Jumamosi, 28 Novemba 2015

TATIZO LA KUOTA NDEVU KWA WANAWAKE

Kawaida watoto wa kiume na wa kike wanapofikisha umri wa kubalehe ma kuelekea utu uzima ,dalili mbalimbali huanza kujitokeza ikiwemo kuota nywele sehemu mbalimbali za mwili kama kwapani na sehemu za siri ,chunusi usoni,sauti kubadilika na kuwa nzito kwa wavulana na nyororo  kwa wasichana.

Ijumaa, 27 Novemba 2015

KAMANDA MPINGA AZINDUA OPARESHENI YA PAZA SAUTI DAR

 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,DCP  Mohamed Mpinga, akisalimiana na Mabalozi wa Usalama Barabarani, muda mfupi kabla ya kuzindua Operesheni ijulikanayo kwa jina la “Paza Sauti” yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.

MAHAKAMA KUU TANZANIA KUFUNGUA NJIA KWA WAANDISHI WA HABARI



JAJI  kiongozi wa Mahakama kuu ya Tanzania Shaaban Lila amesema kuwa majaji wa Tanzania wanabusara katika kufanya maamuzi yao na ndio maana hata vyombo vya habari nchini hata vinapowachafua hawaangaiki kufikisha kwenye vyombo vya dola.

ALIYEKUWA MGURUGENZI MSAIDIZI WA SHUGHULI ZA BUNGE BI.HELLEN MBEBA AFARIKI

Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah, anasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wa Bunge, Bi. Hellen Stephen Mbeba (36), aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi-Shughuli za Bunge, kilichotokea ghafla leo Ijumaa tarehe 27/11/2015 wakati akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu..

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI,AWAVUA GAMBA BAADHI YA MAAFISA TRA



Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi maofisa watano na watumishi watatu wa mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)kutokana na upotevu wa makontena
349 yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni 80.