Wachezaji wa Azam Fc wakishangilia ushindi . |
NA RAYMOND URIO
KLABU ya Azam FC imetinga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho FA kwa kuichapa Prisons kwa mabao 3-1.
Ulikuwa
ni upinzani mkali kati ya timu hizo mbili lakini Azam FC ndiyo
waliokuwa makini kuzitumia nafasi walizozipata kupitia mchezaji wao na beki wa timu hiyo Shomari Kapombe
aliyefunga mabao mawili na Hamis Mcha aliyefunga bao moja.
Jeremiah
Juma ndiye alifunga bao pekee la Prisons ambayo kila muda ulivyokuwa
ukisonga mbele ilionekana kupoteza kasi na umakini.
Azam FC inakuwa ni timu ya tatu kutinga nusu fainali ya Kombe la FA baada ya Mwadui FC na Yanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni