Waziri wa maendeleo ya nyumba na makazi,William Lukuvi amesema atahakikisha wananchi maskini wanapata haki zao za kumiliki ardhi pamoja na kuwawezesha kuwa na makazi bora ya kuishi na kuwashughulikia wale wote wanaotumika kama mawakala na kudhulumu maeneo yao.
Aidha ametoa siku saba kwa Mkurugenzi wa Wizara hiyo kuainisha utaratibu wa namna ya kuwawezesha wananchi hao kujenga nyumba bora za kuishi la sivyo atambadilisha kazi na kumuweka mtu mwingine ili aweze kutekeleza suala hilo ambalo ni agizo toka kwa Rais.John Magufuli na lipo kwenye ilani yao ya Chama.
Ameyasema hayo leo
alipokuwa akizungumza na Wakuu wa Idara mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi
na Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Alphayo Kidata,na kusema kuwa sasa yeye ni mtu mpya
,katika awamu mpya na mambo yake ni mapya hivyo wajipange katika kwenda na kasi
yake mpya.
“Ninataka kumwambia Mkurugenzi wa nyumba na makazi kuwa
ilani yetu inataka ujenzi nyumba bora za wananchi na KUWA suala hili haliwezi kufanywa na shirika la nyumba
(NHC)pekee,sera yetu inataka kila mwananchi awe na nyumba bora ya kuishi hivyo
ifikapo Jumatatu asubuhi nataka kusikia mikakati ya kumuwezesha hata kama ni
kwa kupunguzia bei ya vifaa kutokana na kuwa hawawezi kufanya hivyo bila mchago
wa Serikali kwani hatuwezi kuvumilia kuona wakiendelea kuishi kwenye nyumba za nyasi,”alisema Lukuvi.
Pia amesema atahakikisha kuwa kila mwananchi anamilikishwa
kipande chake cha ardhi kihalali na kuwa
uwezeshaji wao hautawezekana bila kuwa na hati ya umiliki ya ardhi sambamba na kuchunguza
ardhi walizopewa wawekezaji kama zimetumika kihalali na kwa matumizi
yaliyodhamiriwa au kinyume chake na kuwanyang’anya na pia kuwatayamilikisha
maeneo ambayo hayajaendelezwa.
“Tutakwenda kuangalia maeneo ya wawekezaji ili kujua kama ardhi
walizopewa wamezitumia kwa matumizi waliyoombea au wamezitumia kupata fedha
benki na kuzifanyia shughuli nyingine,ninataka kupata taarifa za mashamba na
meneo makubwa yaliyofutwa ili tuweze kudhibiti hili,”alisema.
Lukuvi amesema anataka kuwa na chombo katika Wizara yake
ambacho kitasaidia katika kudhibiti na kusimamia ujenzi wa nyumba za kibiashara
(real estate)kutokana na kumekuwa na watu wengi ambao wamekuwa wakijenga nyumba
na kuzipangisha bila kulipia kodi .
Pia amesema kuwa atakutana na watumishi wa Wizara hiyo kutoka idara zote nchini ili
kupata taarifa za fedha zilizokusanywa
tangu tarehe 1mwezi wa saba tangu pale bajeti ilipoanza na kuwa kwa lengo la
kujua jinsi zilivyotumika.
“Kutakuwa na kikao cha wakuu wa idara wote waliopo hapa na
mikoani pamoja na makamishna wa kanda watakuwepo na ninataka nipate taarifa za
fedha kuanzia tarehe 1/07mpaka leo yaani fedha mlizopata, mlizokusanya na
matumizi yake na pia kazi zilizofanywa na
serikali kipindi hicho baada ya bajeti kuanza ,kazi zilizofanywa na wizar hii
pamoja na vitengo vyake kote nchini lakini pia nipate taarifa za kila mkuu wa
idara malengo yake ya mwaka huu wa fedha yalikuwa yapi na mangapi
ameshayatekeleza,”alisema Lukuvi.
“Lakini pia ninataka nipewe utaratibu tuliouweka kuhusu
kendeleza fukwe za oysterbay ili wale waliovamia na kujenga maghorofa tujue
wanaondoka lini nataka Murugenzi wa mipango miji pamija na manispaa ya
kinondoni kunipa taarifa hizo mapema kwani hizo ni fukwe kwa ajili ya wananchi
na Rais.Magufuli alishtoa tamko,”alisisitiza.
Naye Naibu Waziri wa
wizara hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela,Angela Mabula ,amemshukuru
Rais.Magufuli kwa kuwaamini na kuwa watafanya kazi kwa kushirikiana katika
kutetea haki za wanyonge na kuhakikisha wanapata haki zao za ardhi na
kuwashgulikia watakaohusika na kuwadhulumu bila kujali nafasi zao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni