MeTL YAKANUSHA KUFICHA SUKARI, YAELEZA HALI HALISI

Kampuni
ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imekanusha taarifa
ambayo ilitolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa kampuni hiyo
imeficha sukari tani 2,990 katika Bandari Kavu (ICD) ya PMM iliyopo
Vingunguti, Dar es Salaam.
Taarifa
hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
kutembelea ICD na kukuta tani 2,990 ambazo aliambiwa kuwa ni mali ya
Mohammed Enterprises jambo ambalo halikuwa na usahihi bali ni mali ya
Tanzania Commodities Trading inayomilikiwa na Murtaza Dewji.
Kwaa
mujibu wa Murtaza Dewji ambaye ndiyo mmiliki wa sukari hiyo amesema kuwa
sukari hiyo iliingia nchini kwa kufata utaratibu wote kama jinsi
inavyotakiwa na anashangazwa kwanini hakufatwa ili kutoa maelezo kuhusu
sukari hiyo.
“Tulifuata
taratibu zote zikiwepo mamlaka husika za nchi kma bodi ya sukari,
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na vyombo vyote vya ulinzi na
usalama,” amesema Murtaza.
Akifafanua
zaidi amesema kuwa sukari hiyo ilikuwa njiani kuelekea nchini Uganda na
vielelezo vyote vipo lakini kutokana na uhaba wa sukari nchini,
serikali iliagiza mzigo huo kubaki nchini na kuingiza sokoni ili
kumaliza tatizo hilo ambapo ulitakiwa kuanza kuingia sokoni kati ya Mei,
12 na Mei, 13.
Aidha
ameelezea kuwa ni jambo la kawaida kuagiza sukari kutoka Dubai kwani
hutumia siku 7 pekee kufika nchini tofauti na sukari kutoka Brazil
ambayo hutumia siku 50 hadi 60 ikiwa njiani hadi kufika nchini.
“Wafanyabiashara
wote wanaojua biashara walioko karibu na Dubai hufanya hivyo na sisi
sio wa kwanza kuagiza sukari kutoka kwa wauzaji wa Dubai,” amesema
Murtaza.
Pia
Murtaza amewatoa hofu Watanzania kuhusu uhaba wa sukari kwa kusema kuwa
tayari sukari imeagizwa na ndani ya wiki mbili kutakuwa na sukari ya
uhakika nchini hivyo kuwataka kuondoa hofu iliyokuwapo hapo awali
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni