Kawaida watoto wa kiume na wa kike
wanapofikisha umri wa kubalehe ma kuelekea utu uzima ,dalili mbalimbali huanza
kujitokeza ikiwemo kuota nywele sehemu mbalimbali za mwili kama kwapani na
sehemu za siri ,chunusi usoni,sauti kubadilika na kuwa nzito kwa wavulana na nyororo kwa wasichana.
Balehe ni jumla ya mabadiliko yote
ya kimwili,kimawazo na kihisia yanayowatokea vijana wote wa kiume na wa kike
wanapotoka utotoni na kuingia utu uzima .Kwa mfano misuli ya wavulana hujengeka
na kifua kupanuka wakati matiti ya wanawake hukua zaidi.
Kutokana na asili katika uumbaji
pamoja na ambavyo sisi wanadamu tumezoea kuona, ni kwamba ni jambo la kawaida
kwa mwanaume kuota ndevu,endapo ndevu zitaonekana zimeota kwa mwanamke
basi watu huanza kujiuliza ni kwa nini
na wengine kuwa mitazamo tofauti juu ya mwanamke huyu ambaye ameota ndevu.
Baadhi yao humckulia mwanamke huyu
kama ni mchafu na kumuona kuwa ni asiyejipenda na mitazamo mingine ya tofauti
ambayo kwa kiasi fulani huwaathiri kisaikolojia na kujiona ni tofauti na
wanawake wengine hasa pale anapojikuta akinyooshewa vidole na baadhi ya watu
hata kumcheka.
Wasichana wanapoota ndevu nyingi
hukabiliwa na changamoto za kisaikolojia na ulimbwende. Mitazamo na mila nyingi
za kijamii katika bara la Afrika, bado zinakumbatia unyanyapaa wa wazi au wa
kificho kwa wasichana wanaoota ndevu nyingi mfano,wanaume wengi hawapendi kuoa
wanawake wa aina hiyo kwa kigezo kuwa hawana muonekano huku wengine wakidhani
ni aibu kuwatambulisha mbele ya marafiki zao kama wafanyavyo wapenzi.
Msichana mwenye ndevu nyingi anavuta hisia na
macho ya watu wengi yaani wanaume na wanawake pia kiasi cha kumtazama kwa namna ya kumshangaa na wengine kumkejeli
kwa kumtania na kumtungia majina ya kumdhihaki kama vile “jike dume”hali ambayo
inamnyongonyesha na kumnyima raha.
Katika hali ya kawaida msichana
anatazamiwa asiwe na nywele nyingi kwenye kidevu, juu ya mdomo wake, kifuani,
tumboni na mgongoni. Na hata akiwa nazo basi ziwe malaika zisizokuwa na rangi
nyeusi iliyokolea na kuwa ngumu kama za mwanaume.
Mwanamke anapokuwa na nywele nyingi
sehemu hizo humaanisha kuwepo kwa hitilafu za kijenetiki au dosari za
ulinganifu wa vichocheo vya jinsia mwilini mwake.
Kwa mujibu wa Dkt.Kalegamye Mlondo ,
tatizo la mwanamke kuwa na nywele nyingi mwilini kitaalamu hujulikana kama
“hirsutism”.
Huu ni ugonjwa ambao wanawake
wanaota manyoya sehemu ambazo kikawaida wao hua hawaoti manyoya maeneo hayo
mfano ndevu kidevuni, manyoya kifuani, usoni na mgongoni.
Pia mtawanyiko wa nywele mwilini
huwa kama wa kiume, mbali na ndevu pia
mwanamke huota nywele kifuani, tumboni, mapajani, mgongoni, miguuni na mikononi
kwa wingi. Wengine huota nywele nyingi kwenye makalio na kuzunguka sehemu ya
njia ya haja kubwa.
Kikawaida wingi wa manyoya mwilini
mwa binadamu hutegemea sana vimelea vya ukoo husika, kitaalamu kama genetics
make up lakini mwanamke anapokua na manyoya mengi kama ya mwanaume hasa ndevu
kuna mambo makuu mawili kwamba anaumwa au ukoo wake uko hivyo japokua
waathirika wengi wa shida hii ni wagonjwa.
Lakini pia mwanamke anapobalehe na
kuvunja ungo mwili huanza kutengeneza homoni za kiume na za kike kwa wingi ndio
maana manyoya huota kwapani na maeneo ya uke hivyo homoni za kiume zikiwa
nyingi kitaalamu kama adrogens mwanamke hupata hali hii ya kuota manyoya sehemu
ambazo hazihusiki.
Pamoja na hayo lakini pia ugonjwa
huu unatokana na vyanzo vingi kama, Matumizi ya dawa na vipodozi vyenye
kemikali: hii ndio chanzo kikuu cha wanawake wengi kuota ndevu na
manyoya hasa kwa kundekeza tabia ya
kutumia dawa xenye kemikali bila kupata maelekezo ya daktari,siku hizi kuna maduka ya
urembo yanauza dawa hizi na kuzigeuza dawa za urembo wakati ni hatari sana kiafya kwa watumiaji. Kuna dawa
kitaalamu zinaitwa steroids huingilia mfumo wa kiungo kinachohusika na
utengenezaji wa homoni (adrenal gland) hivyo zikitumika kwa muda mrefu huleta
manyoya ambayo sio ya kawaida kwa wanawake mfano vidonge vya predinisolone na
cream, sonaderm, candiderm,gentaline c, na dawa zingine zenye mchanganyiko huu ambazo
ziko nyingi ila zimetofautishwa kwa majina na viwanda.
Polycystic ovary syndrome: huu ni ugonjwa unaotokana na kutokuwa na uwiano sawa wa
homoni za mwanamke kitaalamu kama homornal imbalance hivyo mwanamke hupata
mzunguko wa damu ambao sio wa kawaida, kua mgumba, kunenepa na kupata uvimbe kadhaa kwenye ovari
za kutengeneza mayai yake.
Uvimbe unaotokana kansa:kansa kwenye kiungo kilichopo juu ya figo(adrenal gland)
huongeza wingi wa homoni hizi kwenye mfumo wa binadamu na kuleta ndevu na
manyoya magumu ya mwili.
Congenital adrenal hyperplasia: huu ni ugonjwa wa adrenal gland ambao mtu huzaliwa nao na
kuanza kutoa homoni nyingi za uzazi na matokeo yake mtu huota ndevu na manyoya
mengi mwilini.
Cushing syndrome: hali hii hutokea baada ya mgonjwa kupata matibabu ya dawa
zenye homoni ya cortisol mwilini mwake
kwa muda mrefu. Mfano matumizi ya dawa ya prednisolone vidonge kwa wagonjwa wa allergy na asthma.
Wakati mwingine ugonjwa huu hutokea
bila sababu yeyote hasa kwa jamii za kiarabu na kihindi.
Hata hivyo mwanamke anapopata tatizo
hili la ndevu dalili mbalimbali huanza kujitokeza ikiwa ni pamoja na kuota chunusi nyingi.
Kutokupata damu ya hedhi kama kawaida.
Wakati mwingine msichana hupata damu pungufu sana, kutoiona kabisa au kupata
hedhi yake bila mpangilio maalumu.
Kusinyaa kwa matiti na mfuko wa mji wa mimba.
Kuwa na sauti nzito wakati mwingine
kisanduku cha sauti (Adam’s apple) hunenepa kama cha wanaume lakini pia kuongezeka
kwa ukubwa wa kinembe kuliko kawaida (enlargement of the clitoris).
Unaweza kutumia njia mbalimbali
kupambana na tatizo hili pia ni vizuri
zaidi kutafuta chanzo cha ugonjwa ili kuanza matibabu sahihi.Endapo chanzo
hakionekani dawa zifuatazo zinaweza kutumika kupunguza tatizo hilo.
malt maca: hivi ni virutubisho vinavyotengenezwa kiasili na husaidia
sana kupanga homoni za uzazi katika hali ya kawaida na vimesaidia wengi,
hupatikana kwa wasambazaji maalumu.
Spironolactone: hizi hutumika
kuzuia homoni zinazosababisha manyoya izingatiwe kuwa dawa hizi zinasababisha madhara kwa kiwango
kikubwa kwa mtoto kama ikitokea ukibeba
mimba hivyo wakati unaendelea na
dozi hiyo hakikisha unatumia uzazi wa mpango.
Eflornithine:hii ni dawa ya
maalum ya kupaka ambayo kitaalamu hutumika kwa kupaka maeneo yalioathirika
na nywele nyingi kwani huzuia kasi ya kukua lakini hazitoi manyoya yaliyopo.
Electrolysis: hii
inahusisha kuweka sindano ndogo maalumu
kwa kila shimo la unywele na kuharibu chanzo chake ni moja ya matibabu mazuri
ila ina maumivu makali sana na dawa za nganzi za kupakwa hutumika kupunguza
maumivu hayo.
Pia unaweza kutumia Veet
Cream;ambayo inasaidia sana hasa ukipaka mara kwa mara yenyewe hunyoa manyoya
yote japokua haimalizi kabisa tatizo la kuota nywele.
Itambulike kuwa kuwa ndevu sio
ulemavu wala sio ajabu kinachotakiwa ni usafi kwa msichana mwenye tatizo kama
hilo yaani asiziache zikajaa na kurefukakama za mwanaume cha kufanya ni
kujitahidi kuzikata au kuzinyoa kila zinapojitokeza.Hapa unaweza kutumia vifaa
kama wembe,mkasi au cream maalum za kuondoa.
Achana na imani potofu za watu kuwa
ukizinyoa ndevu zinazidi kuota jambo hilo halina ukweli wowote.Hata hivyo ni bora kujiepusha au kuachana kabisa na matumizi ya
vipodozi vyenye viambato vya dawa za zinazosababisha madhara kwenye ngozi.
Ndevu zising’olewe kwa vidole, hii
inaweza kusababisha uambukizo wa bakteria katika ngozi kwa urahisi na kuleta
matatizo ya kiafya.
Wasichana waepuke matumizi ya dawa zenye steroid bila kupata ushauri wa kitaalamu
toka kwa wahudumu wa afya na maswala ya tiba.
Endapo
nywele zimetapakaa kwa wingi miguuni na mikononi na kuleta muonekano wa kiume
ni bora kuvaa nguo ndefu zinazofunika mwili vizuri ili kuepuka msongo wa
kisaikolojia ambao unaweza kutokea kutokana na mtazamo hasi wa kijamii.
Vilevile jifunze kupambana na hisia usikubali mitazamo ya watu ikakufanya
usijiamini kama msichana aliyekamili wakati wote jivunie kuwa msichana.
Mara zote serikali imekua ikipiga
marufuku baadhi ya vipodozi na kuvichoma moto lakini watu wanahisi wanaonewa na
kuvitafuta kwa magendo,tena wanaishi huku wakiamini vipodozi hivyo huwafanya
waonekane warembo zaidi bila kujua madhara wanayoweza kuyapata ni makubwa na
gharama kuyatibu.
hii elimu ni nzuri ungeiendeleza ikawa makala ndefu kdogo uelimishe
JibuFutanimeiona ikiwa ni ndefu ni nzuri sana keep it up
JibuFutaI real appreciate your advice to lads the other thing to emphasize is on the genetic makerup. Most of the rural women who are not much exposed to diff.cosmetics it has observed that inheritance is the rootcause of their beads and other abnormal hairs on their body.Yet if happen let them keep on removing them as it may destort their minds because of being diff.from their fellow women.
JibuFutaThanks
Asante sana nimeelewa maana mimi ni muhanga wa tatizo ilo
JibuFutaAsante Sanaa kwa Elimu hiyo na Mimi Ni mhanga wa hili janga
JibuFutaAsantee Sana maahiyo ndoshida yanguu kubwa
JibuFutaNahitaj sababu ya kutokutoa ndevu kwa wanaume je nini tatizo na lipi lifanyike ilibziote na je kunamadhara yoyote mwanaume asipokuwa na ndevu?
JibuFutaNi nzuri, nilikuwa naomba makala hii iwafikie wahanga wa hili jambo
JibuFutaDawa ya kuzuia ndevu kwa wanawake tafadhar
JibuFuta