Utafiti wa malaria kuokoa maisha ya Watanzania.
By Newsroom on May 13, 2016


Waandishi
wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani wakiwa
tayari wamewasili Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)
kituo cha Korogwe.
Mtaalamu
wa utafiti katika Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)
kituo cha Korogwe Dkt. Daniel Minja akifafanua jambo kwa baadhi ya
waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini
Marekani walipotembelea kituoni hapo kujionea namna Tanzania
inavyopambana na ugonjwa wa malaria.
Waandishi
wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini Marekani
wakimsikiliza Mtaalamu wa utafiti katika Kituo cha Utafiti wa Magonjwa
ya Binadamu (NIMR) kituo cha Korogwe Dkt. Daniel Minja (hayupo pichani)
walipotembelea kituoni hapo kujionea namna Tanzania inavyopambana na
ugonjwa wa malaria.
Familia
ya Salumu Rashidi wa kijiji cha Masatu kilichopo wilaya ya Korogwe
mkoani Tanga wakiwa na mtoto wao Mohammedi Salimu ambaye ni miongoni mwa
watoto waliopo kwenye mradi wa kudhibiti malaria wilayani huo. Kushoto
ni mama yake Mohammedi Monica Mugunda.
Vijana
wa Jeshi la Kujenga Taifa, (JKT) wakitumbuiza wakati wa zaira ya
waandishi wa habari kutoka Taasisi ya “Malaria No More” ya nchini
Marekani walipotembelea zahanati ya Mgambo inayomilikiwa na JKT iliyopo
mkoani Tanga kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa wa
malaria.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Tanga)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni