MAAMUZI YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) KUHUSIANA NA KUFUTA UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU WILAYA YA KINONDONI (KIFA)

Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Dar es Salaam baada ya kupitia KATIBA na KANUNI za TFF, DRFA, na KIFA
kimejiridhisha kwamba maamuzi yaliyofanywa na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) ya kufuta matokeo halali ya uchaguzi wa Chama Cha
Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni uliofanyika siku ya Jumapili tarehe
12/06/2016 katika bwalo la maofisa wa polisi Oysterbay bila
hayakuzingatia KATIBA na KANUNI za TFF, DRFA na KIFA.
Maamuzi hayo ya TFF yamevunja
katiba ya TFF, DRFA na KIFA pamoja na kanuni zake ambazo ndiyo mwongozo
wa mpira wetu hasa katika upatikanaji wa mamlaka za uendeshaji wa mpira
katika ngazi mbalimbali za taifa, mkoa na wilaya.
Katiba ya TFF ibara ya 52(2) na
ibara ya 52(6)(a) zinaeleza wazi kazi na majukumu ya kamati ya uchaguzi
ya TFF ni kwa chaguzi za TFF na wanachama wake ambao ni vyama vya
mikoa, vilabu vya ligi kuu na kusimamia uchaguzi wa Board ya ligi pamoja
na kuishauri kamati ya utendaji mambo yanayo husiana na chaguzi hizo.
Kwa mujibu wa katiba ya TFF ya
2013 kamati yake ya uchaguzi haiwajibiki na lolote kwa vyama vya mpira
wa miguu vya wilaya ambao si wanachama wa TFF. Lakini pia Ibara ya 3(i)
ya kanuni za uchaguzi za TFF za 2013 inaeleza kuwa kamati ya uchaguzi ya
TFF itaendesha na kusimamia uchaguzi wa TFF na Bodi ya Ligi.
Ibara ya 6 ya kanuni za
uchaguzi za TFF za 2013 pia inaeleza majukumu ya kamati ya uchaguzi na
katika majukumu yake hakuna popote inapoonyesha kuwa ina mamlaka ya
kusimamia na kutolea maamuzi chaguzi za vyama vya mpira wa miguu vya
wilaya ambao si wanachama wa TFF.
Kwa mujibu wa Katiba ya KIFA
ibara ya 47 na kanuni za uchaguzi kipengele (b) inasema Kamati ya
Uchaguzi ya KIFA itafanya kazi kwa kushirikiana na sekretarieti ya Chama
na chini ya uangalizi na Miongozo ya Kamati ya Uchaguzi ya DRFA.
Kwahiyo ni jukumu la kamati ya uchaguzi ya DRFA kuhakikisha uchaguzi
unakuwa huru na haki.
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kwa kugundua kwamba Kamati yake ya Uchaguzi haina mamlaka
ya KIKATIBA kuweza kusimamia chaguzi za vyama vya wilaya, miongoni mwa
mapendekezo ya mabadiliko ya KATIBA waliyoleta katika Mkutano Mkuu wa
TFF wa mwisho uliofanyika Tanga ni pamoja na hilo kuuomba MKUTANO MKUU
wa TFF uweze kufanya hilo badiliko ili waweze kusimamia chaguzi za
WILAYA lakini BAHATI mbaya marekebisho ya KATIBA hayakuweza kupitishwa
na wajumbe wa MKUTANO Mkuu.
Katiba ya KIFA katika kanuni
zake za uchaguzi 5 (h) inatamka kwamba RUFAA zote zihusuzo uchaguzi
zitawasilishwa kwenye kamati ya RUFAA ya Wilaya na hatimae kama Mrufani
hakuridhika basi atakata RUFAA katika kamati ya RUFAA ya Mkoa ambapo
uamuzi wake utakuwa ndio wa MWISHO.
Baada ya Mwenyekiti wa Kamati
ya Uchaguzi ya KIFA kutangaza matokeo ya uchaguzi huo tajwa hapo juu na
kutuletea ripoti yake, mmoja wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti Bwana
Thomas Mazanda aliamua kukata RUFAA katika Kamati ya uchaguzi ya Chama
Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kama katiba ya KIFA
inavyoelekeza KUPINGA matokeo yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya
uchaguzi wa KIFA. Lakini cha kushangaza wakati kamati ya uchaguzi ya
DRFA ikipanga kusikiliza RUFAA hiyo Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) likaitisha kikao 18/06/2016 na kuamua KUFUTA uchaguzi huo
bila kufuata taratibu za KIKATIBA na KIKANUNI zinazotuongoza.
Kamati ya Uchaguzi ya Chama Cha
Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni kwa mujibu wa Ibara ya 47 inaundwa
na wajumbe watano. Wajumbe wa kamati hii watateuliwa na Mwenyekiti. Na
Mwenyekiti wa kamati hii lazima awe ni mwanasheria na wajumbe wengine
wane lazima wawe ni watu wenye ujuzi na upeo katika masuala ya michezo.
Kwa mujibu wa katiba ya KIFA haina makamu mwenyekiti wala katibu wa
kamati. Na maadam KATIBA inatamka wazi Mwenyekiti lazima awe mwanasheria
TAFSIRI yake ni kwamba bila uwepo wa Mwenyekiti kamati haiwezi
kuendelea na kazi zake kwa sababu ukiondoa Mwenyekiti wajumbe wengine
waliobaki wa kamati ya KIFA hawana taaluma ya SHERIA.
Continue reading →
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni