wadau wa takwimu Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Profesa Adolph Mkenda na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Albina Chuwa. Mkutano huo uliandaliwa na NBS.   

MAADHIMISHO YA SIKU YA MACHO DUNIANI KUFANYIKA LEO.

IMEELEZWA kuwa takribani watu 945,000 wanasumbuliwa na matatizo  ya kuona kwa viwango mbalimbali hapa nchini idadi yao ikiwa ni mara tatu ya watu wasioona kabisa ambao ni takribani watu 315,000.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii idadi ya watoto wenye matatizo ya kuona duniani ni milioni 19 huku wazee wakiongoza kwa asilimia 82 pia nchi zinazoendelea zinaongoza kwa idadi kubwa ya watu wenye matatizo hayo kwa asilimia 90.

Taarifa hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Dkt.Donan Mmbando,Katibu Mkuu wa wizara hiyo,ikiwa nisehemu ya kuadhimisha siku ya afya ya macho duniani yenye kauli mbiu ya "Afya bora ya macho kwa wote"yenye lengo la kuhamasisha wadau kushirikana katika kuimarisha  upatikanaji wa huduma za macho katika ngazi zote za utoaji huduna za afya.

Imebainika  kuwa kuwa asilimia 80 ya matatizo yote ya kutokuona yanayoikabili dunia yanachangiwa na sababu zinazoweza kuzuilika.

"Inakadiriwa kuwa takribani watu milioni 285 duniani wana matatizo ya kuona,kati ya hao wenye upofu ni milioni 39 na 246 wana uoni hafifu,"inaeleza taarifa hiyo.

Aidha kutokana na taarifa hiyo sababu zinazosababisha upofu unaoweza kuzuilika hapa nchini na dunia kwa ujumla ni pamoja na mtoto wa jicho,makovu kwenye kioo cha jicho,trakoma,upofu wa utotoni unaotokana unaookana na upungufu wa vitamini A.

Pia maambukizi ya surua,maambukizi ya kisonono kutoka kwa mam kwenda kwa mtoto,upungufu wa upeo wa macho kuona,matatizo ya retina pamoja na ugonjwa wa kisukari na umri mkubwa.

Hata hivyo Wizara ya Afya na ustawi wa jamii inatoa wito kwa Watanzania kupima afya ya macho angalau mara moja kwa mwaka pamoja na wadu na mashirika ya kiserikali na watu binafsi kuwekeza katika rasilimali katika huduma ya macho kwa maendeleo ya nchi.

Jumatano, 7 Oktoba 2015

MAAFISA 27 WA JESHI LA MAGEREZA KANDA YA KASKAZINI WATUNUKIWA NISHANI‏MAAFISA 27 WA JESHI LA MAGEREZA KANDA YA KASKAZINI WATUNUKIWA NISHANI‏





 CGP, Agustino Nanyaro, Mkuu wa Magereza Tanzania akiongea na waandishi wa habari
 CGP, Agustino Nanyaro, akikagua gwaride maalimu
 Heshima na Utii
 DCP Chiza Ruvugo, Naibu Mkuu wa Magereza Tanzania akivishwa nishani.
Mambo yanaendelea