Kamanda wa Kikosi cha
Usalama Barabarani,DCP  Mohamed Mpinga, akisalimiana na Mabalozi
wa Usalama Barabarani, muda mfupi kabla ya kuzindua Operesheni ijulikanayo kwa
jina la “Paza Sauti” yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa
mara wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni
hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Kamanda  wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed
 Mpinga, akitoa maelekezo ndani ya moja ya basi
linalofanya safari  zake mkoani wakati
wa  kuzindua  wa Operesheni Paza Sauti yenye lengo la
kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona  viashiria 
vya uvunjifu wa sheria za  barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa 
jijini
Dar es Salaam leo.
 Wadau wanaotumia  usafiri wa barabara, wakiwemo madereva na
abiria wakimsikiliza Kamanda wa
Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga(hayupo pichani) alipozindua  Operesheni Paza Sauti, yenye lengo la
kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa 
wanapoona kuna viashiria vya  uvunjifu wa sheria za barabarani,Operesheni
hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Tuzo na Matukio wa Mabalozi wa Usalama Barabarani,Jackson
Kalikumtima(kulia), akitoa elimu kuhusiana na Operesheni ya Paza Sauti
kwa mmoja wa wadau wanaotumia  usafiri wa
barabara, Operesheni hii ilizinduliwa Stendi ya Mabasi yaendayo mikoani ya
Ubungo, jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Mambo ya Ndani ya Nchi)
 




 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni