IMEELEZWA kuwa takribani watu 945,000 wanasumbuliwa na matatizo ya kuona kwa viwango mbalimbali hapa nchini idadi yao ikiwa ni mara tatu ya watu wasioona kabisa ambao ni takribani watu 315,000.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii idadi ya watoto wenye matatizo ya kuona duniani ni milioni 19 huku wazee wakiongoza kwa asilimia 82 pia nchi zinazoendelea zinaongoza kwa idadi kubwa ya watu wenye matatizo hayo kwa asilimia 90.
Taarifa hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Dkt.Donan Mmbando,Katibu Mkuu wa wizara hiyo,ikiwa nisehemu ya kuadhimisha siku ya afya ya macho duniani yenye kauli mbiu ya "Afya bora ya macho kwa wote"yenye lengo la kuhamasisha wadau kushirikana katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za macho katika ngazi zote za utoaji huduna za afya.
Imebainika kuwa kuwa asilimia 80 ya matatizo yote ya kutokuona yanayoikabili dunia yanachangiwa na sababu zinazoweza kuzuilika.
"Inakadiriwa kuwa takribani watu milioni 285 duniani wana matatizo ya kuona,kati ya hao wenye upofu ni milioni 39 na 246 wana uoni hafifu,"inaeleza taarifa hiyo.
Aidha kutokana na taarifa hiyo sababu zinazosababisha upofu unaoweza kuzuilika hapa nchini na dunia kwa ujumla ni pamoja na mtoto wa jicho,makovu kwenye kioo cha jicho,trakoma,upofu wa utotoni unaotokana unaookana na upungufu wa vitamini A.
Pia maambukizi ya surua,maambukizi ya kisonono kutoka kwa mam kwenda kwa mtoto,upungufu wa upeo wa macho kuona,matatizo ya retina pamoja na ugonjwa wa kisukari na umri mkubwa.
Hata hivyo Wizara ya Afya na ustawi wa jamii inatoa wito kwa Watanzania kupima afya ya macho angalau mara moja kwa mwaka pamoja na wadu na mashirika ya kiserikali na watu binafsi kuwekeza katika rasilimali katika huduma ya macho kwa maendeleo ya nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni