Kampeni ya kuwania kujishindia malori ya konyagi yazidi kushika kasi

Meneja Chapa wa Konyagi Martha Bangu akiongea na mawakala katika hafla ya uzinduzi wa kampeni mkoani Arusha

Baadhi ya mawakala na wafanyakazi wa TDL wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa kampeni mjini Arusha

Maofisa wa TDL katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Arusha
…………………………………………………………………………..
Kampeni ya kuwania kujishindia
malori ya usambazaji iliyolenga kuwanufaisha mawakala wa kampuni ya
Tanzania Distilleries kupitia kampeni inayojulikana kama
“Nunua,Uza,Shinda na Konyagi inazidi kushika kasi kadri muda wake wa
kumalizika unavyosogea ambapo mawakala wanaendelea kuchuana kuuza bidhaa
za kampuni kwa ajili ya kufikia lengo lililowekwa ili waweze kushiriki
kwenye droo ya kupata washindi itakayofanyika mapema mwezi Oktoba.
Kampeni hiyo ambayo imewalenga
wasambazaji katika mikoa yote nchini itawawezesha washindi 2
kujishindia kila mmoja lori aina ya Eicher yenye uzito wa tani 3 na
pia katika kipindi hiki cha kampeni wanaendelea kujipatia zawadi
mbalimbali.
Akiongelea maendeleo ya kampeni
hii baada ya kukamilika zoezi la uzinduzi wake kwenye kanda za mikoa
mbalimbali,Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group,George Kavishe,alisema
kuwa mwitikio wa mawakala katika kushiriki ni mzuri kinachosubiriwa ni
washindi wawili kujinyakulia malori ya kuwarahisishia zoezi la
usambazaji na biashara zao kwa ujumla.
“Natoa wito kwa mawakala wetu
kuendelea kushiriki katika kampeni hii na kufikisha malengo ya kuingia
kwenye droo kwa kuwa imeandaliwa kwa ajili yao kwa ajili ya kuwawezesha
na tunachosubiri ni kuona magari haya yatachukuliwa na wasambazaji
kutoka kanda gani.
Kavishe alisema lengo kubwa la
kampeni hii ambayo imesifiwa na wasambazaji wa vinywaji vya kampuni hiyo
kutokana na kuwa na zawadi kubwa ni kuwainua kibiashara wasambazaji wa
bidhaa za kampuni ikiwemo kuwapatia motisha kutokana na kushirikiana na
kampuni kibiashara.
“TBL Group tunazo Programu
mbalimbali za kuwezesha wateja wetu na ndio maana tumekuwa tukiandaa
promosheni mbalimbali zenye lengo la kuwainua kimaisha ikiwemo kuwapatia
mafunzo mbalimbali ya mbinu za kufanya biashara kwa mafanikio”.Alisema
Alisema kampeni itadumu kwa
kipindi cha wiki 12 na wasambazaji wanaoshiriki wamewekewa viwango vya
mauzo; na washiriki wote watakaofikia vigezo wataingia kwenye droo kubwa
ya kupata mshindi mwezi Oktoba mwaka huu . “Tunaamini kabisa kampeni
hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao watoongezea chachu ya
manunuzi ya bidhaa zetu”.Alisema.
Baadhi ya mawakala wamepongeza
jitihada za kampuni kutenga zawadi kubwa za promosheni ambazo
zitawawezesha washindi kurahisisha biashara zao badala ya zawadi
ndogondogo zisizoweza kumwinua kimaisha mshiriki.
Mmoja wa wauzaji wa bidhaa ya
Konyagi kanda ya Kusini aliyejitambulisha kama Saimon Haule amesema kuwa
japo sio mawakala wote watapata malori lakini watakaobahatika kushinda
watakuwa wamepata zawadi ya uhakika na inayofanikisha biashara kukua.
“Kampeni hii ya Konyagi ni kubwa cha muhimu ni kukidhi vigezo vya
kuingia kwenye droo ya kumpata mshindi “.Alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni