Alhamisi, 31 Machi 2016

EBOUE HATIANI KLABUNI SUNDERLAND



KLABU ya Sunderland imemfukuza beki wake Emmanuel Eboue baada ya 22  kufuatia taarifa za kufungiwa mwaka mmoja kwa kushindwa kumlipa wakala wake wa zamani.
Mapema asubuhi ya leo (jana), Shirikisho la Soka Duniani, FIFA imesema leo nyota huyo wa zamani wa Arsenal mwenye umri wa miaka 32 hataruhisiwa kujishughulisha na soka hadi atakapomlipa wakala wake Sebastien Boisseau, anayemdai kiasi cha Pauni Milioni 1.
Sunderland imechukua hatua za haraka kwa kumvunjia Mkataba mchezaji huyo  licha ya kwamba alikuwa hajaripoti kuanza kazi kwenye klabu hiyo baada ya kujiunga nayo kama mchezaji huru Machi 9.
  Eboue akiwa ameshika jezi ya Sunderland baada ya kusajiliwa.
Emmanuel Eboue amefungiwa mwaka mmoja na FIFA hadi hapo atakapomlipa wakala wake wa zam

Pamoja na hayo, Eboue anaweza kurejeshwa kikosini Sunderland iwapo atamalizana na wakala wake kwa kulipa deni hilo ndani ya wiki mbili zijazo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni