Serikali yawashukuru wadau wa michezo kwa kushiriki katika maendeleo ya michezo nchini.
Picha/Habari na Raymond Mushumbusi
………………………………………………………………………………………………………….
Serikali imewashukuru wadau wa michezo nchini kwa kujitokeza na kuwa mstari wa mbele kushiriki
na kudhamini michezo mbalimbali nchini.
na kudhamini michezo mbalimbali nchini.
Shukrani
hizo zimetolewa leo na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa akizungumza na wanamichezo
wanaokwenda kushiriki mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016
yanayofanyika Jijini Rio dejaneiro nchini Brazil.
Mhe.
Anastazia Wambura amesema kuwa wadau wa michezo wamekuwa wakishirikiana
na Serikali sio katika suala la michezo pekee hata katika habari na
Sanaa na amewapongeza kampuni ya ving’amuzi ya Multichoice Tanzania
(DSTV) na Bodi ya Utalii katika azma yao ya kuunga mkono maendeleo ya
sera ya michezo nchini.
“Napenda
kuwashukuru wadau wetu Dstv na Bodi ya Utalii, nawapongeza kwa kuona
fursa hii muhimu na kuitumia kuwatia moyo wawakilishi wa nchi yetu
katika michezo ya Olimpiki kwa mwaka 2016 mueendelee kuiunga mkono
Serikali katika kutekeleza sera ya maendeleo ya Michezo ili kufikia
malengo” alisema Mhe. Anastazia.
Aidha
amewataka wawakilishi wa Olimpiki kutumia fursa hii ya wadau wa michezo
waliojitokeza kuwaunga mkono ikiwemo Bodi ya Utalii kutangaza utalii wa
Tanzania kwa mataifa mengine watakayo kutana nayo katika mashindano
ya Olimpiki nchini Brazil.
ya Olimpiki nchini Brazil.
Kwa
upande wake Mkurungezi Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw.Maharage Chande
ameishukuru Serikali kwa kuwapa fursa ya kushirikiana na timu ya
Olimpiki kuitangaza michezo na kuitangaza Tanzania kimataifa na kuahidi
kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza michezo nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni