NA RAYMOND URIO, Dar
WAKALA wa Usambazaji wa Nishati ya Umeme Vijijini (REA),
wametoa tamko kuwa kusitisha kwa Bodi ya Shirika la Changamoto (MCC), kutoa
misaada nchini haitaathiri mradi wa usambazaji umeme vijijini.
Hayo yamesemwa jana jijini Dar es salaam na Mkurugenzi
Mtendaji wa Wakala wa Usambazaji wa Nishati ya Umeme vijijini Letungano Mbakahesya, wakati akitoa tathimini
ya maendeleo ya mradi huo ambao kwa mara ya kwanza ulinza kusambaza umeme
vijijini mwaka 2007.
Mwakahesya, alisema katika mradi huo serikali inachangia
fedha kwa kiasi cha asilimia 90 huku asilimia nyingine ikipatikana kutoka kwa makampuni
binafsi.
“MCC haijawahi kutupatia kiasi chochote cha fedha , hivyo ,
kustisha kutupatia msaada hakutaathiri jambo lolote, usambazaji utaendelea kama
ulivyo na huduma itakuwepo katika vijiji vyote tulivyokusudia kutoa huduma
hiyo” alisema Mwakahesya
Mkurugenzi mtendaji wa wakala wa Nishati ya
umeme vijijini. Lutengano Mwakahesya, akizungumza na waandishi wa habari jana,
jijini, Dar es Salaam kuhusiana na jinsi umeme huo ulivyosambazwa kwa maeneo ya
vijini. Kushoto Meneja wa wakala wa Nishati ya umeme vijijini Elineema Mkumbo.
Alisema lengo la mradi huo ni kusanbaza umeme katika vijiji
15,000 nchini hadi kufikia sasa wameshasambaza umeme katika vijiji 520 ambayo
sawa na asilimia 36 huku wakifikia idadi ya watumiaji 75,000 ikiwa matarajio
yao kufikia watumiaji 250,000.
Alisema kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mradi huo
walianza na Sh. Bilioni 10 na kufanikiwa kusambaza umeme katika Wilaya za
vijiji vitano ambavyo ni Kilolo, Mkinga, Kilindi, Uyuhi na Bahi.
“Baada ya kusambaza katika vijiji hivyo tuliona mafanikio,
serikali kwa mara ya kwanza ilitupatia Sh. bilioni 120 ambapo mchango mwingine
ulitoka shirika la usambazaji umeme Tanzania (Tanesco), na kusaidia fedha hizo
kusambaza mradi katika vijiji saba na maeneo mengie ya biashara ’’ alisema.
Mwakahesya, alisema utekelezaji wa awamu ya pili ulianza mwaka 2013 hadi 2016 walipatiwa Sh.
bilioni 881 ya usambazaji wa umeme huo
vijijini na kufikia asilimia 90 ya utekelezaji na kutegemea ifikapo mwezi Juni mwaka huu
utekelezaji utakuwa umekamilika katika vijiji vyote walivyovikusudia hapa
nchini.
Alisema baada ya mradi wa awamu ya pili kukamilika
imetengwa Sh. bilioni 584 kwa mwaka wa fedha 2016- 2017 kwajili ya awamu ya
tatu ambayo itaendelea kusambaza umeme katika vijiji vingine ambavyo
awajafikiwa na mladi huo kwa awamu nyingine zilizopita hapo awali.
Meneja wa Usambazaji wa umeme huo Elineema Mkumbo,
aliyataja mashirika binafsi ambayo yanawasaidia kusambaza umeme kutokana na
Tanesco kwa sasa awawezi kufika vijijini huko ambayo ni shirika la Lifti Vale
ambalo linaunganisha umeme kutoka Mufindi na kuusambaza katika vijiji 14 na
kiasi kinachobaki kukiunganisha katika gridi ya taifa.
“Tasisi nyingine tunazoshirikiana nazo ni Lumama ipo Wilaya
ya Ludewa inazalisha umeme na kusambaza katika vijiji 6, tasisi nyingine ipo
mkoani Ruvuma inaitwa Chipole inazalisha megawati 5 na kusambaza umeme Songea
na kusaidia matumizi ya mafuta ya disel kupungua, tasisi nyingine Ndoa ambayo
inasambaza umeme nusu megawaiti katika
kijiji cha Mbinga ’’.
Alisema wawekezaji wanaohitaji kuwekeza katika mradi huo
wanakaribisha na watanzania wategemee huduma bora ya umeme pindi mladi huo
utakapokamilika katika maeneo hayo ya
vijjini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni